02-Swahiyh Fiqh As-Sunnah: Kitabu Cha Ndoa: Walima Wa Harusi: Kualika Watu

 

Swahiyh Fiqh As-Sunnah

 

كِتَابُ الزَّوَاجِ

 

Kitabu Cha Ndoa

 

 

 

وَلِيْمَةُ العُرْسِ

 

Walima Wa Harusi

 

 

Alhidaaya.com

 

 

 

02:  Kualika Watu:

 

Inapendeza kwa mwenye kuoa awaalike watu wema, ni sawa wakiwa mafukara au matajiri kutokana na neno lake Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam):

 

 "لاَ تُصَاحِبْ إِلاَّ مُؤْمِنًا وَلاَ يَأْكُلْ طَعَامَكَ إِلاَّ تَقِيٌّ"

 

“Usisuhubiane ila na Muumini tu, na asile chakula chako isipokuwa mchajimungu tu”.  [Abu Daawuwd (4811) na At-Tirmidhiy (2506).  Al-Albaaniy kasema ni Hasan]

 

Pia inapendeza zaidi akitenga sehemu maalum ya chakula hicho kwa ajili ya mafukara na masikini.  Katika Hadiyth ya Abu Hurayrah (Radhwiya Allaah ‘anhu), Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:

 

"شَرُّ الطَّعَامِ طَعَامُ الْوَلِيمَةِ يُدْعَى لَهَا الْأَغْنِيَاءُ وَيُتْرَكُ الْفُقَرَاءُ، وَمَنْ تَرَكَ الدَّعْوَةَ فَقَدْ عَصَى الله وَرَسُولَه"

 

“Chakula cha shari zaidi ni chakula cha walima.  Hualikwa kuja kula matajiri na masikini wakaachwa.  Na atakayesusa mwaliko, basi hakika amemuasi Allaah na Rasuli Wake”.  [Al-Bukhaariy (5177) na Muslim (1432)] 

 

 

 

Share