13-Swahiyh Fiqh As-Sunnah: Kitabu Cha Ndoa: Mahari: Ikiwa Zitatajwa Mahari Mbili
Swahiyh Fiqh As-Sunnah
كِتَابُ الزَّوَاجِ
Kitabu Cha Ndoa
الصَّدَاقُ
Mahari
13: Ikiwa Zitatajwa Mahari Mbili:
Ikiwa watu wa mke watamtaka mume ataje mahari mbili; moja kwa ajili ya ‘aqdi, na nyingine kwa ajili ya kutangazwa hadhirani kwa lengo la kujifaharishia kwa watu na si kwamba ndio inayomlazimu kutoa, hapa Jumhuwr ya ‘Ulamaa -kinyume na Mahanbali- wanasema kwamba atatoa iliyobainishwa kwenye ‘aqdi, na si ile iliyotangazwa mbele za watu. Ni chaguo pia la Sheikh wa Uislamu.