08-Swahiyh Fiqh As-Sunnah: Kitabu Cha Ndoa: Kufunga Ndoa: Masharti Ya Kuswihi ‘Aqdi Ya Ndoa: Sharti la Kwanza: (e) Walii Kuzuia Ndoa

 

Swahiyh Fiqh As-Sunnah

 

كِتَابُ الزَّوَاجِ

 

Kitabu Cha Ndoa

 

 

عَقْدُ الزَّوَاجِ

 

Kufunga Ndoa

 

 

Alhidaaya.com

 

 

 

08:  Masharti Ya Kuswihi ‘Aqdi Ya Ndoa: Sharti la Kwanza: (e) Walii Kuzuia Ndoa:

 

 

Tumeshasema nyuma kwamba walii haruhusiwi kumlazimisha mwanamke kuolewa na mtu asiyemtaka, kama ambavyo haruhusiwi pia kumzuia kuolewa na mtu aliyemridhia ikiwa mtu huyo ana vigezo vinavyokubalika.

 

Allaah Ta’aalaa Amesema: 

 

"وَإِذَا طَلَّقْتُمُ النِّسَاءَ فَبَلَغْنَ أَجَلَهُنَّ فَلَا تَعْضُلُوهُنَّ أَن يَنكِحْنَ أَزْوَاجَهُنَّ إِذَا تَرَاضَوْا بَيْنَهُم بِالْمَعْرُوفِ"

 

“Na mtakapowataliki wanawake wakafikia muda wa kumaliza eda yao, basi msiwazuie kuolewa na waume zao (wa awali) ikiwa wameridhiana baina yao kwa mujibu wa ada”.  [Al-Baqarah:  (232)]

 

Ikiwa walii atamzuia binti yake, basi uwalii wake utahamishiwa kwa mwengine.  Ash-Shaafi’iy amesema kwamba walii akizuia, basi uwalii wake utahamishiwa kwa kadhi.  Ama Abu Haniyfah, yeye amesema utahamishiwa kwa walii wa ngazi ya mbali zaidi, lakini kwa sharti awe na vigezo vinavyokubalika.  Na ikiwa mawalii wote watakataa kumwozesha na wakamzuia, basi uwalii utahamishiwa kwa kadhi moja kwa moja.  [Majmuw’ul Fataawaa: (32/37)]

 

Ninasema:  “Kauli iliyo karibu zaidi ni ya Abu Haniyfah kutokana na Hadiyth Marfuw’u ya ‘Aaishah:

"فَإِنِ اشْتَجَرُوا فَالسُّلْطَانُ وَلِيُّ من لَا ولي لَهُ "

 

“Na kama watazozana, basi Sultani ndiye walii kwa asiye na walii”.   [Hadiyth Swahiyh.  Imetajwa nyuma]

 

 

Share