Marekebisho Yanayohusiana Na Kuelewa Kimakosa Taariykh (Historia) Ya "Uwahabi"

 

Marekebisho Yanayohusiana Na Kuelewa

Kimakosa Taariykh (Historia) Ya “Uwahabi”

 

Muhammad bin Sa'd Ash-Shuway'ir

 

Bismillaahi R-rahmaanir-Rahiym

 

 

Alhidaaya.com

 

 

Inanipasa hapa nimfahamishe msomaji sababu zilizonielekeza mimi katika kuandika makala haya ya marekebisho yanayohusiana na kuelewa kimakosa Taariykh (Historia) ya “Uwahabi” kwani Allaah Amekipangilia kila kitu kuwa na sababu zake. Mjadala ufuatao, uliozalisha hoja zenye misingi ya kielimu, na mazao yenye mazungumzo yaliyo na uongofu, ndiyo sababu zilizonitia hima kuandika makala haya.

 

Katika mwaka wa 1407H, nilihusika kwenye shughuli muhimu za kibiashara huko Mauritania, na baadae tukaelekea katika nchi ya Senegal, na hatimae, mpangilio wa usafiri wa ndege ukatulazimu kubakia katika ufalme wa nchi ya Morocco kwa muda wa siku sita.

 

Na katika siku mojawapo ya hizo siku sita, nilibahatika kufanya urafiki na mwalimu mmoja wa chuo kikuu hapo aitwae Dr. 'Abdullaah. Na katika kikao kimoja, kwenye maktaba yake, pakawa na mazungumzo mengi sana. Kutokamana na mapenzi aliyokuwa nayo ya Ufalme, na kuhudhuria kwake kwenye vikao vya kielimu pale mjini, alinitupia suali lifuatalo mbele ya wale waliokuwepo katika kikao hicho na idadi yao ilikuwa takriban Mashaykh kumi na mbili, tena miongoni mwao wakiwemo wanati waheshimiwa wamiji.

 

Akasema, "Sisi twaupenda ufalme, na roho za Waislamu pamoja na nyoyo zao ziko tayari nao (huo ufalme) kwa hali na mali, na baina yetu na wewe kunapatikana mapenzi na maelewano, hata utashangaa jinsi mawalii na wanavyuoni katika ufalme huu walivyoendeleza juhudi za kuwa waaminifu, kwa Uislaam pamoja na Waislam wenyewe, lakini ingelikuwa ni uzuri ulioje lau kama nyote mungeliwachana na haya madh-hab ya Wahaabiyyah, ambayo yaliyowatenganisha Waislam?!"

 

Basi nikamjibu, "Pengine huwenda ikawa una fahamu za kimakosa, zilizochukuliwa kutoka katika asili yenye makosa, lakini tungelipendezwa kulijadili suala hili, mbele ya halaiki hii ya ndugu zetu, kwa hoja zenye misingi ya kielimu, zikiandamana na ushahidi mpaka zituwasilishe kunako mapatano ya fahamu zetu..." Kisha nikasema, "Na kwa vile kila mtu ameridhika, na kutosheka moyo wake, kwa yale yaliyoandikwa na Wanavyuoni kutoka katika miji yao, basi kwenye mjadala huu, sitokwenda kufanya utafiti ulioko nje ya maktaba hii, iliyozungukwa na kuta hizi nne, kwa sababu kama munionavyo mimi sikubeba hata kitabu kimoja, na wala sikuutarajia mjadala huu.

 

Na kwa hivyo, kabla ya kuanza, nataraji yakwamba mjadala huu utaepukana na ushupavu na upendeleo, au ukurubishaji wa miswada bila ya ushahidi wenye kuunga mkono kikamilifu, kwa sababu kutafuta ukweli ndiyo makusudiwa yetu, na kuridhika na maamrisho ya Allaah na Nabiy wake (swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) ndiyo malengo yetu, na kuinusuru dini ndiyo matumaini tunayoyatarajia."

 

Akasema, mimi nakubaliana na wewe juu ya suala hili, na hawa Mashaykh waheshimiwa ndiwo watakao kuwa mahakimu baina yetu."

 

Nikasema, "Nimeridhika na hayo, na baada ya kujitegemeza kwa Allaah, sasa nakusubiri kuwasilisha utangulizi wa mjadala huu."

 

Akasema, "Chukulia mfano, yale yaliyosemwa na al- Wanshariysiy katika kitabu chake kiitwacho al- Mi'yaar mijaladi 11, nayo ni maneno yake: Aliulizwa Al- Lakhami kuhusu watu katika kijiji ambacho Mawahabi wamejenga msikiti, ni nini hukmu ya kuswali ndani ya msikiti huwo?"

 

Vilevile kwa kuwapasha habari: Kitabu hichi al- Mi'yaar, ni kitabu kilichokusanya fatwaa za Ki-fiqh kulingana na madh-hab ya Imaam Maalik, kilikusanywa na Ahmad bin Muhammad al- Wanshareesi, na kikachapishwa mijalada 13, na uchapishaji wenyewe umetekelezwa na Serikali ya Morocco, na wakasambaza chapa hizo kwa njia ya misaada.

 

Baada ya kuwasilisha suali, na kukitaja kitabu hicho, mjalada wa 11, mimi nikamjibu: yakwamba fatwaa kuhusu suala hilo ni ya sawa, na tunakubaliana na al-Lakhami katika yaliyokwisha elezwa kwenye fatwaa yake.

 

Akasema, "Kwa hivyo tumeafikiana kuhusu kundi hili, na makosa waliyonayo, haswa zaidi, kutokana na alivyosema mufti: kundi hili ni ma-Khawaarij wapotofu na ni makafiri, Allaah Akikatilie mbali kizazi chao katika ardhi hii, na msikiti unawajibika kuvunjwa, pamoja na kuwafukuza kutoka katika ardhi za Waislamu."

 

Nikasema, "Bado hatujaafikiana, tungali katika awali za mjadala huu... na nitawafahamisha yakwamba fatwaa hii ina mfano wake tangu kabla ya Al-Lakhami na baada yake zilizowahi kutokea kwa wanavyuoni wa Hispania, na wanavyuoni wa Afrika ya Kaskazini, na haya yametokana na hukmu ya Rasuli wa Allaah kuwahusu ma-Khawaarij, ambao 'Aliy ibn Abi Twaalib (Allaah Awe radhi nae), alipopigana nao huko Nahrawaan.

 

Na kwenye mjadala wetu huu tutawasili, apendapo Rabb, katika marekebisho ya taarekh (Historia) iliyoeleweka kimakosa, kuhusu makusudio ya kundi hili, ambalo wanavyuoni wa Ki-Islamu kutoka Hispania na Afrika ya Kaskazini na wanaofanana nao waliotoa Fatwaa kuhusiana nao, na kuhusu jina walosingiziwa nalo kuwa ni sifa ya makosa ya ulinganizi wa urekebishaji wa Shaykh Muhammad bin 'Abdil-Wahhaab, Rehma za Allaah ziwe juu yake. Marekebisho haya hayatofaulu isipokuwa yaandamane na ushahidi, ambao unaokuridhisha, kwa sababu sisi sote tunatarajia kuwasili kwenye ukweli wa mas-ala yenyewe... na hali nzuri ya fahamu iliyo na utulivu ndicho kitu kitakacho kutuondolea upofu na kutusaidia katika kurekebisha tashwishi hii.” Akasema, “Sisi sote tunatarajia kuwasili katika Ukweli..”

 

Kisha akasema, "na baada ya fatwaa hii, tungelipendelea utuletee ulicho nacho, na sisi tutakusikiliza pamoja na ndugu zetu ambao watakaotoa hukmu baina yetu, nao watahukumu kulingana na yatakayosemwa au yatakayowasilishwa kwao iwapo ni ya sawa au ya makosa."

 

Nikasema, "Mutajionea, Akipenda Rabb, yale ambayo yatakayong'arisha njia katika kufichua mas-ala haya, kwa yule apendeleae kufika kwenye rai iliyo ya sawa, na kwa haya: tutaanza na kilichoko mbele yenu kutoka katika mijalada ya al-Mi’yaar …. Waweza kutusomea kutoka kwenye Gamba la kitabu ili ndugu zetu waweze kusikiya?

 

Akasema, "Unamaanisha fatwaa, yaani niwasomee, au nianze na maelezo yaliyoko kwenye gamba la nje? Nikasema, “Gamba la nje…..au gamba la ndani, yote hayo ni sawa, vyovyote…..”

 

Akaanza kusoma, "Al-Kitaab al- Ma'rib Fiy Fataawaa Ahl Al-Maghrib, kilikusanywa na: Ahmad bin Muhammad al- Wanshariysiy aliyekufa 914H mjini Fez, Morocco. Nikasema kumwambia Shaykh aliyekuwa na umri zaidi ya waliohudhuria pale, alikuwa ndiye anaestahiwa zaidi na khulka yake ni mtu mkarimu sana. Jina lake ni Ahmad, "Ee Shaykh Ahmad, hebu andika tarehe ya kifo cha muandishi Ahmad al- Wanshariysiy ...” nae akaandika kama mwaka wa 914H.

 

Kisha nikasema, "Tunaweza kuleta taarekh (historia) ya al- Lakhami ?”

Akasema, "Naam..." akasimama na kuelekea kwenye rafu (shelf) miongoni mwa marafu ya maktaba na akaleta mjalada kutoka kwenye vitabu vya taarekh, na ndani yake ikawemo taarekh ya: ‘Ali bin Muhammad al- Lakhami, ambae ni Mufti wa Hispania na Afrika ya Kaskazini na taarekh yenyewe ikawa ni ndefu, ndani yake mulikuwa na sifa zake na daraja yake ya ilimu... nikasema, "Kuna mstari wa mashairi mwishoni mwa taarekh yake: kwa hivyo alikufa lini yeye?

Msomaji akasema, "... na alikufa katika mwaka wa 478H.”

 

Nikamwambia Shaykh Ahmad, “Andika tarehe aliyokufa Shaykh ‘Ali al- Lakhami, nae akaandika mwaka wa 478H”. Hapo Daktari ‘Abdullaah akasema, “Kwani wewe una shaka na Wanavyuoni wetu na fatwaa zao? Nikasema, “na ni kitu gani kilichokuelekeza kwenye shaka? Kisha nikawageukia Mashaykh…. Nikasema: Nishawahi kusema kitu chochote kinachoitisha kuwe na shaka katika matamshi yangu?.” Hapo hapo likaja jawabu, kuwa njia ya muwafaka, la kukanusha.

 

Nikasema, "Ili niweze kukanusha shaka hii kunihusu mimi, na kutoka kwa wanavyuoni wa nchi yangu, kwani sisi twawaheshimu na kuwakirimu wao, na tunajisalimisha na fatwaa zao zilizoandamana na ushahidi kutoka katika Kitabu Kitakatifu, na yale yaliyosihi kutoka katika Sunnah za Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayi wa aalihi wa sallam). Hatahivyo, kuwasili mahali hapo kutoka tulipoanzia mazungumzo yetu hapo mwanzoni, imeungana na yale aliyotumia kama ushahidi wake, na yanahitaji uvumilivu na subira.

 

Na kutokamana na yale yatakayo hamasisha majibu ni kwamba: Ningelipenda kuwauliza kila mmoja wenu hapa: Jee inawezekana kwa wanavyuoni kuwahi kutoa fatwaa kuhusu kanuni za Imani ambazo mtetezi wake, ambae aliyehusishwa na imani hiyo, bado hajawahi hata kuja hapa ulimwenguni, au watoe hukmu kuhusu pote fulani miongoni mwa makundi chungu nzima ambalo halijawahi kuwepo??!!"

 

Wote wakasema, "Laa...na hilo ni jambo lisiloweza kujulikana, isipokuwa lile ambalo riwaya zitokazo kwa Nabiy Muhammad (swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) kuhusiana na jambo hilo zimepokelewa. Na hayo ni miongoni mwa miujiza ya Utume, na kwa mara nyingi hayo huja kwa njia ya sifa bila ya kutaja jina."

 

Nikasema, "Maneno yangu nikimkusudia yule ambae mapambano haya ni baina yetu, "Wewe huamini, kama wanavyoamini wengine, ya kwamba Uwahabi kwanza ulianzishwa na Muhammad bin 'Abdil-Wahhaab huko Najd ?” Akajibu, "Hapana shaka."

 

Nikasema, "Kwa hakika Shaykh Muhammad bin 'Abdil-Wahhaab; alipotoa fatwaa yake al-Lakhami, pamoja na wengine miongoni mwa msururu wa wanavyuoni wa ki-Maalik huko Hispania, na wale wakutoka Afrika ya Kaskazini, palikuwa na zaidi ya vizazi 22 ambavyo hata havijawahi kuzaliwa, tukichukulia ya kwamba katika kila karne (miaka mia moja) kunapatikana vizazi vitatu. Kama ilivyo baina ya kifo cha ‘Abdul-Wahhaab bin Rustum na kifo cha Shaykh Muhammad bin 'Abdil-Wahhaab palikuwepo na takriban vizazi 31. Si Wanavyuoni wenu, wala Wanavyuoni wa Kiislamu wanaojua mambo yaliyofichamana, na sisi tunaamini ya kwamba wao hawahusiki na mambo ya uchawi wala uganga, na kuzungumza mambo wasiyoyajua, kama alivyosema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) kama alivyofasiriwa:

 

قُل لَّا يَعْلَمُ مَن فِي السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ الْغَيْبَ إِلَّا اللَّـهُ ۚ وَمَا يَشْعُرُونَ أَيَّانَ يُبْعَثُونَ ﴿٦٥﴾

 

Sema: Hakuna katika mbingu na ardhi ajuaye ghayb isipokuwa Allaah. Na wala hawatambui lini watafufuliwa. [An-Naml: 65]

 

Akasema: Hebu nifafanulie zaidi...!!

 

Nikasema: Kwa hakika Shaykh Muhammad bin 'Abdil-Wahhaab alizaliwa katika mwaka wa 1115H, na akafa katika mwaka wa 1206H, na baina yake na Ahmad Al-Wanshareesi, aliyeandika kitabu cha al-Mi'yaar, na yule aliyenukuu fatwaa ya Al- Lakhami - kama tulivyoona - ni miaka 292 kulingana na tarehe za vifo vyao. Kama ilivyo baina ya Shaykh Muhammad bin 'Abdil-Wahhaab na Al- Lakhami, ambae ndie muanzilishi wa fatwaa hiyo, kuna miaka 728, kulingana na tarehe za vifo vyao, na kulingana na alivyoandika Shaykh Ahmad kuhusu tarehe walizokufia kila mmoja wao.

 

Na twakisiya, kwa hayo, na wale wote ambao waliopitisha fatwaa, kutoka kwa wanavyuoni wa Hispania na Afrika ya Kaskazini, kuwahusu hawa ma-Wahabi...

 

Akasema, "Waweza kufafanua zaidi yale ambayo ulokusudia... kwa ushahidi wa kutosha?

 

Nikasema: "Haikuwahusu Wanavyuoni wa Hispania na Afrika ya Kaskazini kutoa fatwaa kuwahusu ma-Wahabi na kutoa maonyo dhidi yao, isipokuwa tu kutokana na ukweli wa kwamba walikuwemo miongoni mwao, kinyume chao kupatikana katika miji mengine ya Kiislamu. Ash-Shahrastaani alivitaja Vikundi vyao na akatoa uchambuzi kuwahusu wao kwenye kitabu "al- Milal wan Nihal" kama alivyo fanya Ibn Hazm katika kitabu chake "Al-Fiswal Fiy Al- Milal Wal-Ahwaa Wan-Nihal.

 

Na katika mazungumzo yetu, unacho kitabu "Al-Firaq Al-Islaamiyyah Fiy Shimaal Ifriyqiyyah," kilichoandikwa na Mfaransa: Verdibel, na kufasiriwa kwa lugha ya kiarabu na ‘Abdur-Rahmaan Badawi... nacho ni kitabu kimoja tu.
 

Akasema: Hiki hapa ninacho... kisha akasimama na kukichukuwa kutoka kwenye sarafu.

 

Nikasema: "Tutasoma karibu na mwisho wake, tafuta Herufi "WAAW"... nae akasoma moja wapo: Al-Wahabiyyah au Al-Wahhaabiyyah: Kundi la ‘Ibaadhi Khaariji lililoanzishwa na ‘Abdul-Wahhaab bin ‘Abdur-Rahmaan bin Rustum, Al- Khaariji Al-‘Ibaadhi, na likaitwa kundi hilo Al- Wahhaabiyyah baada ya jina lake. Alibadilisha sheriya ya Kiislamu, akafutilia mbali Hajj, hata pakatokea vita chungu nzima baina yake na wapinzani wake... mpaka akasema: Alikufia katika mwaka wa 197H, kwenye mji wa Taahirat ulioko Afrika ya Kaskazini, na akahadithia ya kwamba kundi hili lilichukuwa jina lake: kwa sababu ya yale waliyoyazuwa ndani ya madh-hab yao ya mageuzi na Imani, na walikuwa wakiwachukia Ma-Shi'ah, kama walivyowachukia Ahl as-Sunnah. Na mtu huyu akasema katika kitabu chake chenye kusifika mno kuhusu makundi ya Uislaam yaliyoko Afrika ya Kaskazini tangu kwenye enzi za ukombozi wa Waarabu hadi kufikia zama za muandishi, karibuni na zama hizi zetu.

 

Wale waloandika kumuhusu ‘Abdul-Wahhaab bin Rustum, wamekhitilafiana maoni yao, kuhusu tarehe ya kifo chake, az-Zarkili amesema katika kitabu chake, Al- A'laam, yakwamba alikufa katika mwaka wa 190 H. Kwa kushikilia tarehe hiyo, nikamwambia pamoja na wale walohudhuria pale: Huu ndiwo Uwahabi uliowatenganisha Waislam, na ndiwo (Uwahabi) ule ambao Hukmu hii (au Fatwaa hii) ulitolewa kuwahusu wao, kutoka kwa Wanavyuoni na Ma-faqeehi wa Hispania na Afrika ya Kaskazini. Kama muonavyo kwenye vitabu vyao vya nguzo za itikadi, na bila ya shaka walikuwa sawa katika yote waliyoyasema kwenye mas-ala hayo.

 

Ama kuhusu da'wah ya Shaykh Muhammad bin 'Abdil-Wahhaab, iliyosaidiwa na Imaam Muhammad bin Sa'ud, Allaah Amrehemu, ambayo ni Salafiyyah iliyo saheeh, ni kinyume cha Ma-Khawaarij na vitendo vyao, kwa sababu ilistawishwa juu ya Kitabu cha Allaah, na yale yaliyo sahihi kutoka katika sunnah za Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu alayhi wa aalihi wa sallam), na yanakataa yale ambayo yanayokwenda kinyume nayo, nayo (da'wah hiyo) ni miongoni mwa Ahl as-Sunnah wal Jama'ah.

       

Na zile chuki zilizosambazwa katika miji ya Uislaam, zilienezwa na maadui wa Uislaam, na Waislam, kutoka kwa Wakoloni pamoja na wengine, kwa madhumuni ya kusababisha mgawanyiko kwenye hadhi zao, kama vile jinsi Wakoloni walivyoteka sehemu kubwa ya Ulimwengu wa Ki-Islam katika zama hizo, na zilikuwa hizo ni nyakati zao za kufana, nao walikuwa wakitambua kutoka kwa maharamia wao walokusudia kuumaliza Uislaam ya kwamba maadui wao wa kwanza walokuwa na ushupavu wa kutaka kustawisha Nguvu zao: Ni Uislaam usokuwa na uharibifu, wenye mfano uliofuata mfumo wa Salaf.

 

Na kwa hivyo wakauona wajihi fulani ambao wanaweza kuutumia kwa makusudi ya kuificha da'wah hii ili waweze kuwafukuza watu, na kuwatenganisha Waislam - kwa sababu lengo lao lilikuwa ni kugawanya na kuwatawala, Na hii ni kwa sababu Salaah ad- Diyn Al-Ayyuubiy (Rahimahu Allaah) hakuwang'owa kutoka katika ardhi za Shaam hadi kwenye sehemu nyengine isipokuwa baada ya kuukomesha utawala wa Faatimiyyah - 'Ubayd Baatiniyyah - katika sehemu za Misri, kisha akawaeneza wanavyuoni wa Ahlus-Sunnah wa kutoka Shaam kwenye ardhi zote za Misri. Kwa hivyo, Misri ikabadilishwa kutoka katika minyororo ya U-Shia’ah wa Baatiniyyah na kuwa katika njia ya Ahl as-Sunnah, na hayo yako wazi katika Ushahidi wake, vitendo vyake na itikadi zake.

 

Kwa hivyo Wakoloni wakahofia marejeo ya matukio, baada ya kuona ya kwamba Taifa la Sunni la Tawhiyd - lililoongozwa na Imaam wawili: Muhammad bin ‘Abdil-Wahhaab, na Muhammad bin Sa'ud, na kisha wale walokuja baada yao - yakuwa kazi zao zinasambaa, na wale wanaoikubali da'wah hiyo walikuwa wakizidi. Na hata nyinyi munaelewa vyema ya kwamba Wakoloni hawakuingia kwenye ardhi za Waislam isipokuwa hutafuta kuwafitini Ahl as-Sunnah, na hujinasibisha na kuwa pamoja na watu wa bid'ah na wenye matamanio, kwa sababu wao ndiwo chombo chao cha kufanya wayatakayo kwenye Ardhi za Ki-Islam.

 

Share