16-Majini: Nasaba Zao Na Nchi Zao

 

 

Majini

   

Alhidaaya.com 

 

16-  Nasaba Zao Na Nchi Zao:

 

 

 

Majini wana makabila na mataifa kama tulivyo sisi wanadamu.  Allaah Akiwazungumzia majini walioisikiliza Qur-aan toka kwa Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) Anasema:

 

"يَا قَوْمَنَا أَجِيبُوا دَاعِيَ اللَّـهِ وَآمِنُوا بِهِ يَغْفِرْ لَكُم مِّن ذُنُوبِكُمْ وَيُجِرْكُم مِّنْ عَذَابٍ أَلِيمٍ"

 

Enyi kaumu yetu!  Mwitikieni Mlinganiaji wa Allaah, na mwaminini.  (Allaah) Atakughufurieni madhambi yenu, na Atakukingeni na adhabu iumizayo”.  [Al-Ahqaaf:  31]

 

Na Anasema tena Allaah ‘Azza wa Jalla:

 

"إِنَّهُ يَرَاكُمْ هُوَ وَقَبِيلُهُ مِنْ حَيْثُ لَا تَرَوْنَهُمْ"

 

“Hakika yeye (Ibliys) anakuoneni, yeye na kabila lake (la mashaytwaan) na hali ya kuwa nyinyi hamuwaoni”.

 

Na baadhi ya majini ni raia na wakazi wa maeneo na nchi tofauti kwa mujibu wa vipimo vyao wenyewe kama tulivyo sisi wanadamu.  Kati ya hao, ni kundi la majini waliomjia Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) toka Nasibin.

 

Nasibin ulikuwa ni mji kati ya Sham na Iraki.  Inasemekana pia ulikuwa Yemen.

 

Toka kwa Abu Hurayrah (Radhwiya Allaah ‘anhu) kwamba:

 

" كانَ يَحمِلُ مَعَ النَّبيِّ صلَّى اللهُ عليه وسلَّم إدواةً لوُضوئِهِ وحاجَتِهِ، فبَينَما هوَ يَتبَعُه بها فقال: من هَذا؟ فقال: أنا أبو هُريرةَ، فقال: أبغِني أحجارًا أستَنفِضُ بها، ولا تَأتِني بعَظمٍ ولا بِرَوْثةٍ، فأتَيتُه بأحجارٍ أحمِلُها في طَرَفِ ثَوبي حَتَّى وضعْتُها إلى جَنبِهِ، ثُمَّ انصَرَفْتُ، حَتَّى إذا فرَغَ مَشَيتُ فقُلتُ: ما بالُ العَظمِ والرَّوْثةِ؟! قال: هُما من طَعَامِ الجِنِّ، وإنَّه أتاني وفدُ جِنِّ نَصيبِينَ، ونِعْمَ الجِنِّ فسَألوني الزَّادَ، فدَعَوتُ اللهَ لَهم ألَّا يَمُرُّوا بعَظمٍ ولا بِرَوثةٍ إلَّا وجَدوا عليها طعمًا"  

 

Abu Hurayrah (Radhwiya Allaah ‘anhu) ameeleza kwamba alikuwa pamoja na Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na alikuwa amembebea kiriba cha  maji yake ya kutawadhia na kustanjia.  Na wakati akiwa anamfuata nyuma akiwa na kiriba hicho, Rasuli aliuliza:  Nani huyu?  Akasema:  Mimi Abu Hurayrah.  Akamwambia:  Niletee vijiwe nipate kustanjia kwavyo, lakini usiniletee mfupa wala kinyesi cha mnyama.  Nikamletea vijiwe ambavyo nilivibeba kwenye ncha ya nguo yangu na kuviweka pembeni mwake halafu nikaondoka.  Nikasubiri hadi alipomaliza halafu nikamwendea na kumuuliza:  Imekuwaje nisikuletee mfupa au kinyesi cha mnyama?  Akasema:  Viwili hivi ni chakula cha majini.  Na kwa hakika ulinijia ujumbe wa majini wa Nasibin, ni wema walioje majini hao!  Wakaniomba chakula, nami nikawaombea kwa Allaah kwamba wasipite popote ulipo mfupa au kinyesi cha mnyama isipokuwa wapate humo chakula”[Swahiyhul Bukhaariy: 3860]

 

Sababu ya Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) kuwasifu majini hao kuwa ni wema wa majini, ni yale yaliyosimuliwa na At-Tirmidhiy toka kwa Jaabir aliyesema: 

 

"خرَج رَسولُ اللهِ صلَّى اللهُ عليه وسلَّمَ على أصْحابِه، فقَرأَ عليهم سُورةَ الرَّحمَنِ مِن أوَّلِها إلى آخِرِها، فسَكَتوا، فقال: لقد قَرأْتُها على الجِنِّ ليلةَ الجِنِّ، فكانوا أحسَنَ مَرْدودًا منكم؛ كُنتُ كلَّما أتَيْتُ على قولِه: "فَبِأَيِّ آلَاءِ رَبِّكُمَا تُكَذِّبَانِ"، قالوا: لا بشَيءٍ مِن نِعَمِكَ ربَّنا نُكذِّبُ، فلكَ الحَمدُ"

 

“Rasuli wa Allaah (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alitoka kwa Maswahaba wake akawasomea Suwrat Ar-Rahmaan kuanzia mwanzo hadi mwisho, nao wakanyamaza bila kujibu kitu.  Akawaambia:  Hakika niliwasomea majini usiku nilipokutana nao (suwrah hii), nao walijibisha vizuri sana kukushindeni nyinyi.  Nilikuwa kila nikifika kwenye Kauli Yake Ta’aalaa: 

 

"فَبِأَيِّ آلَاءِ رَبِّكُمَا تُكَذِّبَانِ"

 

Basi ni ipi katika Neema za Rabb wenu mnaweza kuikanusha?”…wao walikuwa wakijibu:  Hakuna neema yoyote kati ya neema Zako ee Rabbi wetu tunayoikanusha, na Himdi unastahiki Wewe tu”.  [Hadiyth Hasan.  Swahiyhul Jaami’i (5138)]

 

 

Share