Tahadhari Na Misemo Ya Kimakosa Makubwa! Kusema: لا حول الله (Laa Hawli-LLaah)
Tahadhari Na Misemo Ya Kimakosa Makubwa!
Kusema: لا حول الله (Laa Hawli-LLaah)
Kwa sababu inamaanisha: "Hapana uwezo wa Allaah!"
Ni kosa kubwa kusema Allaah Hana nguvu! Ilhali Allaah ni Mweza wa kila kitu na ni Mwenye Nguvu wala hakuna linalomshinda!
La sahihi kusema ni kama ilivyothibiti katika Sunnah:
لا حَوْلَ وَلا قُوَّةَ إِلا باللَّهِ
"Hapana uwezo wala nguvu isipokuwa (unatoka) kwa Allaah."