24-Swahiyh Fiqh As-Sunnah: Kitabu Cha Ndoa: Posa Na Hukumu Zake:Kuvunja Uchumba

 

Swahiyh Fiqh As-Sunnah

 

كِتَابُ الزَّوَاجِ

 

Kitabu Cha Ndoa

 

 

 

الخِطْبَةُ وأَحْكَامُهَا

 

Posa Na Hukumu Zake

 

 

 

Alhidaaya.com

 

 

 

24:   Kuvunja Uchumba:

 

Posa haimaanishi kwamba ndoa ndiyo tayari, bali ni ahadi ya kuja kufungwa ndoa, na ahadi hii sio wajibishi kwa mujibu wa kauli ya Jumhuwr ya ‘Ulamaa.  Walii wa binti halazimishwi kutekeleza ahadi hiyo baada ya kuikubali posa, na anaweza kuitengua kama ataona maslaha ya binti yake katika hilo, na hata binti pia ikiwa atamchukia mposaji.  Sababu ni kuwa ndoa ni fungamano la maisha, na kama yako madhara ndani yake, basi yatakuwa ni ya kudumu.

 

Ninasema:  “Allaah Ta’aalaa Amesema:

 

"كَبُرَ مَقْتًا عِندَ اللَّـهِ أَن تَقُولُوا مَا لَا تَفْعَلُونَ"

 

 

Ni chukizo kubwa mno mbele ya Allaah kwamba mnasema yale msiyoyafanya”.  [As-Swaff: 03]

 

 

Na katika Hadiyth ya Abu Hurayra (Radhwiya Allaah ‘anhu), Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:

 

"آيَةُ اَلْمُنَافِقِ ثَلَاثٌ: إِذَا حَدَّثَ كَذَبَ، وَإِذَا وَعَدَ أَخْلَفَ، وَإِذَا ائْتُمِنَ خَانَ"

 

“Alama za mnafiki ni tatu:  Akizungumza husema uongo, akiahidi hatekelezi, na akiaminiwa husaliti”.  [Hadiyth Swahiyh.  Imechakatwa na Al-Bukhaariy na Muslim]

 

Aayaat na Hadiyth kama hizi, ni dalili za nguvu zenye kuashiria wajibu wa kutekeleza ahadi na kutoivunja bila ya udhuru unaokubalika.

 

 

Share