059-Maswali 200 Na Majibu Ya ‘Aqiydah: Ni Zipi Dalili Sifa Ya Dhati Kutoka Katika Qur-aan?
200 سُؤالٌ وَ جَوَابٌ فِي الْعَقِيدَة
Maswali 200 Na Majibu Ya ‘Aqiydah
لِلشَّيخ حافِظ بن أحْمَد الحَكمَيّ
Shaykh Haafidhw Bin Ahmad Al-Hakamiyy (رحمه الله)
Imefasiriwa na: Alhidaaya.com
059-Ni Zipi Dalili Sifa Ya Dhati Kutoka Katika Qur-aan?
Swali:
س: فما مثال صفات الذات من الكتاب
Ni zipi dalili Sifa ya Dhati kutoka katika Qur-aan?
Jibu:
ج: مثل قوله تعالى( بل يداه مبسوطتان )(كل شيء هالك إلا وجهه )( ويبقى وجه ربك ذو الجلال والإكرام )( ولتصنع على عيني )( أبصر به وأسمع )( إنني معكما أسمع وأرى )( يعلم ما بين أيديهم وما خلفهم ولا يحيطون به علما )( وكلم الله موسى تكليما )( وإذ نادى ربك موسى أن ائت القوم الظالمين )( وناداهما ربهما ألم أنهكما عن تلكما الشجرة )( ويوم يناديهم فيقول ماذا أجبتم المرسلين )وغير ذلك.
Ni kauli ya Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):
بَلْ يَدَاهُ مَبْسُوطَتَانِ
Bali Mikono Yake (Allaah) imefumbuliwa Hutoa Atakavyo. [Al-Maaidah: (5:64)]
Na kauli ya Allaah (عزَّ وجلَّ):
كُلُّ شَيْءٍ هَالِكٌ إِلَّا وَجْهَهُ ۚ
Kila kitu ni chenye kuhiliki isipokuwa Wajihi Wake. [Al-Qaswasw: (28:88)]
Na kauli ya Allaah (عزَّ وجلَّ):
وَيَبْقَىٰ وَجْهُ رَبِّكَ ذُو الْجَلَالِ وَالْإِكْرَامِ ﴿٢٧﴾
Na utabakia Wajihi wa Rabb wako Mwenye Ujalali na Ukarimu. [Ar-Rahmaan: (55:27)]
Na kauli ya Allaah (عزَّ وجلَّ):
وَلِتُصْنَعَ عَلَىٰ عَيْنِي ﴿٣٩﴾
Na ili ulelewe vyema Machoni Mwangu. [Twaahaa: (20:39)
Na kauli ya Allaah (عزَّ وجلَّ):
أَبْصِرْ بِهِ وَأَسْمِعْ ۚ
Kuona kulioje Kwake na Kusikia! [Al-Kahf: (18:26)]
Na kauli ya Allaah (عزَّ وجلَّ):
إِنَّنِي مَعَكُمَا أَسْمَعُ وَأَرَىٰ ﴿٤٦﴾
Hakika Mimi Niko pamoja nanyi, Nasikia na Naona. [Twaahaa: (20:46)]
Na kauli ya Allaah (عزَّ وجلَّ):
يَعْلَمُ مَا بَيْنَ أَيْدِيهِمْ وَمَا خَلْفَهُمْ وَلَا يُحِيطُونَ بِهِ عِلْمًا ﴿١١٠﴾
Anajua yale yaliyoko mbele yao, na yale yaliyoko nyuma yao, na wala hawawezi kufikia kuelewa chochote cha Ujuzi Wake. [Twaahaa: (20:110)]
Na kauli ya Allaah (عزَّ وجلَّ):
وَكَلَّمَ اللَّـهُ مُوسَىٰ تَكْلِيمًا ﴿١٦٤﴾
Na bila shaka Allaah Alimsemesha Muwsaa maneno moja kwa moja. [An-Nisaa: (4:164)]
Na kauli ya Allaah (عزَّ وجلَّ):
وَإِذْ نَادَىٰ رَبُّكَ مُوسَىٰ أَنِ ائْتِ الْقَوْمَ الظَّالِمِينَ ﴿١٠﴾
Na Rabb wako Alipomwita Muwsaa kwamba: Nenda kwa watu madhalimu. [Ash-Shu'araa: (26:10)]
Na kauli ya Allaah (عزَّ وجلَّ):
وَنَادَاهُمَا رَبُّهُمَا أَلَمْ أَنْهَكُمَا عَن تِلْكُمَا الشَّجَرَةِ
Na Rabb wao Akawaita: Je, kwani Mimi Sikukukatazeni mti huo [Al-A'raaf: (7:22)
Na kauli ya Allaah (عزَّ وجلَّ):
وَيَوْمَ يُنَادِيهِمْ فَيَقُولُ مَاذَا أَجَبْتُمُ الْمُرْسَلِينَ ﴿٦٥﴾
Na Siku (Allaah) Atakapowaita, Atasema: Mliwajibu nini Rusuli? [Al-Qaswasw: (28:65)]