21-Swahiyh Fiqh As-Sunnah: Kitabu Cha Ndoa: Posa Na Hukumu Zake:Mwanaume Haruhusiwi Kumpa Mkono Mchumba Wake Wala Kumgusa Sehemu Yoyote Ya Mwili Wake

 

Swahiyh Fiqh As-Sunnah

 

كِتَابُ الزَّوَاجِ

 

Kitabu Cha Ndoa

 

 

 

الخِطْبَةُ وأَحْكَامُهَا

 

Posa Na Hukumu Zake

 

 

Alhidaaya.com

 

 

 

21:   Mwanaume Haruhusiwi Kumpa Mkono Mchumba Wake Wala Kumgusa Sehemu Yoyote Ya Mwili Wake:

 

 

Hii ni hata bila matamanio, kwa kuwa msichana anakuwa bado ni ajnabiyya kwake.   Dalili za uharamu huu ni hizi zifuatazo:

 

1-  Ma’aqal bin Yasaar:  Rasuli wa Allaah (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:

 

"لَأنْ يُطعَنَ في رأسِ رجلٍ بِمِخْيَطٍ من حديدٍ خيرٌ من أن يمَسَّ امرأةً لا تَحِلُّ له"

 

Kudungwa mtu kichwani na sindano la chuma, ni nafuu zaidi kwake kuliko kumgusa mwanamke asiye halali kwake”.  [Hadiyth Hasan.  Imechakatwa na At-Twabaraaniy katika Al-Kabiyr (30/211).  Angalia As-Swahiyhah (226)]

 

Na kwa ajili hii, Rasuli wa Allaah (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) hakuwa anawapa mkono wanawake wala kuchukua toka kwao ahadi ya utiifu kwake isipokuwa kwa maneno tu.

 

2-  ‘Aaishah (Radhwiya Allaah ‘anhaa): 

 

"كَانَ يَقُولُ للمَرْأَةِ المبَايِعَةِ: "قَدْ بَايَعْتُكِ" كَلَامًا. وقَالَتْ: وَاللَّهِ مَا مَسَّتْ يَدُهُ يَدَ امْرَأَةٍ قَطُّ فِي الْمُبَايَعَةِ، وَمَا بَايَعَهُنَّ إِلاَّ بِقَوْلِهِ‏: "قَدْ بَايَعْتُكِ"

 

“Rasuli wa Allaah (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa anamwambia kwa maneno mwanamke anayechukua toka kwake ahadi ya utiifu:  “Nimechukua ahadi yako”.  Na akasema:  Wal Laah!  Haukugusa kamwe mkono wake mkono wa mwanamke wakati wa kuchukua ahadi ya utiifu kwao isipokuwa kwa kumwambia mwanamke:  Nimechukua ahadi ya utiifu kwako juu ya hilo”.   [Hadiyth Swahiyh.  Imechakatwa na Al-Bukhaariy (2713)]

 

Na katika riwaayah aliwaambia: 

 

"إِنِّي لاَ أُصَافِحُ النِّسَاءَ"

 

“Mimi kwa hakika sipeani mikono na wanawake”.  [Swahiyh.  Imechakatwa na At-Tirmidhiy (1597), An-Nasaaiy (4181), Ibn Maajah (2874) na Ahmad (6/357)]

 

 

Share