033-Majina Ya Allaah Mazuri Na Sifa Zake أسماء الله الحسنى وصفاته: AL-GHAFUWR, AL-GHAFFAAR

 

 

أسماء الله الحسنى وصفاته

Majina Ya Allaah Mazuri Na Sifa Zake

 

 

Alhidaaya.com

 

 

الْغَفُور - الْغَفَّار

033-Al-Ghafuwr, Al-Ghaffaar

 

 

 

Al-Ghafuwr: Mwingi Wa Kughufuria 

 

Al-Ghaffaar: Mwingi Mno Wa Kughufria

 

 

Ni Anayemsitiri mwenye kutenda dhambi; Hamfedheheshi na kumuadhibu kwa dhambi hiyo.

 

Asili ya ghafara katika lugha ni kusitiri na kufunika na mighfaar ni kile kinachowekwa katika kichwa cha mpiganaji wakati wa vita ili kujikinga na mishale, nayo ina maana mbili: Kusitiri na kuzuia.

 

Ni Jina linaloelezea maghfirah mengi ya Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) kwa mja Wake mwenye kufanya dhambi na kuomba maghfirah, kama Anavyosema:

 

وَإِنِّي لَغَفَّارٌ لِّمَن تَابَ وَآمَنَ وَعَمِلَ صَالِحًا ثُمَّ اهْتَدَىٰ ﴿٨٢﴾

Na hakika Mimi bila shaka Ni Mwingi mno wa Kughufuria kwa anayetubia na akaamini na akatenda mema, tena akathibiti katika njia ya sawa.  [Twaahaa (20:82)]

 

 

Jina hili la Al-Ghafuwr na Al-Ghaffaar limekariri katika Qur-aan mara nyingi, miongoni mwa Aayah ni zifuatazo:

 

لَقَدْ كَانَ لِسَبَإٍ فِي مَسْكَنِهِمْ آيَةٌ ۖ جَنَّتَانِ عَن يَمِينٍ وَشِمَالٍ ۖ كُلُوا مِن رِّزْقِ رَبِّكُمْ وَاشْكُرُوا لَهُ ۚ بَلْدَةٌ طَيِّبَةٌ وَرَبٌّ غَفُورٌ ﴿١٥﴾

Kwa yakini ilikuwa ni Aayah (Ishara) kwa (watu wa) Saba-a katika masikani zao. Bustani mbili; kulia na kushoto. (Wakaambiwa): Kuleni katika riziki ya Rabb wenu na mshukuruni. Mji mzuri na Rabb Ambaye Ni Mwingi wa Kughufuria. [Sabaa (34:15)]

 

فَقُلْتُ اسْتَغْفِرُوا رَبَّكُمْ إِنَّهُ كَانَ غَفَّارًا﴿١٠﴾

Nikasema: Ombeni maghfirah kwa Rabb wenu, hakika Yeye Ni Mwingi mno wa Kughufuria. [Nuwh (71:10)]

 

وَهُوَ الْغَفُورُ الْوَدُودُ ﴿١٤﴾

Naye Ni Mwingi wa Kughufuria, Mwenye Upendo halisi. [Al-Buruwj (85:14)]

 

 

Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) Ni Mwenye Kusitiri dhambi za waja Wake, Haonyeshi dhambi ya mja Wake yeyote kwa mja mwingine. Ni Mwenye Kughufuria makosa ya waja wake muda baada ya muda hadi katika idadi isiyohesabika, kila mara mja anapotubia, Naye Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) Anaendelea Kumghufuria.

 

 

Faida, Mafunzo Tuyapatayo Na Jinsi Ya Kufanyia Kazi Jina Hili La Allaah, Al-Ghafuwr, Al-Ghaffaar:

 

1-Binaadam ni mwenye kukosea na kutenda dhambi, lakini aliye mbora zaidi ni yule mwenye kutubia kwa Al-Ghafuwr ili aghufuriwe madhambi yake. Amethibitisha hayo Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) aliposema:

 

 كل ابن آدم خطّاء وخير الخطّائين التوابون     رواه الترمذي وحسنه الألباني

“Kila mwanaadam ni mkosa, na mbora mwenye kukosa ni yule anayetubia.”  [Imepokelewa na At-Tirmidhiy na Shaykh Al-Albaaniy amesema ni Hadiyth Hassan]

 

2-Kimbilia kuomba maghfirah kama Anavyoamrisha Al-Ghafuwr katika Kauli Yake:

 

وَسَارِعُوا إِلَىٰ مَغْفِرَةٍ مِّن رَّبِّكُمْ وَجَنَّةٍ عَرْضُهَا السَّمَاوَاتُ وَالْأَرْضُ أُعِدَّتْ لِلْمُتَّقِينَ﴿١٣٣﴾ 

Na kimbilieni maghfirah kutoka kwa Rabb wenu, na Jannah upana wake ni wa mbingu na ardhi imeandaliwa kwa wenye taqwa. [Aal-‘Imraan (3:1330]

 

 

3-Kumbuka kwamba hata Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) ambaye ameshaghufuriwa madhambi yake, lakini alikuwa akiomba maghfirah kwa wingi kila siku kwa dalili ifuatayo: 

 

 

 عن الأَغَرِّ المزني رضي الله عنه: أنَّ رسُول اللهِ صلى الله عليه وسلم قال : (( إنَّهُ لَيُغَانُ عَلَى قَلْبِي ، وإنِّي لأَسْتَغفِرُ اللهَ في اليَوْمِ مِئَةَ مَرَّةٍ )) . رواه مسلم .

Al-Agharri Al-Mazany (Radhwiya Allaahu 'anhu) amesema: Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: " Kwa hakika wakati mwengine huwa nikihisi moyo wangu umeghumiwa. Kwa hakika mimi humuomba Allaah maghfirah mara mia kwa siku. [Muslim]   

 

 

4-Jua kwamba Al-Ghafuwr Anafurahi mja Wake anapotambua kuwa hakuna wa kumghufuria madhambi isipokuwa Yeye. Imethibiti katika Hadiyth ifuatayo ya kuhusu duaa ya kipando:

 

عن عَلِي بن ربيعة ، قَالَ : شهدت عليَّ بن أَبي طالب رضي الله عنه ، أُتِيَ بِدَابَّةٍ لِيَرْكَبَهَا ، فَلَمَّا وَضَعَ رِجْلَهُ في الرِّكَابِ ، قَالَ : بِسْمِ اللهِ ، فَلَمَّا اسْتَوَى عَلَى ظَهْرِهَا ، قَالَ : الحَمْدُ للهِ الَّذِي سَخَّرَ لَنَا هَذَا وَمَا كُنَّا لَهُ مُقْرِنينَ ، وَإنَّا إِلَى رَبِّنَا لَمُنْقَلِبُونَ ، ثُمَّ قَالَ : الحمْدُ للهِ ، ثَلاثَ مَرَّاتٍ ، ثُمَّ قَالَ : اللهُ أكْبَرُ ، ثَلاثَ مَرَّاتٍ ، ثُمَّ قَالَ : سُبْحَانَكَ إنّي ظَلَمْتُ نَفْسِي فَاغْفِرْ لِي إنَّهُ لاَ يَغْفِرُ الذُّنُوبَ إِلاَّ أنْتَ ، ثُمَّ ضَحِكَ ، فَقيلَ : يَا أمِيرَ المُؤمِنِينَ ، مِنْ أيِّ شَيْءٍ ضَحِكْتَ ؟ قَالَ : رَأيتُ النبيَّ صلى الله عليه وسلم فَعَلَ كَمَا فَعَلْتُ ثُمَّ ضَحِكَ ، فقُلْتُ : يَا رسول اللهِ ، مِنْ أيِّ شَيْءٍ ضَحِكْتَ ؟ قَالَ : ((  إنَّ رَبَّكَ تَعَالَى يَعْجَبُ مِنْ عَبدِهِ إِذَا قَالَ : اغْفِرْ لِي ذُنُوبِي ، يَعْلَمُ أنَّهُ لاَ يَغْفِرُ الذُّنُوبَ غَيْرِي )) رواه أَبُو داود والترمذي ، وقال: ((حديث حسن))، وفي بعض النسخ: ((حسن صحيح )) . وهذا لفظ أَبي داود .

 

 'Aliy bin Rabiy’ah (Radhwiya-Allaahu ‘anhu) amesema: Nimemshuhudia 'Aliy bin Abiy Twaalib (Radhwiya-Allaahu ‘anhu) akiletewa mnyama ampande. Alipoweka mguu wake kwenye kipando alisema:

 

بِسْمِ اللهِ

Alipolingana juu ya mgongo wake alisema:

 

الحَمْدُ للهِ الَّذِي سَخَّرَ لَنَا هَذَا وَمَا كُنَّا لَهُ مُقْرِنينَ ، وَإنَّا إِلَى رَبِّنَا لَمُنْقَلِبُونَ    

Kisha akasema:

 الحمْدُ للهِ

 

AlhamduliLlaah (Himdi Anastahiki Allaah) (mara tatu).

 

Kisha akasema:

اللهُ أكْبَرُ
 

Allaahu Akbar (Allaah Ni Mkubwa) (mara tatu).

 

Kisha akasema:

 

سُبْحَانَكَ إنّي ظَلَمْتُ نَفْسِي فَاغْفِرْ لِي إنَّهُ لاَ يَغْفِرُ الذُّنُوبَ إِلاَّ أنْتَ

Kutakasika ni Kwako, hakika mimi nimedhulumu nafsi yangu, basi Nighufurie, kwani hakuna mwenye kughufuria dhambi ila Wewe. 

 

Kisha akacheka. Akaulizwa: Ee Amiri wa Waumini! Unacheka nini?

 

Akasema: Nilimuona Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akifanya kama nilivyofanya, kisha akacheka. Nikamuuliza: Ee Rasuli wa Allaah! Unacheka nini? Akasema: “Hakika Rabb wako Anamridhia mja Wake anaposema: Nighufurie dhambi zangu akijua kuwa hakuna anayeghufuria dhambi isipokuwa Yeye (Allaah).”

 

[Abuu Daawuwd na At-Tirmidhiy, amesema ni Hadiyth Hasan. Na katika baadhi ya mapokezi ni Hadiyth Hasan Swahiyh, na hii ni lafdhi ya Abuu Daawuwd]

 

Na duaa kama hiyo takriban, imethibiti katika Hadiyth ifuatayo:

 

 عَنْ أَبِي بَكْرٍ اَلصِّدِّيقِ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُ  أَنَّهُ قَالَ لِرَسُولِ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم{ عَلِّمْنِي دُعَاءً أَدْعُو بِهِ فِي صَلَاتِي . قَالَ قُلْ : "اَللَّهُمَّ إِنِّي ظَلَمْتُ نَفْسِي ظُلْمًا كَثِيرًا ، وَلَا يَغْفِرُ اَلذُّنُوبَ إِلَّا أَنْتَ ، فَاغْفِرْ لِي مَغْفِرَةً مِنْ عِنْدِكَ ، وَارْحَمْنِي ، إِنَّكَ أَنْتَ اَلْغَفُورُ اَلرَّحِيمُ}  مُتَّفَقٌ عَلَيْهِ

Kutoka kwa Abuu Bakr Asw-Swiddiyq (Radhwiya-Allaahu ‘anhu) amepokea   kuwa alimuambia Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) Nifundishe du’aa ya kuomba katika Swalaah yangu. Akasema: Sema:

 اَللَّهُمَّ إِنِّي ظَلَمْتُ نَفْسِي ظُلْمًا كَثِيرًا ، وَلَا يَغْفِرُ اَلذُّنُوبَ إِلَّا أَنْتَ ، فَاغْفِرْ لِي مَغْفِرَةً مِنْ عِنْدِكَ ، وَارْحَمْنِي ، إِنَّكَ أَنْتَ اَلْغَفُورُ اَلرَّحِيمُ

“Allaahumma inniy dhwalamtu nafsiy dhwulman kathiyran, walaa yaghfirudh-dhunuwba illaa Anta, faghfir-liy maghfiratan min ‘Indika, war-hamniy, Innaka Antal-Ghafuwrur-Rahiym.”

 

Ee Allaah, hakika mimi nimedhulumu nafsi yangu dhulma nyingi, wala hapana wa kughufiria dhambi isipokuwa Wewe, kwa hivyo naomba unighufirie maghfirah Yako na unirehemu, Hakika Wewe ni Mwingi wa kughufuria, Mwenye kurehemu. [Al-Bukhaariy, Muslim]

 

Na duaa ifuatayo inaitwa sayyid al-istighfaar kama ilivyothibiti katika Hadiyth ifuatayo:

 

وَعَنْ شَدَّادِ بْنِ أَوْسٍ‏ رضى الله عنه قَالَ: قَالَ رَسُولُ اَللَّهِ‏ صلى الله عليه وسلم ‏{سَيِّدُ اَلِاسْتِغْفَارِ، أَنْ يَقُولَ اَلْعَبْدُ: اَللَّهُمَّ أَنْتَ رَبِّي، لَا إِلَهَ إِلَّا أَنْتَ، خَلَقْتَنِي، وَأَنَا عَبْدُكَ، وَأَنَا عَلَى عَهْدِكَ وَوَعْدِكَ مَا اِسْتَطَعْتُ، أَعُوذُ بِكَ مِنْ شَرِّ مَا صَنَعْتُ، أَبُوءُ لَكَ بِنِعْمَتِكَ عَلَيَّ، وَأَبُوءُ لَكَ بِذَنْبِي، فَاغْفِرْ لِي; فَإِنَّهُ لَا يَغْفِرُ اَلذُّنُوبَ إِلَّا أَنْتَ} أَخْرَجَهُ اَلْبُخَارِيُّ

Kutoka kwa Shaddaad bin Aws (Radhwiya-Allaahu ‘anhu): Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: “Bwana wa Istighfaar ni mja kusema:

 

اَللَّهُمَّ أَنْتَ رَبِّي، لَا إِلَهَ إِلَّا أَنْتَ، خَلَقْتَنِي، وَأَنَا عَبْدُكَ، وَأَنَا عَلَى عَهْدِكَ وَوَعْدِكَ مَا اِسْتَطَعْتُ، أَعُوذُ بِكَ مِنْ شَرِّ مَا صَنَعْتُ، أَبُوءُ لَكَ بِنِعْمَتِكَ عَلَيَّ، وَأَبُوءُ لَكَ بِذَنْبِي، فَاغْفِرْ لِي; فَإِنَّهُ لَا يَغْفِرُ اَلذُّنُوبَ إِلَّا أَنْتَ

Ee Allaah, Wewe ni Rabb wangu, hapana mwabudiwa wa haki ila Wewe, umeniumba mimi na mimi ni mja Wako, nami niko juu ya  ahadi Yako, na agano Lako, kiasi cha uwezo wangu, najikinga Kwako kutokana na shari ya nilichokifanya, nakiri  Kwako kwa kunineemesha, na nakiri kwa madhambi yangu, basi nakuomba unighufurie  kwani hakuna wa kughufuria  madhambi ila Wewe.” [Imetolewa na Al-Bukhaariy]

 

 

5-Usikate tamaa kuomba maghfirah kwa Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) unapotenda madhambi hata yawe mengi vipi, kwa sababu Yeye ni Al-Ghafuwr na Anaweza kukughufuria madhambi yote Akitaka kama Anavyosema:

 

 

قُلْ يَا عِبَادِيَ الَّذِينَ أَسْرَفُوا عَلَىٰ أَنفُسِهِمْ لَا تَقْنَطُوا مِن رَّحْمَةِ اللَّـهِ ۚ إِنَّ اللَّـهَ يَغْفِرُ الذُّنُوبَ جَمِيعًا ۚ إِنَّهُ هُوَ الْغَفُورُ الرَّحِيمُ﴿٥٣﴾

Sema: Enyi Waja Wangu ambao wamepindukia mipaka juu ya nafsi zao: Msikate tamaa na Rehma ya Allaah, hakika Allaah Anaghufuria dhambi zote. Hakika Yeye Ndiye Mwenye Kughufuria, Mwenye Kurehemu. [Az-Zumar (39:53)]

 

 

6-Usiwe mwenye kuyelezea madhambi ya wenzako kwa watu, bali yasitiri, kwani utakapositiri aibu na makosa ya mwenzako, basi nawe utasitiriwa madhambi yako Siku ya Qiyaamah na Al-Ghafuwr:

 

 

عن ابْنَ عُمَرَ (رضي الله عنهما)  أَنَّ رَسُولَ اللَّهِ (صلى الله عليه و آله وسلم) قَالَ: ((الْمُسْلِمُ أَخُو الْمُسْلِمِ لاَ يَظْلِمُهُ ولاَ يُسْلِمُهُ، وَمَنْ كَانَ فِي حَاجَةِ أَخِيهِ كَانَ اللَّهُ فِي حَاجَتِهِ، وَمَنْ فَرَّجَ عَنْ مُسْلِمٍ كُرْبَةً فَرَّجَ اللَّهُ عَنْهُ كُرْبَةً مِنْ كُرُبَاتِ يَوْمِ الْقِيَامَةِ، وَمَنْ سَتَرَ مُسْلِمًا سَتَرَهُ اللَّهُ يَوْمَ الْقِيَامَةِ)) متفق عليه

Amehadithia Ibn ‘Umar (Radhwiya-Allaahu ‘anhumaa):  Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: “Muislamu ni ndugu wa Muislamu, hamdhulumu wala hamsalimishi (kwa adui). Na atakayemtimizia haja nduguye, Allaah Atamtimizia haja yake. Na atakayemfariji (atakayemuondoshea) Muislamu dhiki yake, Allaah Atampa faraja ya dhiki zake Siku ya Qiyaamah. Na atakayemsitiri Muislamu mwenzake (aibu zake), Allaah Atamsitiri (aibu zake) Siku ya Qiyaamah.” [Al-Bukhaariy na Muslim]

 

 

7-Tambua ndugu Muislamu kwamba hata kujistiri mtu nafsi yake kutokana na madhambi yake, ni jambo ambalo limeamrishwa, hivyo basi tahadhari kwamba kutoa siri ni miongoni mwa madhambi makubwa. Na Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) Hamsamehe mwenye kufichua maasi yake ilhali Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) Amemsitiri. Hadiyth ya Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) ifuatayo inathibitisha:  

 

عن ابي هُرَيْرَةَ، يَقُولُ سَمِعْتُ رَسُولَ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم يَقُولُ: (( كُلُّ أُمَّتِي مُعَافًى إِلاَّ الْمُجَاهِرِينَ، وَإِنَّ مِنَ الْمَجَانَةِ أَنْ يَعْمَلَ الرَّجُلُ بِاللَّيْلِ عَمَلاً، ثُمَّ يُصْبِحَ وَقَدْ سَتَرَهُ اللَّهُ، فَيَقُولَ: يَا فُلاَنُ عَمِلْتُ الْبَارِحَةَ كَذَا وَكَذَا، وَقَدْ بَاتَ يَسْتُرُهُ رَبُّهُ وَيُصْبِحُ يَكْشِفُ سِتْرَ اللَّهِ عَنْهُ )) البخاري ‏

 

Amehadithia Abuu Hurayrah (Radhwiya-Allaahu ‘anhu):  Nimemisikia Rasuli wa Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) akisema: “Dhambi za Ummah wangu zitasamehewa isipokuwa za Al-Mujaahiriyn (wanaotenda maasi waziwazi au wanaofichua maasi yao kwa watu.  Mfano wa kufichua huko siri ni mtu anayetenda kitendo usiku kisha akaamka hali ya kuwa Allaah Amemsitiri, lakini anasema: Ee fulani, jana usiku nilitenda kadhaa wa kadhaa, ilhali amekesha usiku akiwa katika sitara ya Rabb wake lakini yeye asubuhi anajifichulia sitara ya Allaah.” [Al-Bukhaariy]

 

 

Share