19-Majini: Sifa Za Shaytwaan

 

 

Majini

  

 

Alhidaaya.com 

 

 

19   Sifa Za Shaytwaan

 

 

 

Shaytwaan amesifiwa katika Qur-aan kwa sifa mbaya.  Kati ya sifa hizo ni:

 

1-  Rajiym "الرَّجِيْمُ" (Aliyelaaniwa, aliyewekwa mbali na Rahma za Allaah)

 

Sifa hii imetajwa katika aayah zifuatazo:

 

"قَالَ فَاخْرُجْ مِنْهَا فَإِنَّكَ رَجِيمٌ"

 

(Allaah) Akasema:  Basi toka humo, kwani hakika wewe umetokomezwa mbali na kulaaniwa”.  [Al-Hijr: 34]

 

Hii ni baada ya Ibliys kukataa kumsujudia Aadam.

 

Anasema tena Allaah:

 

"فَإِذَا قَرَأْتَ الْقُرْآنَ فَاسْتَعِذْ بِاللَّـهِ مِنَ الشَّيْطَانِ الرَّجِيمِ"

 

Unaposoma Qur-aan basi (kwanza) omba kinga kwa Allaah dhidi ya shaytwaan aliyetokomezwa mbali na kulaaniwa.  [An-Nahl:  98]

 

Pia,

 

 "فَلَمَّا وَضَعَتْهَا قَالَتْ رَبِّ إِنِّي وَضَعْتُهَا أُنثَىٰ وَاللَّـهُ أَعْلَمُ بِمَا وَضَعَتْ وَلَيْسَ الذَّكَرُ كَالْأُنثَىٰ ۖ وَإِنِّي سَمَّيْتُهَا مَرْيَمَ وَإِنِّي أُعِيذُهَا بِكَ وَذُرِّيَّتَهَا مِنَ الشَّيْطَانِ الرَّجِيمِ"

 

“Basi alipomzaa akasema:  Rabb wangu!  Hakika mimi nimezaa mwanamke, na Allaah Anajua zaidi alichokizaa.  Na mwanamme si kama mwanamke.  Nami nimemwita Mayram, nami namkinga Kwako na dhuria wake kutokana na shaytwaan aliyetokomezwa mbali na kulaaniwa”.  [Aal-‘Imraan: 36]

 

2-  Al-Maarid "المَارِدُ" (aliyeasi)

 

Hili ni katika aayaat zifuatazo:

 

"وَحِفْظًا مِّن كُلِّ شَيْطَانٍ مَّارِدٍ"

 

Na hifadhi kutokana na kila shaytwaan asi”.  [As-Swaaffaat: 07]

 

"وَمِنَ النَّاسِ مَن يُجَادِلُ فِي اللَّـهِ بِغَيْرِ عِلْمٍ وَيَتَّبِعُ كُلَّ شَيْطَانٍ مَّرِيدٍ "

 

Na miongoni mwa watu kuna ambao wanaobishana kuhusu Allaah bila ya elimu, na wanafuata kila shaytwaan muasi”.  [Al-Hajj: 03]

 

إِن يَدْعُونَ مِن دُونِهِ إِلَّا إِنَاثًا وَإِن يَدْعُونَ إِلَّا شَيْطَانًا مَّرِيدًا

 

Hawaombi badala Yake isipokuwa miungu ya kike na hawaombi isipokuwa shaytwaan muasi”.   [An-Nisaa: 117]

 

 

Share