055-Maswali 200 Na Majibu Ya ‘Aqiydah: Kuna Aina Ngapi Zinazojulisha Majina Mazuri?
200 سُؤالٌ وَ جَوَابٌ فِي الْعَقِيدَة
Maswali 200 Na Majibu Ya ‘Aqiydah
لِلشَّيخ حافِظ بن أحْمَد الحَكمَيّ
Shaykh Haafidhw Bin Ahmad Al-Hakamiyy (رحمه الله)
Imefasiriwa na: Alhidaaya.com
055-Kuna Aina Ngapi Zinazojulisha Majina Mazuri?
Swali:
س: على كم نوع دلالة الأسماء الحسنى
Kuna aina ngapi zinazojulisha Majina Mazuri?
Jibu:
ج: هي على ثلاثة أنواع دلالتها على الذات مطابقة ودلالتها على الصفات المشتقة منها تضمنا ودلالتها على الصفات التي ما اشتقت منها التزاما.
Kuna aina tatu; ya kwanza ni dalili juu ya dhati yenye kwenda sambamba.
Pili: Ni dalili juu ya sifa zinazotokana na majina yaliotokana nayo.
Tatu: Ni dalili juu ya sifa zisizo gawika kutokana na majina kwa kulazimika.