18-Swahiyh Fiqh As-Sunnah: Kitabu Cha Ndoa: Posa Na Hukumu Zake:Je, Inatosha Kuangalia Picha Ya Mchumba?

 

Swahiyh Fiqh As-Sunnah

 

كِتَابُ الزَّوَاجِ

 

Kitabu Cha Ndoa

 

 

الخِطْبَةُ وأَحْكَامُهَا

 

Posa Na Hukumu Zake

 

 

Alhidaaya.com

 

 

 

18:   Je, Inatosha Kuangalia Picha Ya Mchumba?

 

Mposaji anaruhusiwa kuangalia picha ya mchumba wake ni sawa ikiwa ni ya fotografu au video.  Hizi zinaingia kwenye ujumuishi wa dalili zenye kuhimiza kumwangalia sehemu zitakazomshawishi kumwoa.

 

Hali hii inakuja pale mwanamke anapokuwa mbali na mwanaume mchumbiaji.  Pamoja na hivyo, inabidi kuzindusha hapa kwamba utumiaji wa picha unaweza ukawa njia ya udanganyifu na ghushi.  Picha inaweza kuhadaa ikamwonyesha mwenye picha kinyume na alivyo. Na kwa mujibu wa teknolojia ya sasa, mwanamke mbaya anaweza kufanywa mzuri mrembo.  Vile vile, mtu anaweza kutumiwa picha ya mwanamke mwingine asiye yule aliyemkusudia.  Isitoshe, picha hiyo inaweza kuwafikia watu wengi na hatimaye kuwa madhara kwake na kwa familia yake.  [Rawdhwat At-Twaalibiyna (7/21) na Mughnil Muhtaaj (2/85)]

 

 

Share