034-Majina Ya Allaah Mazuri Na Sifa Zake أسماء الله الحسنى وصفاته: AT-TAWWAAB

 

 

 

أسماء الله الحسنى وصفاته

Majina Ya Allaah Mazuri Na Sifa Zake

 

 

Alhidaaya.com

 

التَّوَّاب

 

034-At-Tawwaab

 

 

 

At-Tawwaab: Mwingi Wa Kukubali Tawbah

 

 

Ni Ambaye Anawawezesha kutubu waja Wake Awatakao na kuwakubalia kutubu kwao.

 

 

Jina hili limekariri mara kadhaa katika Qur-aan, miongoni mwa Aayah ni zifuatazo:

 

رَبَّنَا وَاجْعَلْنَا مُسْلِمَيْنِ لَكَ وَمِن ذُرِّيَّتِنَا أُمَّةً مُّسْلِمَةً لَّكَ وَأَرِنَا مَنَاسِكَنَا وَتُبْ عَلَيْنَا ۖ إِنَّكَ أَنتَ التَّوَّابُ الرَّحِيمُ ﴿١٢٨﴾

Rabb wetu, Tujaalie tuwe wenye kujisalimisha Kwako pamoja na kizazi chetu wawe ummah wenye kujisalimisha Kwako, na Tuonyeshe taratibu za ibaada zetu na Pokea tawbah zetu, hakika Wewe Ni Mwingi wa Kupokea Tawbah, Mwenye Kurehemu.  [Al-Baqarah (2:128)]

 

 

وَاللَّذَانِ يَأْتِيَانِهَا مِنكُمْ فَآذُوهُمَا ۖ فَإِن تَابَا وَأَصْلَحَا فَأَعْرِضُوا عَنْهُمَا ۗ إِنَّ اللَّـهَ كَانَ تَوَّابًا رَّحِيمًا ﴿١٦﴾ 

Na wale wawili wanaofanya huo (uchafu) waadhibuni. Wakitubu na wakajirekebisha basi waacheni. Hakika Allaah Ni Mwingi wa Kupokea Tawbah, Mwenye Kurehemu. [An-Nisaa (4:16)]

 

 

أَلَمْ يَعْلَمُوا أَنَّ اللَّـهَ هُوَ يَقْبَلُ التَّوْبَةَ عَنْ عِبَادِهِ وَيَأْخُذُ الصَّدَقَاتِ وَأَنَّ اللَّـهَ هُوَ التَّوَّابُ الرَّحِيمُ﴿١٠٤﴾

 

Je, hawajui kwamba Allaah Ndiye Anayekubali tawbah ya Waja Wake, na Anapokea swadaqa, na kwamba Allaah Ndiye Mwingi wa Kupokea Tawbah, Mwenye Kurehemu. [At-Tawbah (9:104)]

 

فَسَبِّحْ بِحَمْدِ رَبِّكَ وَاسْتَغْفِرْهُۚ إِنَّهُ كَانَ تَوَّابًا ﴿٣﴾

Basi hapo sabbih na mhimidi Rabb wako (kwa wingi zaidi) na muombe maghfirah. Hakika Yeye daima Ni Mwingi mno wa Kupokea tawbah. [An-Naswr (110:3)]

 

 

Tawbah ni mja kurudia kwa Rabb wake kumuomba Amsamehe madhambi yake na kuacha hizo dhambi kwa sura zote. 

 

 

Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) Ndiye At-Tawwaab. Amejisifu Mwenyewe kuwa ni At-Tawwaab, kwa wingi wa kuwapokea wenye kurudia Kwake kuomba maghfirah na msamaha na kurejea tendo hilo mara kwa mara, moja baada ya jengine kwa muda mrefu, na Allaah kuwakubalia Anaowataka kuwakubalia, Akawa ni At-Tawwaab kama Anavyosema:

 

غَافِرِ الذَّنبِ وَقَابِلِ التَّوْبِ شَدِيدِ الْعِقَابِ ذِي الطَّوْلِ ۖ لَا إِلَـٰهَ إِلَّا هُوَ ۖ إِلَيْهِ الْمَصِيرُ﴿٣﴾

Mwenye Kughufuria dhambi, Anayepokea tawbah, Mkali wa Kuakibu Mwenye wingi wa Ukarimu, hakuna Muabudiwa wa haki ila Yeye, Kwake ndio mahali pa kuishia. [Ghaafir (40:3)]

 

Na Anasema pia:

 

وَهُوَ الَّذِي يَقْبَلُ التَّوْبَةَ عَنْ عِبَادِهِ وَيَعْفُو عَنِ السَّيِّئَاتِ وَيَعْلَمُ مَا تَفْعَلُونَ﴿٢٥﴾

Naye Ndiye Ambaye Anapokea tawbah kutoka kwa Waja Wake, na Anasamehe maovu, na Anayajua mnayoyafanya. [Ash-Shuwraa (42:25)]

 

 

Na kwa sababu maasi yanatendwa na waja Wake na kurudiwa kutendwa mara kwa mara, ndio maana Akajiita kwa tamko la kukuza jambo hili la kupokea tawbah mara kwa mara ili aweze kupokea madhambi makubwa kwa tawbah pana. Yeye Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) Anapokea tawbah za waja Wake. Na kama ilivyokariri tawbah Yake kadhalika na kukubali kwake kumekariri, hadi kusikokuwa na mwisho, Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):

 

 

فَمَن تَابَ مِن بَعْدِ ظُلْمِهِ وَأَصْلَحَ فَإِنَّ اللَّـهَ يَتُوبُ عَلَيْهِ ۗ إِنَّ اللَّـهَ غَفُورٌ رَّحِيمٌ ﴿٣٩﴾

Lakini atakayetubia baada ya dhulma yake na akarekebisha matendo yake na kuwa mwema, basi hakika Allaah Atapokea tawbah yake. Hakika Allaah Ni Mwingi wa Kughufuria, Mwenye Kurehemu. [Al-Maaidah (4:39)]

 

 

Na tawbah ya mja kwa Rabb wake, imezingirwa na tawbah ya Allaah. Tawbah hiyo ya mja inatanguliwa na Allaah Mwenyewe kwa kuwa Ameshamkubalia na kumuwafikisha na kuutingisha moyo wake kuelekea kwenye tawbah yenyewe, Basi mja kurudia kutubia kwa Allaah, huwa ni tawfiq ya Rabb wake. Kisha Allaah Hukubali tawbah yake. Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) Anasema:

 

  ثُمَّ تَابَ عَلَيْهِمْ لِيَتُوبُوا ۚ إِنَّ اللَّـهَ هُوَ التَّوَّابُ الرَّحِيمُ﴿١١٨﴾

 

Kisha (Allaah) Akapokea tawbah yao, ili watubie. Hakika Allaah Yeye Ndiye Mwingi wa Kupokea Tawbah, Mwenye Kurehemu. [At-Tawbah (9:118)]

 

 

Faida, Mafunzo Tuyapatayo Na Jinsi Ya Kufanyia Kazi Jina Hili La Allaah At-Tawwaab:

 

 

1-Kila unapotenda dhambi, rudia haraka kwa Rabb wako kwa sababu Yeye At-Tawaab Anapenda wenye kurudia kutubia Kwake kama Anavyosema:

 

إِنَّ اللَّـهَ يُحِبُّ التَّوَّابِينَ وَيُحِبُّ الْمُتَطَهِّرِينَ ﴿٢٢٢﴾ 

Hakika Allaah Anapenda wenye kutubia na Anapenda wenye kujitwaharisha. [Al-Baqarah (2:222)]

 

Na Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema katika Hadiyth ifuatayo kwamba Allaah Anapokea tawbah nyakati zote zile mja anaporudia Kwake kutubia:

 

 

عن أبي موسَى عبدِ اللهِ بنِ قَيسٍ الأشْعريِّ رضي الله عنه عن النَّبيّ صلى الله عليه وسلم، قَالَ: ((إنَّ الله تَعَالَى يَبْسُطُ يَدَهُ بالليلِ لِيَتُوبَ مُسِيءُ النَّهَارِ، ويَبْسُطُ يَدَهُ بالنَّهَارِ لِيَتُوبَ مُسِيءُ اللَّيلِ، حَتَّى تَطْلُعَ الشَّمْسُ مِنْ مَغْرِبِها)). رواه مسلم

Amesimulia Abuu Muwsa, 'Abdullaah bin Qays Al-Ash’ariyy (Radhwiya Allaahu ‘anhu): Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: “Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) Hunyoosha Mkono Wake usiku ili yule aliyekosea mchana apate kutubia, na Hunyoosha mkono Wake mchana ili yule aliyekosea usiku apate kutubia, (hali hiyo huendelea) mpaka jua lichomozapo upande wa magharibi”  [Muslim]

 

 

Na Hadiyth ifuatayo inaonyesha jinsi gani At-Tawwaab Anavyofurahi pindi mja Wake anaporudia kwake kutubia hata kama alikosea bila ya kukusudia katika kuomba kwake tawbah:

 

عن أَنَسُ بْنُ مَالِكٍ قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم: ((الَلَّهُ أَشَدُّ فَرَحًا بِتَوْبَةِ عَبْدِهِ حِينَ يَتُوبُ إِلَيْهِ مِنْ أَحَدِكُمْ كَانَ عَلَى رَاحِلَتِهِ بِأَرْضِ فَلاَةٍ فَانْفَلَتَتْ مِنْهُ وَعَلَيْهَا طَعَامُهُ وَشَرَابُهُ فَأَيِسَ مِنْهَا فَأَتَى شَجَرَةً فَاضْطَجَعَ فِي ظِلِّهَا قَدْ أَيِسَ مِنْ رَاحِلَتِهِ فَبَيْنَا هُوَ كَذَلِكَ إِذَا هُوَ بِهَا قَائِمَةً عِنْدَهُ فَأَخَذَ بِخِطَامِهَا ثُمَّ قَالَ مِنْ شِدَّةِ الْفَرَحِ: "اللَّهُمَّ أَنْتَ عَبْدِي وَأَنَا رَبُّكَ" ‏ أَخْطَأَ مِنْ شِدَّةِ الْفَرَحِ)) مسلم

Amesimulia Anas (Radhwiya-Allaahu ‘anhu) Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: “Allaah Hufurahikiwa mno na tawbah ya mja Wake wakati anapotubia Kwake kuliko furaha ya mmoja wenu aliyekuwa amempanda mnyama wake kwenye jangwa (la joto kali hakuna mtu), kisha mnyama huyo aliyebeba chakula chake na maji yake akampotea, na akakata tamaa kabisa ya kumpata tena. Akaenda kwenye mti, akalala chini ya kivuli chake huku akiwa amekata tamaa kabisa ya kumpata tena mnyama wake. Akiwa katika hali hiyo (ya kutojua nini la kufanya), mara anashtuka kumwona huyo amesimama mbele yake, akaikamata hatamu yake, na kwa ile furaha akasema:  Ee Allaah, Wewe ni mja wangu na mimi ni Rabb wako. Alikosea (kumshukuru Rabb wake) kwa wingi wa furaha aliyokuwa nayo.” [Muslim]

 

 

 

2-Soma duaa baada ya wudhuu ambayo ina fadhila ya kufunguliwa milango minane ya Jannah:

 

عن عمر بن الخطاب رضي اللهُ عنه ، عن النبيِّ صلى الله عليه وسلم ، قَالَ : ((مَا مِنْكُمْ مِنْ أحَدٍ يَتَوَضَّأُ فَيُبْلغُ – أَوْ فَيُسْبِغُ – الوُضُوءَ ، ثُمَّ يقول : أشهَدُ أنْ لا إلهَ إِلاَّ اللهُ وَحْدَهُ لاَ شَرِيكَ لَهُ ، وَأشْهَدُ أنَّ مُحَمَّداً عَبْدُهُ وَرَسُولُهُ ؛ إِلاَّ فُتِحَتْ لَهُ أَبْوَابُ الجَنَّةِ الثَّمَانِيَةُ يَدْخُلُ مِنْ أَيِّهَا شَاءَ )) رواه مسلم .

وزاد الترمذي : ((  اللَّهُمَّ اجْعَلْنِي مِنَ التَّوَّابِينَ ، وَاجْعَلْنِي مِنَ المُتَطَهِّرِينَ )) .

 

Amesimulia 'Umar bin Al-Khatwaab (Radhwiya Allaahu 'anhu): Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Hakuna yeyote mingoni mwenu anatawadha vizuri au akaeneza wudhuu, kisha akasema:

 

 

  أشهَدُ أنْ لا إلهَ إِلاَّ اللهُ وَحْدَهُ لاَ شَرِيكَ لَهُ ، وَأشْهَدُ أنَّ مُحَمَّداً عَبْدُهُ وَرَسُولُهُ  اللَّهُمَّ اجْعَلْنِي مِنَ التَّوَّابِينَ ، وَاجْعَلْنِي مِنَ المُتَطَهِّرِينَ

Nashuhudia kuwa hapana mwabudiwa wa haki isipokuwa Allaah, Peke Yake Hana mshirika. Na nashuhudia kuwa Muhammad ni mja na Rasuli Wake. Ee Allaah! Nijaalie katika miongoni mwa wenye kutubia na nijaalie katika wenye kujitakasa.   

 

Isipokuwa itafunguliwa milango minane ya Jannah ataingia katika mlango wowote autakao." [Muslim, At-Tirmidhiy]

 

 

3-Kimbilia kurudia kwa At-Tawwaab kutubia Kwake kabla ya kufika nyakati ambazo tawbah hazitapokelewa tena:

 

a-Kabla ya kufikia sakaraatul-mawti:

 

Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):

 

إِنَّمَا التَّوْبَةُ عَلَى اللَّـهِ لِلَّذِينَ يَعْمَلُونَ السُّوءَ بِجَهَالَةٍ ثُمَّ يَتُوبُونَ مِن قَرِيبٍ فَأُولَـٰئِكَ يَتُوبُ اللَّـهُ عَلَيْهِمْ ۗ وَكَانَ اللَّـهُ عَلِيمًا حَكِيمًا ﴿١٧﴾

Hakika tawbah inayokubaliwa na Allaah ni ya wale wanaofanya uovu kwa ujahili kisha wakatubia haraka, basi hao Allaah Anapokea tawbah yao. Na Allaah Ni Mjuzi wa yote, Mwenye Hikmah wa yote.

 

 

وَلَيْسَتِ التَّوْبَةُ لِلَّذِينَ يَعْمَلُونَ السَّيِّئَاتِ حَتَّىٰ إِذَا حَضَرَ أَحَدَهُمُ الْمَوْتُ قَالَ إِنِّي تُبْتُ الْآنَ وَلَا الَّذِينَ يَمُوتُونَ وَهُمْ كُفَّارٌ ۚ أُولَـٰئِكَ أَعْتَدْنَا لَهُمْ عَذَابًا أَلِيمًا ﴿١٨﴾ 

Lakini tawbah si kwa wale wanaofanya maovu mpaka mauti yanapomjia mmoja wao ndipo aseme: Hakika mimi sasa nimetubu. Na wala wale wanaokufa na hali wao ni makafiri. Hao Tumewaandalia adhabu iumizayo. [An-Nisaa (4:17-18)]

 

 

Na katika Hadiyth: 

 

قال صلى الله عليه وسلم: ((إِنَّ الله عزَّ وجَلَّ يقْبَلُ توْبة العبْدِ مَالَم يُغرْغرِ)) رواه أحمد والترمذي وصححه النووي

Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: “Hakika Allaah ‘Azza wa Jalla  Huikubali tawbah ya mja Wake kabla ya roho kufika kwenye mkoromo wa mauti.: [Imesimuliwa na Ahmad na At-Tirmidhiy na kusahishwa na An-Nawawiy]

 

b-Kabla ya alama mojawapo ya Qiyaamah, nayo ni jua kuchomoza upande wa Magharibi:

 

عن أبي هريرة رضي الله عنه أن النبي صل قال : ((مَنْ تَابَ قَبْلَ أَنْ تَطْلُعَ الشَّمْسُ مِنْ مَغْرِبِهَا، تَابَ اللَّهُ عَلَيْهِ)) رواه مسلم

 

Amehadithia Abuu Hurayrah (Radhwiya Allaahu ‘anhu): Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: “Atakayetubu kabla ya kuchomoza jua upande wa Magharibi, Allaah   Atamkubalia tawbah yake.” [Muslim]

 

 

4-Na kimbilia kutubia kwa At-Tawwaab kabla ya moyo kupofuka kabisa:

 

 

عن أبي هُرَيرة، قال: قال رسول الله صلى الله عليه وسلم: ((إنَّ العبدَ إذا أخطأَ خطيئةً نُكِتت في قلبِهِ نُكْتةٌ سوداءُ، فإذا هوَ نزعَ واستَغفرَ وتابَ سُقِلَ قلبُهُ، وإن عادَ زيدَ فيها حتَّى تعلوَ قلبَهُ، وَهوَ الرَّانُ الَّذي ذَكَرَ اللَّه عز وجل ((كَلاَّ بَلْ رَانَ عَلَى قُلُوبِهِم مَّا كَانُوا يَكْسِبُونَ)) رواه أحمد والترمذي وحسنه الألباني

Amehadithia Abuu Hurayrah (Radhwiya Allaahu ‘anhu):  Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: “Mja anapofanya dhambi, doa jeusi (kutu) huwekwa katika moyo wake.  Akiacha dhambi hiyo, na kuomba maghfirah na kutubia, moyo wake husafishwa ukawa msafi, lakini akirudia kufanya dhambi, doa (kutu)  huzidi kuenea  mpaka kufunika moyo wote na hiyo ndio 'Raan'  (kutu)  aliyosema Allaah ('Azza wa Jalla)  ‘

كَلَّاۖ بَلْۜ رَانَ عَلَىٰ قُلُوبِهِم مَّا كَانُوا يَكْسِبُونَ ﴿١٤﴾

Laa hasha! Bali yamefanya kutu juu ya nyoyo zao yale waliyokuwa wakiyachuma [Al-Mutwaffifiyn (83:14)] [Ahmad, At-Tirmidhiy na Shaykh Al-Albaaniy amesema ni Hasan]

 

 

5-Rudia kwa At-Tawwaab utubie tawbah ya naswuwhaa (ya kwelikweli) kama Anavyotuamrisha katika Kauli Yake:

 

 

أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا تُوبُوا إِلَى اللَّـهِ تَوْبَةً نَّصُوحًا عَسَىٰ رَبُّكُمْ أَن يُكَفِّرَ عَنكُمْ سَيِّئَاتِكُمْ وَيُدْخِلَكُمْ جَنَّاتٍ تَجْرِي مِن تَحْتِهَا الْأَنْهَارُ يَوْمَ لَا يُخْزِي اللَّـهُ النَّبِيَّ وَالَّذِينَ آمَنُوا مَعَهُ ۖ نُورُهُمْ يَسْعَىٰ بَيْنَ أَيْدِيهِمْ وَبِأَيْمَانِهِمْ يَقُولُونَ رَبَّنَا أَتْمِمْ لَنَا نُورَنَا وَاغْفِرْ لَنَا ۖ إِنَّكَ عَلَىٰ كُلِّ شَيْءٍ قَدِيرٌ﴿٨﴾

Enyi walioamini! Tubieni kwa Allaah tawbah ya nasuha (kwelikweli), asaa Rabb   wenu Akakufutieni maovu yenu, na Akakuingizeni Jannaat zipitazo chini yake mito. Siku ambayo Allaah Hatomfedhehesha Nabiy (Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) na wale walioamini pamoja naye. Nuru yao itatembea mbele yao na kuliani mwao, watasema: Rabb wetu! Tutimizie Nuru yetu, na Tughufurie, hakika Wewe juu ya kila kitu Ni Muweza. [At-Tahriym (66:8)]

 

 

6-Utakaporudia kwa At-Tawwaab kutubia, basi ufuate masharti ya kutubia, yakiwemo (i) Kuomba maghfirah (ii) Kuacha hayo maasi (iii) Kujuta (v) Kama mtu amedhulumu haki ya mwengine, basi ni kuirudisha hiyo  haki (iv) Kuweka niya na azimio ya kutokurudia tena maasi hayo,  badala yake kutenda mema, kwani hivyo ndio kutubia kwelikweli kabisa. Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):

 

إِلَّا مَن تَابَ وَآمَنَ وَعَمِلَ عَمَلًا صَالِحًا فَأُولَـٰئِكَ يُبَدِّلُ اللَّـهُ سَيِّئَاتِهِمْ حَسَنَاتٍ ۗ وَكَانَ اللَّـهُ غَفُورًا رَّحِيمًا ﴿٧٠﴾

Isipokuwa yule aliyetubu na akaamini na akatenda amali njema. Basi hao Allaah Atawabadilishia maovu yao kuwa mema. Na Allaah daima Ni Mwingi wa Kughufuria, Mwenye Kurehemu.

 

 

وَمَن تَابَ وَعَمِلَ صَالِحًا فَإِنَّهُ يَتُوبُ إِلَى اللَّـهِ مَتَابًا ﴿٧١﴾

Na atakayetubu na akatenda mema, basi hakika yeye anatubia kwa Allaah tawbah ya kweli. [Al-Furqaan (25:70-71)]

 

 

 

7-Kumbuka kwamba hata Muumini anatakiwa awe mwenye kurudia kwa At-Tawwaab kutubia kwa sababu hakuna binaadam asiyefanya makosa. Basi Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) Anawataka Waumini pia warudia Kwake kutubia na Anaambatanisha kufaulu kwa kurudia kutubiwa Kwake kama Anavyosema:

 

وَتُوبُوا إِلَى اللَّـهِ جَمِيعًا أَيُّهَ الْمُؤْمِنُونَ لَعَلَّكُمْ تُفْلِحُونَ ﴿٣١﴾

Na tubuni kwa Allaah nyote, enyi Waumini mpate kufaulu. [An-Nuwr (24:31)]

 

 

 

8-Duaa za kuomba tawbah ni nyingi katika Qur-aan na Sunnah, miongoni mwa za Sunnah ni ifuatayo:

 

اللَّهُمَّ أغْفِرْ لِي وَتُبْ عَلَيَّ إِنَّكَ أَنْتَ ألتَّوَابُ  الْغَفُورُ

Allaahumma-ghfirliy watub ‘alayya innaka Antat-Tawwaabul-Ghafuwr

Ee Allaah nighufurie na nipokelee tawbah yangu, hakika Wewe ni Mwingi wa Kupokea Tawbah, Mwingi wa Kughufuria. [Abuu Daawuwd, At-Tirmidhiy, An-Nasaaiy, Ibn Maajah Taz Majma’ Az-Zawaaid (10/113)]

 

 

 

 

Share