062-Maswali 200 Na Majibu Ya ‘Aqiydah: Ni Ipi Mifano Ya Sifa Ya Vitendo Kwa Dalili Ya Sunnah?
200 سُؤالٌ وَ جَوَابٌ فِي الْعَقِيدَة
Maswali 200 Na Majibu Ya ‘Aqiydah
لِلشَّيخ حافِظ بن أحْمَد الحَكمَيّ
Shaykh Haafidhw Bin Ahmad Al-Hakamiyy (رحمه الله)
Imefasiriwa na: Alhidaaya.com
062-Ni Ipi Mifano Ya Sifa Ya Vitendo Kwa Dalili Ya Sunnah?
Swali:
س: ما مثال صفات الأفعال من السنة
Ni ipi mifano ya sifa ya vitendo kwa dalili ya Sunnah?
Jibu:
ج: مثل قوله صلى الله عليه وسلم( ينزل ربنا كل ليلة إلى السماء الدنيا حين يبقى ثلث الليل الآخر )الحديث, وقوله صلى الله عليه وسلم في حديث الشفاعة( فيأتيهم الله في صورته التي يعرفون فيقول أنا ربكم فيقولون أنت ربنا ) الحديث, ونعني بصفة الفعل هنا الإتيان لا الصورة فافهم, وقوله صلى الله عليه وسلم( إن الله يقبض يوم القيامة الأرض وتكون السماوات بيمينه ثم يقول أنا الملك )الحديث, وقوله صلى الله عليه وسلم( لما خلق الله الخلق كتب بيده على نفسه أن رحمتي تغلب غضبي )وفي حديث احتجاج آدم وموسى: "فقال آدم يا موسى اصطفاك الله بكلامه وخط لك التوراة بيده" فكلامه تعالى ويده صفتا ذات وتكلمه صفة ذات وفعل معا وخطه التوراة صفة فعل, وقوله صلى الله عليه وسلم( إن الله تعالى يبسط يده بالليل ليتوب مسيء النهار ويبسط يده بالنهار ليتوب مسيء الليل ) الحديث, وغيرها كثير.
Ni kauli ya Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) inayosema:
“Rabb wetu Hushuka katika mbingu ya kwanza kila unapoingia usiku katika theluthi ya mwisho ya usiku”. [Imepokewa na Al-Bukhaariy (1145) na Muslim (758) kutoka katika Hadiyth ya Abu Hurayrah]
Hadiyth ya Shifaa Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) anasema:
"Allaah Atawaijia kwa Sura Yake wanayoijua Atawaambia: Mimi Ndio Rabb wenu, watasema Wewe ni Rabb wetu " [Imepokewa na Al-Bukhaariy (7437) na Muslim (194) kutoka katika Hadiyth ya Abuu Sa'id]
Tunakusudia kwa: Sifa ya kitendo hapa: Kuja, na sio sura tupu, na kauli nyingine ya Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam):
“Hakika ya Allaah Ataishika ardhi Siku ya Qiyaamah na mbingu zitakuwa kuliani Mwake kisha Atasema, Mimi Ndio Mfalme.“ [Imepokewa na Al-Bukhaariy (7412) na Muslim (2787) kutoka katika Hadiyth ya Ibnu ‘Umar]
Na kauli ya Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam):
“Allaah Alipoumba viumbe, Aliandika kwa Mkono Ndani ya Nafsi Yake kwamba, Rehema Yangu inashinda hasira Zangu.” [Imepokewa na Al-Bukhaariy (7404) na Muslim (2751) kutoka katika Hadiyth ya Abu Hurayrah]
Katika majadiliano ya Nabiy Aadam na Muwsaa (‘Alayhimu sallam) Hadiyth inasema:
“Aadam alimwambia Nabiy Muwsaa, Ee Muwsaa! Allaah amekuchagua wewe kwa maneno Yake, na Akakuandikia wewe Tawraat kwa Mkono Wake.”[Imepokewa na Al-Bukhaariy (3409) na Muslim (2652)]
Maneno Yake Allaah pamoja na Mkono Wake ni sifa za dhati Yake, na Kuongea Kwake ni sifa ya dhati na ni sifa ya kitendo pamoja, na kuandika Tawraat ni sifa Yake ya kitendo.
Na kauli ya Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam):
“Hakika Allaah Anakunjua Mkono Wake usiku ili atubie mkosaji wa usiku". [Imepokewa na Muslim (2759)]