08-Swahiyh Fiqh As-Sunnah: Kitabu Cha Ndoa: Mahari: Mahari Anayostahiki Mwanamke Na Hali Zake: Hali Zinazolazimu Apewe Mahari Kamili (b) Mke Akikaa Mwaka Mzima Kwenye Nyumba Ya Mumewe Hata Bila Ya Kuingiliwa
Swahiyh Fiqh As-Sunnah
كِتَابُ الزَّوَاجِ
Kitabu Cha Ndoa
الصَّدَاقُ
Mahari
08: Mahari Anayostahiki Mwanamke Na Hali Zake: Hali Zinazolazimu Apewe Mahari Kamili (b) Mke Akikaa Mwaka Mzima Kwenye Nyumba Ya Mumewe Hata Bila Ya Kuingiliwa:
Kwa mujibu wa kauli ya Wamaalik, ikiwa mtu ameoa mke, na mke akapelekwa kwake, halafu akakaa kwake mwaka mzima bila kumuingilia, basi ni lazima atoe mahari kamili kwa mujibu wa Wamaalik.
Ninasema: “Sioni dalili yoyote kuhusiana na wao kuainisha kipindi cha mwaka mmoja. Lau mwanamke atapelekwa kwa mumewe, na akakaa bila kumuingilia, hili litarejeshwa kwenye hali iliyotangulia kuelezwa (faragha sahihi inayozingatiwa). Yaliyoelezwa huko ndiyo yatakayosemwa kuhusiana na hili”.
