054-Maswali 200 Na Majibu Ya ‘Aqiydah: Ni Ipi Mifano Ya Majina Matukufu Katika Sunnah?
200 سُؤالٌ وَ جَوَابٌ فِي الْعَقِيدَة
Maswali 200 Na Majibu Ya ‘Aqiydah
لِلشَّيخ حافِظ بن أحْمَد الحَكمَيّ
Shaykh Haafidhw Bin Ahmad Al-Hakamiyy (رحمه الله)
Imefasiriwa na: Alhidaaya.com
054-Ni Ipi Mifano Ya Majina Matukufu Katika Sunnah?
Swali:
س: ما مثال الأسماء الحسنى من السنة
Ni ipi mifano ya Majina Matukufu katika Sunnah?
Jibu:
ج: مثل قوله صلى الله عليه وسلم( لا إله إلا الله العظيم الحليم لا إله إلا الله رب العرش العظيم, لا إله إلا الله رب السماوات ورب الأرض ورب العرش الكريم )وقوله صلى الله عليه وسلم( يا حي يا قيوم يا ذا الجلال والإكرام يا بديع السماوات والأرض )وقوله صلى الله عليه وسلم( بسم الله الذي لا يضر مع اسمه شيء في الأرض ,ولا في السماء وهو السميع العليم )وقوله صلى الله عليه وسلم( اللهم عالم الغيب والشهادة فاطر السماوات والأرض رب كل شيء ومليكه )الحديث وقوله صلى الله عليه وسلم( اللهم رب السماوات السبع ورب العرش العظيم ربنا ورب كل شيء فالق الحب والنوى منزل التوراة والإنجيل والقرآن أعوذ بك من شر كل ذي شر أنت آخذ بناصيته أنت الأول فليس قبلك شيء وأنت الآخر فليس بعدك شيء, وأنت الظاهر فليس فوقك شيء وأنت الباطن فليس دونك شيء )الحديث.
وقوله صلى الله عليه وسلم( اللهم لك الحمد أنت نور السماوات والأرض ومن فيهن ولك الحمد أنت قيوم السماوات والأرض ومن فيهن )الحديث. وقوله صلى الله عليه وسلم( اللهم إني أسألك بأني أشهد أنك أنت الله لا إله إلا أنت الأحد الصمد الذي لم يلد ولم يولد ولم يكن له كفوا أحد )وقوله صلى الله عليه وسلم( يا مقلب القلوب )الحديث وغير ذلك كثير.
Ni mfano wa kauli yake Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam):
"Hapana mwabudiwa wa haki isipokuwa Allaah Mtukufu, Mpole, Rabb wa 'Arshi Tukufu, Rabb wa mbingu na ardhi na Rabb wa 'Arshi tukufu”. [Al-Bukhaariy (7436), (7431) na Muslim (2730)]
Na kauli yake Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam):
"Ee Ulie Hai, na Msimamizi, Ee Ulie Mtukufu na Ukarimu, Ee Ulie Umba mbingu na ardhi". [Imepokewa na Abdul Ghani Al-Maqdisiy katika At-Targhiyb fiy Ad-Du'aa (57), An-Nasaai (3/52), Abu Daawuud (1495), Al-Bukhaariy katika Al-Adabu Al-Mufrad (705), Ibn Hibaan (893), At-Twahawiy katika Sharh Al-Mushkal (175), At-Twabraniy katika Ad-Du'aa (116), Al-Haakim (1/503), (504)]
Na kauli yake Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam):
"Kwa Jina la Allaah Ambae kwa Jina Lake Hilo Halidhuriwi na kitu chochote mbinguni na ardhini na Yeye Ndie Msikivu na Mjuzi”. [Imepokewa na At-Twayalisiy (79), na katika njia yake Al-Bukhaariy katika Al-Adabu Al-Mufrad (660), At-Tirmidhiy (3388), Ibn Majah (3869), Ahmad ((1/62), (66), At-Twahawiy katika Sharh Al-Mushkal (3076), Al-Haakim (1/54).
Na kauli yake Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam):
“Ee Mola. Mjuzi wa Ghaibu na Dhahiri, Muumba wa mbingu na ardhini na Mola wa kila kitu na Mmiliki Wake” [Ahmad (1/9), Al-Bukhaariy katika Al-Adabu Al-Mufrad (1202), Abu Daawuwd (5067), At-Tirmidhiy (3392), An-Nasaai katika Kitabu Chake, 'Amalul Yawm Wal-Layla' (967), At-Twayalisiy (1/251), Ibn Hibaan (962), Ad-Darimiy (2689), Al-Haakim (1/513), Ibn Sunniy (45), Al-Miziy katika At-Tahdhiyb (22/86)
Na kauli yake Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam):
“Ee Rabb wa mbingu saba, Rabb wa 'Arshi tukufu, Rabb wetu na Rabb wa kila kitu, Muotesha mbegu na punje, Mteremshaji wa Tawrat Injili na Qur-aan, najilinda kwako kwa kila shari ya mwenye shari, na Wewe Ndio Mzuiaji wake, Wewe Ndio wa tangu hakuna kitu kabla Yako, na Wewe Ndio Unaejua undani wa kila kitu, hakuna mwingine zaidi Yako…” (Al-Hadiyth). [Imepokewa na Muslim (2713), Abu Daawuwd (5051), At-Tirmidhiy (3460), Ahmad (2/381, 5537), Al-Haakim (3/157)]
Na kauli yake Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam):
“Ee Mola, Kuhimidiwa Kwako, Wewe ni Nuru ya mbingu na ardhi na vilivyomo ni Vyako pia Sifa njema na Wewe Ndio Msimamizi wa mbingu na ardhi na vilivyomo”. (Al-Hadiyth). [Impokewa na Al-Bukhaariy (1120), Muslim (769), Ahmad (1/298, 308), Malik katika Al-Muwatwa (1/127), An-Nasaai katika kitabu chake, 'Amalul Yawm Wal-Layla' (868), na katika As-Sughara (3/210), At (3418), Ibn Majah (1355) katika Hadiyth ya Ibn 'Abbas]
Na kauli yake Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam):
“Ee Mola, Hakika mimi nakuomba Wewe kwani mimi nashuhudia kwamba Wewe Ndio Allaah. Hakuna mwingine ila Wewe, wa Pekee, Mwenye kukusudiwa kwa kila kitu, Hajazaa wala Hajazaliwa, na wala Hana yoyote wa kufanana Naye” . [Imepokewa na Abu Daawuud (1493), At-Tirmidhiy (3475), Ahmad (5/349, 350, 360), Ibn Abi Shaybah (7/57), Ibn Majah (3857), Ibn Hibaan (891), At-Twabaraniy katika Ad-Du'aa (114), Al-Haakim (1/504)]
Na kauli ya Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam): “Ee Mwenye Kupindua nyoyo…”. (Al-Hadiyth) [Imepokewa na Ahmad (3/112), Ibn Abi Shaybah (7/28), At-Tirmidhi (2140), Ibn Abi 'Aswim (225), Abu Ya'ala (6/359) na Al-Haakim (1/526)].
Na nyinginezo zaidi ya hizo.