063-Maswali 200 Na Majibu Ya ‘Aqiydah: Je Sifa Zote Za Vitendo Zinazotokana Na Majina Yake? Au Majina Yote Ya Allaah Yana Kikomo (Tawqiyfiyah)?
200 سُؤالٌ وَ جَوَابٌ فِي الْعَقِيدَة
Maswali 200 Na Majibu Ya ‘Aqiydah
لِلشَّيخ حافِظ بن أحْمَد الحَكمَيّ
Shaykh Haafidhw Bin Ahmad Al-Hakamiyy (رحمه الله)
Imefasiriwa na: Alhidaaya.com
063-Je Sifa Zote Za Vitendo Zinazotokana Na Majina Yake? Au Majina Yote Ya Allaah Yana Kikomo (Tawqiyfiyah)?
Swali:
س: هل يشتق من كل صفات الأفعال أسماء أم أسماء الله كلها توقيفية
Je Sifa Zote Za Vitendo Zinazotokana Na Majina Yake? Au Majina Yote Ya Allaah Yana Kikomo (Tawqiyfiyah)?
Jibu:
ج: لا بل أسماء الله تعالى كلها توقيفية لا يسمى إلا بما سمى به نفسه في كتابه أو أطلقه عليه رسوله صلى الله عليه وسلم وكل فعل أطلقه الله تعالى على نفسه فهو فيما أطلق فيه مدح وكمال ولكن ليس كلها وصف الله به نفسه مطلقا ولا كلها يشتق منها أسماء بل منها ما وصف به نفسه مطلقا كقوله تعالى( الله الذي خلقكم ثم رزقكم ثم يميتكم ثم يحييكم )وسمى نفسه الخالق الرازق المحي المميت المدبر, ومنها أفعال أطلقها الله تعالى على نفسه على سبيل الجزاء ,والمقابلة وهي فيما سيقت له مدح وكمال كقوله تعالى( يخادعون الله وهو خادعهم )( ومكروا ومكر الله والله خير الماكرين )( نسوا الله فنسيهم )ولكن لا يجوز إطلاقها على الله في غير ما سيقت فيه من الآيات, فلا يقال أنه تعالى يمكر ويخادع ويستهزئ ونحو ذلك, وكذلك لا يقال ماكر مخادع مستهزئ ولا يقوله مسلم ولا عاقل ,فإن الله عز وجل لم يصف نفسه بالمكر والخداع إلا على وجه الجزاء لمن فعل ذلك بغير حق ,وقد علم أن المجازاة على ذلك بالعدل حسنة من المخلوق فكيف من الخلاق العليم العدل الحكيم.
Hapana, sio kila sifa inatokana na Majina Yake, bali Majina Yake Yote ni Tawqiyf haitwi isipokuwa Anaitwa kama Alivyojiita Mwenyewe ndani ya Qur-aan au Sunnah za Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam).
Kila sifa ya kitendo Aliyojiita Mwenyewe, na sio kila sifa inatokana na majina Yake, bali kuna sifa Amejisifia Mwenyewe. Kwa mfano Mfano ni kauli ya Allaah (عزَّ وجلَّ):
اللَّـهُ الَّذِي خَلَقَكُمْ ثُمَّ رَزَقَكُمْ ثُمَّ يُمِيتُكُمْ ثُمَّ يُحْيِيكُمْ ۖ ﴿٤٠﴾
Allaah, Ndiye Amekuumbeni, kisha Akakuruzukuni, kisha Anakufisheni, kisha Atakuhuisheni. [Ar-Ruwm: (30:40)]
Allaah Amejiita Mwenyewe kuwa Ndio; Muumba, Mruzuku, Muhuyishaji, Mfishaji na Mpangiaji. Na zipo sifa za Allaah za vitendo Amejiita Mwenyewe kwa mfano: Sifa ya Ulipaji ni sifa Yake ya Ukamilifu.
Na kauli ya Allaah (عزَّ وجلَّ):
إِنَّ الْمُنَافِقِينَ يُخَادِعُونَ اللَّـهَ وَهُوَ خَادِعُهُمْ ﴿١٤٢﴾
Hakika wanafiki (wanadhani) wanamhadaa Allaah, na hali Yeye (Allaah) Ndiye Mwenye kuwahadaa. [An-Nisaa: (4:142)]
Na kauli ya Allaah (عزَّ وجلَّ):
وَمَكَرُوا وَمَكَرَ اللَّـهُ ۖ وَاللَّـهُ خَيْرُ الْمَاكِرِينَ ﴿٥٤﴾
Wakapanga makri (njama) na Allaah Akapanga makri. Na Allaah Ni Mbora wa wenye kupanga makri. [Aal-'Imraan: (3:54)]
Na kauli ya Allaah (عزَّ وجلَّ):
نَسُوا اللَّـهَ فَنَسِيَهُمْ ۗ ﴿٦٧﴾
Wamemsahau Allaah, basi Naye Amewasahau. [At-Tawbah: (9:67)]
Sifa hii ya kuwasahau haifai kabisa kuegemezwa kwa Allaah bila mtiririko ule wa muktadha wa aya kwa hiyo haisemwi: Allaah ana vitimbi, au ana hadaa, au kufanya shere, na mifano mingine. Kwa kinyume chake, na zimetumika sifa hizi kwa Allaah kwa njia ya Malipo ya wale wanaofanya shere au hadaa au vitimbi bila haki. Na ifahamike kwa kulipiana huko ni kama mfano viumbe kufanyiana hisani vipi kwa mtukuka, Muumba mjuzi, muadilifu, mwingi wa hekima.