19-Swahiyh Fiqh As-Sunnah: Kitabu Cha Ndoa: Posa Na Hukumu Zake:Je, Mwanamke Naye Anaruhusiwa Kumwangalia Mwanaume
Swahiyh Fiqh As-Sunnah
كِتَابُ الزَّوَاجِ
Kitabu Cha Ndoa
الخِطْبَةُ وأَحْكَامُهَا
Posa Na Hukumu Zake
19: Je, Mwanamke Naye Anaruhusiwa Kumwangalia Mwanaume?:
Hukmu ya mwanamke kumwangalia aliyemposa ni sawa na hukmu ya mwanaume kumwangalia yeye, kwa kuwa yanayompendeza kutoka kwa mwanaume ni yale yale yanayompendeza mwanaume kutoka kwake. Hili ni muhimu zaidi kwa mwanamke, kwa sababu mwanaume ana uwezo wa kumwacha mwanamke kama hakumpendeza baada ya kumwoa kinyume na mwanamke.
Hapa kiufupi tunaweza kusema kwamba sharia haikumwelekeza mwanamke kumwangalia aliyemchumbia, kwa kuwa wanaume ni rahisi kuwaona katika jamii, hawafichiki kama wanavyofichikana wanawake. Mwanamke anaweza kwa urahisi kumwona mwanaume aliyemposa. Na mpaka wa kumwangalia ni zaidi ya uso na viganja isipokuwa kati ya kitovu na magoti, sehemu hiyo ndio uchi wa mwanaume.