09-Swahiyh Fiqh As-Sunnah: Kitabu Cha Ndoa: Mahari: Mahari Anayostahiki Mwanamke Na Hali Zake: Hali Zinazolazimu Apewe Mahari Kamili (c) Talaka Ya Kukimbia (Mke Asirithi) Katika Maradhi Ya Umauti Kabla Ya Kumuingilia

 

Swahiyh Fiqh As-Sunnah

 

كِتَابُ الزَّوَاجِ

 

Kitabu Cha Ndoa

 

 

الصَّدَاقُ

 

Mahari

 

 

Alhidaaya.com

 

 

 

09:  Mahari Anayostahiki Mwanamke Na Hali Zake:  Hali Zinazolazimu Apewe Mahari Kamili  (c)  Talaka Ya Kukimbia (Mke Asirithi) Katika Maradhi Ya Umauti Kabla Ya Kumuingilia:

 

 

Kwa mujibu wa Mahanbali, ikiwa mume atamtaliki mkewe ambaye hakuwahi kumuingilia katika ugonjwa ambao hatima yake kwa asilimia kubwa ni umauti ili mke asiambulie mirathi, na mume akafariki kweli, basi ni lazima apewe mahari kamili (kwa mujibu wa Mahanbali), kwa sababu ni lazima mke akae eda katika hali hii madhali hajaolewa au kuritadi.

 

 

Share