061-Maswali 200 Na Majibu Ya ‘Aqiydah: Ni Ipi Mifano Kuhusiana Na Sifa Za Vitendo Ndani Ya Qur-aan?
200 سُؤالٌ وَ جَوَابٌ فِي الْعَقِيدَة
Maswali 200 Na Majibu Ya ‘Aqiydah
لِلشَّيخ حافِظ بن أحْمَد الحَكمَيّ
Shaykh Haafidhw Bin Ahmad Al-Hakamiyy (رحمه الله)
Imefasiriwa na: Alhidaaya.com
061-Ni Ipi Mifano Kuhhusiana Na Sifa Za Vitendo Ndani Ya Qur-aan?
Swali:
س: ما مثال صفات الأفعال من الكتاب
Ni ipi mifano Kuhusiana na sifa za vitendo ndani ya Qur-aan?
Jibu:
ج: مثل قوله تعالى( ثم استوى إلى السماء )وقوله( هل ينظرون إلا أن يأتيهم الله )الآية, وقوله تعالى( وما قدروا الله حق قدره والأرض جميعا قبضته يوم القيامة والسماوات مطويات بيمينه )وقوله تعالى( ما منعك أن تسجد لما خلقت بيدي )وقوله تعالى( وكتبنا له في الألواح من كل شيء )وقوله تعالى( فلما تجلى ربه للجبل جعله دكا )وقوله تعالى( إن الله يفعل ما يشاء )وغيرها من الآيات.
Mfano ni kauli ya Allaah (عزَّ وجلَّ):
ثُمَّ اسْتَوَىٰ إِلَى السَّمَاءِ ﴿٢٩﴾
Kisha Akazikusudia mbingu (Kuziumba) [Al-Baqarah: (2:29)]
Na kauli ya Allaah (عزَّ وجلَّ):
هَلْ يَنظُرُونَ إِلَّا أَن يَأْتِيَهُمُ اللَّـهُ ﴿٢١٠﴾
Je, wanangojea nini isipokuwa Allaah Awajie [Al-Baqarah: (2:210)]
Na kauli ya Allaah (عزَّ وجلَّ):
وَمَا قَدَرُوا اللَّـهَ حَقَّ قَدْرِهِ وَالْأَرْضُ جَمِيعًا قَبْضَتُهُ يَوْمَ الْقِيَامَةِ وَالسَّمَاوَاتُ مَطْوِيَّاتٌ بِيَمِينِهِ ۚ ﴿٦٧﴾
Na hawakumkadiria Allaah kama inavyostahiki kumkadiria. Na hali ardhi yote Ataikamata Mkononi Mwake Siku ya Qiyaamah, na mbingu zitakunjwa kwa Mkono Wake wa kulia. [Az-Zumar: (39:67)]
Na kauli ya Allaah (عزَّ وجلَّ):
قَالَ يَا إِبْلِيسُ مَا مَنَعَكَ أَن تَسْجُدَ لِمَا خَلَقْتُ بِيَدَيَّ ۖ ﴿٧٥﴾
(Allaah) Akasema: Ee Ibliys! Nini kilichokuzuia usimsujudie Niliyemuumba kwa Mikono Yangu? [Swaad: (38:75)
Na kauli ya Allaah (عزَّ وجلَّ):
وَكَتَبْنَا لَهُ فِي الْأَلْوَاحِ مِن كُلِّ شَيْءٍ ﴿١٤٥﴾
Na Tukamwandikia kwenye vibao kila kitu; [Al-A'raaf: (7:145)]
Na kauli ya Allaah (عزَّ وجلَّ):
فَلَمَّا تَجَلَّىٰ رَبُّهُ لِلْجَبَلِ جَعَلَهُ دَكًّا ﴿١٤٣﴾
Basi Rabb wake Alipojidhihirisha katika mlima, Aliufanya uvurugike kuwa vumbi [Al-A'raaf: (7:143)]
Na kauli ya Allaah (عزَّ وجلَّ):
إِنَّ اللَّـهَ يَفْعَلُ مَا يَشَاءُ ۩﴿١٨﴾
Hakika Allaah Anafanya Atakavyo. [Al-Hajj: (22:18)]
Na Aayah zingine zaidi.