057-Maswali 200 Na Majibu Ya ‘Aqiydah: Kuna Vigawanyo Vingapi Vya Dalili Ya Majina Matukufu Yaliyoambatana Na Jina Lake?
200 سُؤالٌ وَ جَوَابٌ فِي الْعَقِيدَة
Maswali 200 Na Majibu Ya ‘Aqiydah
لِلشَّيخ حافِظ بن أحْمَد الحَكمَيّ
Shaykh Haafidhw Bin Ahmad Al-Hakamiyy (رحمه الله)
Imefasiriwa na: Alhidaaya.com
057-Kuna Vigawanyo Vingapi Vya Dalili Ya Majina Matukufu Yaliyoambatana Na Jina Lake?
Swali:
س: على كم قسم دلالة الأسماء الحسنى من جهة التضمن
Kuna vigawanyo vingapi vya dalili ya Majina matukufu yalioambatana na jina lake?
Jibu:
ج: هي على أربعة أقسام:
الأول: الاسم العلم المتضمن لجميع معاني الأسماء الحسنى وهو الله ;ولهذا تأتي الأسماء جميعها صفات له كقوله تعالى
( هو الله الخالق البارئ المصور )ونحو ذلك, ولم يأت هو قط تابعا لغيره من الأسماء.
الثاني: الثاني ما يتضمن صفة ذات الله عز وجل كاسمه تعالى السميع المتضمن سمعه الواسع جميع الأصوات, سواء عنده سرها وعلانيتها واسمه البصير المتضمن بصره النافذ في جميع المبصرات سواء دقيقها وجليلها ,واسمه العليم المتضمن علمه المحيط الذي( لا يعزب عنه مثقال ذرة في السماوات ولا في الأرض ولا أصغر من ذلك ولا أكبر )واسمه القدير المتضمن قدرته على كل شيء إيجادا وإعداما وغير ذلك.
الثالث: ما يتضمن صفة فعل الله كالخالق الرازق البارئ المصور وغير ذلك.
الرابع: ما يتضمن تنزهه تعالى وتقدسه عن جميع النقائص كالقدوس السلام.
Kuna vigawanyo vinne. Navyo ni:
Kwanza: Ni jina Maalumu lenye kukusanya maana ya Majina Matukufu, Nalo Ni Allaah, Jina Hilo Linakusanya Majina Yote kuwa Sifa Zake Allaah. Kama Anavyosema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):
هُوَ اللَّـهُ الْخَالِقُ الْبَارِئُ الْمُصَوِّرُ ۖ لَهُ الْأَسْمَاءُ الْحُسْنَىٰ ۚ ﴿٢٤﴾
Yeye Ndiye Allaah, Muumbaji, Mwanzishi wa viumbe bila kasoro, Muundaji sura na umbile, Ana Majina Mazuri kabisa. [Al-Hashr: (59:24)]
Na Jina Hili Halijawahi kufuata Majina Mengine, ila Lenyewe Ndio kufuatwa na Majina Mengine Ambayo ni Sifa Zake Allaah.
Pili: Ni Majina Yanayokusanya Sifa ya Dhati Yake Allaah. Kwa mfano “As-Samiy’u: Mwenye Kusikia Yote Daima”, ni Jina Linahusiana na Usikivu Wake upana wa sauti zote ni sawa sawa iwe ya dhahiri au ya siri. Na “Al-Baswiyr: Mwenye kuona yote daima” Ni Jina Linalohusiana na Kuona Kwake Kukali juu ya vyote vyenye kuonwa, Sawa kwa vidogo mno au vya dhahiri. Na Jina La Al-‘Aliym: Mjuzi wa yote daima Linahusiana na Ufahamu Wake Ulioenea kila kitu.
Allaah Amesema katika Qur-aan.
لَا يَعْزُبُ عَنْهُ مِثْقَالُ ذَرَّةٍ فِي السَّمَاوَاتِ وَلَا فِي الْأَرْضِ وَلَا أَصْغَرُ مِن ذَٰلِكَ وَلَا أَكْبَرُ إِلَّا فِي كِتَابٍ مُّبِينٍ ﴿٣﴾
Hakuna kinachofichika Kwake hata chenye uzito wa chembe (kama atomu) mbinguni wala ardhini, wala kidogo zaidi kuliko hicho, wala kikubwa zaidi . [Saba-a: (34:3)]
Na Jina Lake Al-Qadiyr: Muweza Wa Yote Daima: Linabeba Uwezo Wake wa kila kitu wa Kuumba na Kufisha.
Tatu: Ni Majina Yanayobeba Sifa Ya Allaah Ya Kufanya. Kama vile Kuumba, Kuruzuku, Kuanzisha, Kusawirishwa na Mengineyo.
Nne: Kigawanyo cha nne ni Majina Yanayohusiana na Utakasifu Wake na Kutokuwa na Mapungufu kama Sifa ya Al-Qudduws: Mtakatifu Ametakasika Na Sifa Zote Hasi (Pungufu) na As-Salaam: Mwenye Amani, Mwenye kusalimika na kasoro zote.