12-Swahiyh Fiqh As-Sunnah: Kitabu Cha Ndoa: Mahari: Kusamehe Mwanamke Mahari Au Yule Ambaye Fungamano La Ndoa Liko Mikononi Mwake

 

Swahiyh Fiqh As-Sunnah

 

كِتَابُ الزَّوَاجِ

 

Kitabu Cha Ndoa

 

 

الصَّدَاقُ

 

Mahari

 

 

Alhidaaya.com

 

 

 

 

12:   Kusamehe Mwanamke Mahari Au Yule Ambaye Fungamano La Ndoa Liko Mikononi Mwake:

 

 

Allaah Mtukufu Amesema:

 

"وَإِن طَلَّقْتُمُوهُنَّ مِن قَبْلِ أَن تَمَسُّوهُنَّ وَقَدْ فَرَضْتُمْ لَهُنَّ فَرِيضَةً فَنِصْفُ مَا فَرَضْتُمْ إِلَّا أَن يَعْفُونَ أَوْ يَعْفُوَ الَّذِي بِيَدِهِ عُقْدَةُ النِّكَاحِ ۚ وَأَن تَعْفُوا أَقْرَبُ لِلتَّقْوَىٰ ۚ وَلَا تَنسَوُا الْفَضْلَ بَيْنَكُمْ ۚ إِنَّ اللَّـهَ بِمَا تَعْمَلُونَ بَصِيرٌ" 

 

“Na mkiwataliki kabla ya kuwagusa na mkawa mmeshawabainishia mahari yao, basi (wapeni) nusu ya hayo mliyobainisha isipokuwa wakisamehe au asamehe yule ambaye fungamano la ndoa liko mikononi mwake.  Na kusamehe kuko karibu zaidi na taqwa. Na wala msisahau fadhila baina yenu.  Hakika Allaah Ni Mwenye Kuona yote myatendayo”.  [Al-Baqarah: 237]

 

Maana ya aayah hii tukufu ni kwamba mwanamke akitalikiwa na mumewe kabla hajamuingilia, na mume akawa amembainishia kiasi cha mahari yake, naye akawa ameridhia kiasi hicho, basi ni haki yake apewe nusu ya mahari hiyo, isipokuwa kama mwenyewe atasamehe nusu hiyo na kumwachia mwanamume, au asamehe yule ambaye fungamano la ndoa liko mkononi mwake.

 

‘Ulamaa wamekhitilafiana katika kauli mbili kuhusu maana ya mtu ambaye fungamano la ndoa liko mkononi mwake. 

 

Kauli ya kwanza:

 

Ni walii wa mwanamke.  Walii anaweza kusamehe nusu ya mahari aliyostahiki mwanamke.

 

Kauli ya pili:

 

Ni mume mwenyewe.  Hapa maana inakuwa:  Au mume mwenyewe asamehe na akampa mwanamke mahari kamili.

 

Mwelekeo wa taawili hii ni imara zaidi.  Kwa sababu mahari ni haki ya mwanamke kama ilivyoelezwa nyuma, haijuzu kwa yeyote kutia mkono wake kuigusa ila kwa idhini yake.  Ni haki yake kabla ya talaka na baada ya talaka.

 

Basi yeyote kati ya wawili atakayesamehe haki yake, basi anakuwa karibu zaidi na taqwa, na Allaah Ndiye Mjuzi zaidi.

 

 

Share