05-Swahiyh Fiqh As-Sunnah: Kitabu Cha Ndoa: Walima Wa Harusi: Pongezi Kwa Maharusi

Swahiyh Fiqh As-Sunnah

 

كِتَابُ الزَّوَاجِ

 

Kitabu Cha Ndoa

 

 

وَلِيْمَةُ العُرْسِ

 

Walima Wa Harusi

 

 

Alhidaaya.com

 

 

 

05:  Pongezi Kwa Maharusi::

 

Katika mambo mazuri kabisa tuliyofundishwa na Uislamu, ni Muislamu kumpongeza nduguye Muislamu kwa kheri yoyote anayoipata, na kumwombea baraka, kudumu kwa neema na kuishukuru.  Hivi ndivyo alivyokuwa akifanya Rasuli wa Allaah (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam).  Alikuwa akimwombea aliyeoa baraka, umri mrefu na tawfiyq ya kudumu.

 

Maneno Ya Kupongeza:

 

Imepokelewa:
 

"أنَّ النَّبيَّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ كانَ إذا رفَّأَ الإنْسَانَ إِذَا تزوَّجَ قالَ: بارَكَ اللَّهُ لَكَ، وبارَكَ علَيكَ، وَجَمعَ بَينَكُمَا فيْ خَيْرٍ"

 

“Kwamba Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa anapompongeza mtu na kumwombea baada ya kuoa humwambia:  Allaah Akubarikie, Akuteremshie barakah Zake, na Awatangamanishe kati yenu ndani ya kheri zote”.   [Hadiyth Swahiyh.  Swahiyh Abu Daawuwd (2130)]

 

Toka kwa ‘Aaishah (Radhwiya Allaah ‘anhaa), amesema:

 

"تَزَوَّجَنِي النَّبِيُّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ فَأَتَتْنِي أُمِّي فَأَدْخَلَتْنِي الدَّارَ، فَإِذَا نِسْوَةٌ مِنَ الأَنْصَارِ فِي الْبَيْتِ فَقُلْنَ عَلَى الْخَيْرِ وَالْبَرَكَةِ، وَعَلَى خَيْرِ طَائِرٍ‏"

 

“Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alinioa.  Mama yangu akaja kunichukua akaniingiza nyumbani.  Nikashtukizwa kuwakuta wanawake wa Kianswaar wako ndani wakinisubiri, na hapo hapo wakaniombea wakisema:  Uingie kwa kheri na barakah, uingie na fali njema”.  [Swahiyhul Bukhaariy (5156)]

 

Muislamu anatakiwa ashikamane na matamshi haya ya pongezi na aachane na mengineyo ambayo yanaweza kutoka nje ya mstari wa dini.

 

Kadhalika, mbali na maneno mazuri ya pongezi, inapendeza kuwapa maharusi zawadi.  Na asili ya hili ni Hadiyth ya Anas aliyesema: 

 

"لَمَّا تَزَوَّجَ النَّبِيُّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ زَيْنَبَ أَهْدَتْ لَهُ أُمُّ سُلَيْمٍ حَيْسًا فِي تَوْرٍ مِنْ حِجَارَةٍ "

 

“Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alipomwoa Zaynab, Ummu Sulaym alimzawadia “hays” kwenye bakuli la mawe.”  [Muslim (1428)

 

“Hays” ni tende zilizotolewa kokwa, zikachanganywa na samli au unga.

 

 

Share