04-Swahiyh Fiqh As-Sunnah: Kitabu Cha Ndoa: Mahari: Mahari Ni Haki Ya Mwanamke Na Si Mawalii Wake
Swahiyh Fiqh As-Sunnah
كِتَابُ الزَّوَاجِ
Kitabu Cha Ndoa
الصَّدَاقُ
Mahari
04: Mahari Ni Haki Ya Mwanamke Na Si Mawalii Wake:
Ni kwa Neno Lake Ta’aalaa:
"وَآتُوا النِّسَاءَ صَدُقَاتِهِنَّ نِحْلَةً"
“Na wapeni wanawake mahari zao kwa maridhawa.” [An-Nisaa: 04]
Na Kauli Yake:
"فَمَا اسْتَمْتَعْتُم بِهِ مِنْهُنَّ فَآتُوهُنَّ أُجُورَهُنَّ فَرِيضَةً"
“Basi mliostarehe nao, wapeni mahari yao kuwa ni waajib”. [An-Nisaa: 24]
Pamoja na Aayaat nyinginezo zinazoonyesha kwamba mahari ni haki ya mwanamke. Hivyo si halali kwa baba yake wala mwingine yeyote kuchukua chochote katika mahari yake bila idhini yake. Na kwa ajili hiyo, Mashaafi’iy na Mahanbali wanasema kwamba haijuzu kwa mume kulipa mahari kwa asiye mke au mwakilishi wake au yeyote aliyeidhinisha apokee.