26-Swahiyh Fiqh As-Sunnah: Kitabu Cha Ndoa: Posa Na Hukumu Zake: Kumfidia Aliyedhurika Kutokana Na Kuvunjika Posa

 

Swahiyh Fiqh As-Sunnah

 

كِتَابُ الزَّوَاجِ

 

Kitabu Cha Ndoa

 

 

الخِطْبَةُ وأَحْكَامُهَا

 

Posa Na Hukumu Zake

 

 

Alhidaaya.com

 

 

 

 

26:   Kumfidia Aliyedhurika Kutokana Na Kuvunjika Posa:

 

Baadhi ya wasomi wa kileo wanaona kwamba kuvunja posa kunawajibisha fidia ya fedha kama ilivyo kwa baadhi ya makundi ya Kinaswara wakati ambapo Fuqahaa hapo nyuma pamoja na kutofautiana kwao kimaoni, hawakupanga malipo yoyote ya fidia kwa upande uliosababisha posa kuvunjwa.  Na hili ndilo lililo sahihi kwa haya yafuatayo:

 

1-  Fidia inazidisha tatizo juu ya tatizo, na wala hailitatui.  Lakini pia, madhara yanayotokana na kuvunja posa yanazalikana kutokana na watu kuipa posa uzito mkubwa zaidi ya inavyostahili.  Posa ni ahadi tu, na haijuzu watu waijengee hali ambayo italeta madhara kwao.  Na gharama ambazo waposaji wanazibeba, manunuzi na mfano wa hayo kwa wachumba, ni kuharakia jambo ambalo lina wasaa na muda wa kutosha.

 

2-  Fidia inafungua mlango kwa pande zote mbili wa kulipiziana na kutiana hasara kwa nguvu na hila zote kutokana na machungu na maumivu ya rohoni.  Na idadi ya kesi kama hizi kwenye jamii zetu ni nyingi mno kuzidi uwezo wa mahakama.

 

3-  Fidia inakwenda kinyume na uhalisia wa posa ambayo ni ahadi na makubaliano ya awali ya matayarisho ya ndoa.

 

4-  Fidia inakhalifu Ijmaa ya Umma na si uadilifu.

 

5-  Inaweza kulazimisha posa kurejeshwa upya na ndoa kufungwa huku chuki ikiwa imetamalaki, na hili ni jambo la hatari kabisa.

 

 

 

Share