058-Maswali 200 Na Majibu Ya ‘Aqiydah: Kuna Migawanyiko Mingapi Ya Majina Ya Allaah Kwa Upande Wa Dhati Yake Allaah?
200 سُؤالٌ وَ جَوَابٌ فِي الْعَقِيدَة
Maswali 200 Na Majibu Ya ‘Aqiydah
لِلشَّيخ حافِظ بن أحْمَد الحَكمَيّ
Shaykh Haafidhw Bin Ahmad Al-Hakamiyy (رحمه الله)
Imefasiriwa na: Alhidaaya.com
058-Kuna Migawanyiko Mingapi Ya Majina Ya Allaah Kwa Upande Wa Dhati Yake Allaah?
Swali:
كم أقسام الأسماء الحسنى من جهة إطلاقها على الله عز وجل
Kuna migawanyiko mingapi ya Majina ya Allaah kwa upande wa Dhati Yake Allaah?
Jibu:
ج: منها ما يطلق على الله مفردا أو مع غيره وهو ما تضمن صفة الكمال بأي إطلاق كالحي القيوم الأحد الصمد ونحو ذلك, ومنها ما لا يطلق على الله إلا مع مقابله وهو ما إذا أفرد أوهم نقصا كالضار النافع, والخافض الرافع والمعطي المانع والمعز المذل ونحو ذلك فلا يجوز إطلاق الضار ولا الخافض ولا المانع ولا المذل كل على انفراده, ولم يطلق قط شيء منها في الوحي كذلك لا في الكتاب ولا في السنة, ومن ذلك اسمه تعالى المنتقم لم يطلق في القرآن إلا مع متعلقه كقوله تعالى( إنا من المجرمين منتقمون )أو بإضافة ذو إلى الصفة المشتق منها كقوله تعالى( والله عزيز ذو انتقام ).
Yapo yanayohusiana na Jina Lake Allaah au pamoja na Majina Yake Mengine. Nayo ni Yale Yanayo husiana na Sifa ya Ukamilifu. Kwa Aina Yake, kama Sifa ya Uhai, Msimamizi, Mmoja wa Pekee na Mwenye Kukusudiwa na mengineyo mfano wa hayo. Na yapo ambayo hayahusishwi na Allaah isipokuwa lina husishwa na jingine, ni kwamba likiwa moja, litaleta upungufu. Kama mwenye kudhuru mwenye kunufaisha; au mshushaji mnyanyuaji, Mtoaji Mzuiaji, Mshindishaji na Mdhalilishaji, na mengineyo. Kwa hivyo haifai kuleta Sifa ya Allaah: “Mwenye kudhuru”, au “Mshushaji”, au “Mzuiaji” wala Mwenye kudhalilisha bila kuleta kinyume chake, wala haijawahi kutokea katika/wahyi, na sio katika Qur-aan au Sunnah.
Mfano mwingine ni Jina Lake Allaah la Mwenye kuangamiza (Al-Muntaqim) halijapata kuwepo katika Qur-aan ila kwa kuambatana kama Kauli ya Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):
إِنَّا مِنَ الْمُجْرِمِينَ مُنتَقِمُونَ ﴿٢٢﴾
Hakika Sisi Tutawalipiza wahalifu. [As-Sajdah: (32:22)]
Au kuambatanisha na neno (ذو) dhuu (mwenye), kwa Sifa ya Allaah itokanayo na Jina Lake Al-Muntaqim. Kama Kauli Ya Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):
وَاللَّـهُ عَزِيزٌ ذُو انتِقَامٍ ﴿٩٥﴾
Na Allaah Ni Mwenye Enzi ya Nguvu Asiyeshindika, Mwenye Kulipiza. [Al-Maaidah: (5:95)]