056-Maswali 200 Na Majibu Ya ‘Aqiydah: Ni Ipi Mifano Yake?

 

 

200 سُؤالٌ وَ جَوَابٌ فِي الْعَقِيدَة

 

Maswali 200 Na Majibu Ya ‘Aqiydah

 

لِلشَّيخ حافِظ بن أحْمَد الحَكمَيّ

Shaykh Haafidhw Bin Ahmad Al-Hakamiyy (رحمه الله)

Imefasiriwa na:  Alhidaaya.com

 

 

056-Ni Ipi Mifano Yake?

 

 

 

Swali:

س: ما مثال ذلك

 

Ni ipi mifano yake?

 

Jibu:

ج: مثال ذلك: اسمه تعالى الرحمن الرحيم يدل على ذات المسمى وهو الله عز وجل مطابقة وعلى الصفة المشتق منها وهي الرحمة تضمنا وعلى غيرها من الصفات التي لم تشتق منها كالحياة والقدرة التزاما ,وهكذا سائر أسمائه وذلك بخلاف المخلوق فقد يسمى حكيما وهو جاهل وحكما وهو ظالم وعزيزا وهو ذليل وشريفا وهو وضيع وكريما وهو لئيم وصالحا وهو طالح وسعيدا وهو شقي وأسدا وحنظلة وعلقمة وليس كذلك, فسبحان الله وبحمده هو كما وصف نفسه وفوق ما يصفه به خلقه.

 

Mifano hiyo ni Jina Lake Allaah kama vile: Ar-Rahmaan na Ar-Rahiym, yanajulisha dhati iliyotokana na Allaah kwa usambamba na Jina Hilo. Na juu ya Sifa iliyotokana na Jina Hilo Ambalo ni (Rehmah) lililoambatana Nalo. Na Sifa zingine ambazo hazijatokana na jina hilo kama vile: Uhai na uwezo, kwa kulazimika. Na hivi ndivyo majina mengine yaliyosalia, kinyume na viumbe vilivyo umbwa, vinaweza kuitwa (Hakiim) lakini kikawa (Jahili) kisichojua kitu. Au (Hakiim) kumbe ni dhalimu, au ‘Aziiz kumbe ni dhalili au Sharifu kumbe ni Mtumwa, au mwenye kuheshimika kumbe ni mwenye kulaumiwa au mwema kumbe muovu, au mwenye kufaulu kumbe ni mwenye hasara, au Asad na Handhala na Al-Qamah kumbe sivyo. Ametakasika Allaah kwa Sifa Zake, kama Alivyojisifu Yeye Mwenyewe na zaidi ya Anavyosifiwa na waja Wake.

 

 

Share