07-Swahiyh Fiqh As-Sunnah: Kitabu Cha Ndoa: Kufunga Ndoa: Masharti Ya Kuswihi ‘Aqdi Ya Ndoa: Sharti la Kwanza: (d) Kumlazimisha Binti Mdogo

 

Swahiyh Fiqh As-Sunnah

 

كِتَابُ الزَّوَاجِ

 

Kitabu Cha Ndoa

 

 

عَقْدُ الزَّوَاجِ

 

Kufunga Ndoa

 

 

Alhidaaya.com

 

 

 

 

 

07:  Masharti Ya Kuswihi ‘Aqdi Ya Ndoa: Sharti la Kwanza: (d) Kumlazimisha Binti Mdogo:

 

 

‘Ulamaa wamekubaliana wote -isipokuwa wachache mno- kwamba binti bikra mdogo ambaye bado hajabaleghe, inajuzu kwa baba yake kumwozesha bila ya idhini yake.  Kwa kuwa hakuna maana ya kumtaka idhini binti kama huyu ambaye hajui nini maana ya idhini yake, na ambaye pia kunyamaza kwake na kununa kwake ni sawa. 

 

Dalili yao wanasema kwamba Abu Bakr (Radhwiya Allaah ‘anhu) alimwozesha ‘Aaishah akiwa binti mdogo ambaye bado hajabaleghe.  Kadhalika, wamelichukulia neno lake Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam):

 

"وَلَا تُنْكَحُ الْبِكْرُ حَتَّى تُسْتَأْذَنَ"

 

“Na bikra haolewi mpaka atakwe idhini yake”….kwamba muradi wa bikra ambaye anatakwa idhini ni yule ambaye amebaleghe (na siye ambaye bado hajavunja ungo). 

 

Lakini, ikiwa binti huyo mdogo anajitambua na anajua nini ndoa, na anaweza kumtathmini aliyekusudia kumwoa, basi hapa ni wazi kwamba atatakwa idhini yake.  Ni kwa kuwa pia anaingia ndani ya wigo wa ujumuishi wa mabikra; haijalishi ni mdogo au mkubwa, pamoja na kuzingatia maslaha ya kumtaka mwenyewe idhini.  Allaah Ndiye Ajuaye zaidi.

 

Faida:

 

Je, Asiye Baba Anaweza Kumlazimisha Binti Mdogo?

 

Sheikh wa Uislamu ameeleza kwamba kwa mujibu wa itifaki ya ‘Ulamaa, sharia haimpi kibali mtu mwingine yeyote asiye baba au babu kumlazimisha binti mdogo.  [Majmuw’ul Fataawaa (32/57)]

 

Ninasema:  “Huenda (Sheikh wa Uislamu) anawakusudia Maimamu watatu (katika itifaki hiyo).  Kwani Abu Haniyfah na Al-Awzaa’iy wamesema kuhusiana na “thayyib” mdogo (binti mdogo aliyeshawahi kuolewa):  “Atamwozesha msimamizi wake yeyote, lakini akibaleghe, basi haki ya kujichagulia mwenyewe itathibiti”.  [Fat-hul Baariy (9/98) na Bidaayatul Mujtahid (2/29)]

 

Jumhuwr ya ‘Ulamaa wametolea dalili Hadiyth ya Abu Hurayrah:  “Kwamba Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:

 

"تُسْتَأْمَرُ الْيَتِيمَةُ فِي نَفْسِهَا، فَإِنْ صَمَتَتْ فَهُوَ إِذْنُهَا، وَإِنْ أَبَتْ فَلَا جَوَازَ عَلَيْهَا"

 

“Yatima ni lazima atakwe ushauri kuhusiana na nafsi yake mwenyewe.  Kama atanyamaza, basi hiyo ndiyo idhini yake, na kama atakataa, basi hakuna ndoa kwake”. [Hadiyth Swahiyh.  Imechakatwa na Abu Daawuwd (2093), At-Tirmidhiy (1190), An-Nasaaiy (3270) na Ahmad (7519)]

 

Yatima anayekusudiwa hapa ni msichana mdogo aliyefiwa na baba yake na ambaye pia bado

hajavunja ungo.  Akivunja, si yatima tena.

 

 

 

 

Share