23-Swahiyh Fiqh As-Sunnah: Kitabu Cha Ndoa: Posa Na Hukumu Zake: Pete Ya Uchumba

 

Swahiyh Fiqh As-Sunnah

 

كِتَابُ الزَّوَاجِ

 

Kitabu Cha Ndoa

 

 

 

الخِطْبَةُ وأَحْكَامُهَا

 

Posa Na Hukumu Zake

 

 

 

Alhidaaya.com

 

23:   Pete Ya Uchumba:

 

Watu siku hizi wameingia bila kujijua kwenye tabia ya kijana mposaji kumvalisha pete ya posa mchumba wake.  Ataukamata mkono wake -naye bado ni ajnabiy kwake- na kumvisha pete, na msichana naye atafanya hivyo hivyo.  Pete hiyo anayovishwa mwanaume inaweza pia kuwa ni ya dhahabu!!   Na baya zaidi, hilo linafanyika kwenye hafla yenye mvumo mkubwa huku wanaume na wanawake wakichanganyika pamoja.   Haya yote ni katika munkari mbali na kwamba katika Uislamu hakuna chochote kinachogusia posa kufanyika kwa picha hii.  Ni mambo ya kuiga yaliyoanzishwa na Mafarao au Manaswara, na kuyafanya ni sawa na kuiga kibubusa na kujifananisha na makafiri.  Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam):

 

"مَنْ تَشَبَّهَ بِقَوْمٍ فَهُوَ مِنْهُمْ"

 

“Mwenye kujifananisha na watu basi yeye ni katika wao”.  [Hadiyth Hasan.  Imechakatwa na Abu Daawuwd (4031), Ahmad (2/50) na wengineo]

 

Yote ni mamoja katika uharamu ni sawa pete ikiwa ya dhahabu au silva, lakini uharamu unakuwa ni mkubwa zaidi ikiwa ni ya dhahabu.  Allaah Ndiye Ajuaye zaidi.

 

 

 

Share