060-Maswali 200 Na Majibu Ya ‘Aqiydah: Ni Zipi Sifa Za Dhati Kupitia Sunnah?

 

 

200 سُؤالٌ وَ جَوَابٌ فِي الْعَقِيدَة

 

Maswali 200 Na Majibu Ya ‘Aqiydah

 

لِلشَّيخ حافِظ بن أحْمَد الحَكمَيّ

Shaykh Haafidhw Bin Ahmad Al-Hakamiyy (رحمه الله)

Imefasiriwa na:  Alhidaaya.com

 

 

060-Ni Zipi Sifa Za Dhati Kupitia Sunnah?

 

 

 

 

 

 

Swali:

س: ما مثال صفات الذات من السنة 

 

Ni zipi Sifa za Dhati kupitia Sunnah?

 

Jibu:

 

ج: كقوله صلى الله عليه وسلم( حجابه النور لو كشفه لأحرقت سبحات وجهه ما انتهى إليه بصره من خلقه )وقوله صلى الله عليه وسلم( يمين الله ملأى لا تغيضها نفقة سحاء الليل والنهار أرأيتم ما أنفق منذ خلق السماوات والأرض ,فإنه لم يغض ما في يمينه وعرشه على الماء وبيده الأخرى الفيض أو القبض يرفع ويخفض )وقوله صلى الله عليه وسلم في حديث الدجال( إن الله لا يخفي عليكم أن الله ليس بأعور )وأشار بيده إلى عينه الحديث, وفي حديث الاستخارة( اللهم إني أستخيرك بعلمك وأستقدرك بقدرتك وأسألك من فضلك العظيم فإنك تقدر ولا أقدر وتعلم ولا أعلم وأنت علام الغيوب )الحديث, وقوله صلى الله عليه وسلم( إنكم لا تدعون أصم لا غايبا تدعون سميعا بصيرا قرييا )وقوله صلى الله عليه وسلم( إذا أراد الله أن يوحي بالأمر تكلم بالوحي )الحديث, وفي حديث البعث( يقول الله تعالى: يا آدم فيقول لبيك )الحديث, وأحاديث كلام الله لعباده في الموقف ,وكلامه لأهل الجنة وغير ذلك ما لا يحصى.

 

Ni kauli ya Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) aliposema:

 

“Pazia Lake ni Nuru laiti Lingefunguliwa zingeunguza nuru ya Uso Wake, zisingemaliza Uoni Wake kwa viumbe Vyake”. [Imepokewa na Muslim (179), Ibn Majah (196, 196) na Twayalisi (491)]

 

Na kauli yake Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam):

 

“Mkono Wake Wa Kulia Umejaa, na Haupungui kwa Kutoa Kwake Usiku na Mchana, Mnaonaje Tangu Ameanza kutoa tangu Alipoumba  Mbingu na Ardhi, hakika hapaja pungua kitu katika Mkono Wake Wa Kulia, na 'Arshi Yake Ipo juu ya maji na Mkono Wake Mwingine Umejaa kwa Kutoa na Kuzuia Ana Nyanyua na Kushusha”. [Imepokewa na Al-Bukhaariy (7419) na Muslim( 992)]

 

Katika Hadiyth ya Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) kuhusiana na Dajjaal:

 

"Hakika Allaah Hajifichi kwenu, na hakika Yeye Sio Chongo.”[Imepokewa na Al-Bukhaariy (3057) na Muslim (169)]

 

Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akaashiria kwa mkono wake katika jicho.

 

Hadiyth ya Istikhaarah Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) anasema:

“Ee Allaah hakika mimi na kuomba ushauri kwa elimu Yako, na niwezeshe kwa uwezo Wako, na nakuomba fadhila Zako bora, Wewe  Unaweza  mimi siwezi, na Wewe Ndio Mjuzi wa Siri”. [Imepokewa na Al-Bukhaariy (6382)]

 

Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) anasema:

“Nyinyi hamumuombi kiziwi wala asiyekuwepo, bali mnamuuomba Allaah Msikivu, Muoni wa Karibu Mno”. [Imepokewa na Al-Bukhaariy (2992) na Muslim (2074) katika Hadiyth ya Abu Muwsaa]

 

Na kauli yake Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam):

 

“Allaah Akitaka kutoa Amri ya jambo Hushusha Wahyi (Ufunuo)”. [Imepokewa na Al-Bukhaariy (4701, 4800, 7481), At-Tirmidhiy (3223), Abu Dawuwd (3989, 4738), Ibn Majah (194) katika Hadiyth ya Abu Hurayrah]

 

Na katika Hadiyth ya wahyi ufufuo Allaah Anasema:

 

“Ee Adam, Akaitika Naam.…” (Hadiyth) [Imepokewa na Al-Bukhaariy (3348, 4741, 6530, 7483), Muslim (222) katika Hadiyth ya Abu Sa'id], na Hadiyth za maneno ya Allaah kuhusiana na waja Wake Siku ya Kisimamo, na maneno Yake kwa watu wa peponi na zinginezo nyingi tu.

 

 

Share