08-Swahiyh Fiqh As-Sunnah: Kitabu Cha Ndoa: Posa Na Hukumu Zake:Ikiwa Mtu Ataposa Juu Ya Posa Ya Mwingine Kisha Akamwoa Mwanamke, Je, Itaswihi Ndoa?

 

Swahiyh Fiqh As-Sunnah

 

كِتَابُ الزَّوَاجِ

 

Kitabu Cha Ndoa

 

 

الخِطْبَةُ وأَحْكَامُهَا

 

Posa Na Hukumu Zake

 

 

Alhidaaya.com

 

 

 

08: Ikiwa Mtu Ataposa Juu Ya Posa Ya Mwingine Kisha Akamwoa Mwanamke, Je, Itaswihi Ndoa?

 

Tumeshasema kwamba mtu kuposa juu ya posa ya nduguye ni haramu.  Sasa ikiwa mposaji wa pili atamwoa mwanamke badala ya mposaji wa kwanza, hapa ‘Ulamaa wana kauli mbili:

 

Kauli ya kwanza: 

 

Ndoa hii ni batili, ni lazima waachanishwe.  Ni chaguo la Sheikh wa Uislamu ambaye amesema kwamba katazo linaonyesha kuwa kilichokatazwa madhara yake ni makubwa kuliko maslaha yake. 

 

Kauli ya pili:

 

Ndoa ni sahihi, lakini mwoaji huyo anakuwa ni mwasi na anapata madhambi.  Haya ni madhehebu ya Jumhuwr.  Wanasema kwamba hakuna mafungamano kati ya uharamu wa posa juu ya posa na kuswihi kwa ndoa ya mposaji wa pili, na kwamba posa si sehemu ya ‘aqdi ya ndoa, na ndoa inaswihi hata bila posa.  Isitoshe, kosa la mposaji huyo wa pili linabaki pale pale hata kama hakufunga ndoa.

 

Ninasema:  “Kauli ya Jumhuwr ina nguvu zaidi”. 

 

 

Share