Khomeini Ndani Ya Darubini - 3: Masingizio Ya Khomeini Kwa Rasuli Wa Allaah

Khomeini Ndani Ya Darubini – 3

 Masingizio Ya Khomeini Kwa Rasuli Wa Allaah

 

Imeandikwa na Wajiyh Al-Madini

 

Toleo la Pili

 

Alhidaaya.com

 

 

 

 

Achilia mbali kuwaendea kinyume Imaamu na kughushi uongo dhidi yao, Allaah Amnyime Rehma zake, Khomeini anadai kwamba wote hao wameshindwa kusimamisha msingi wa haki, au kuwaongoza au kuubadili ubinaadamu, anasema:

 

 

‘Rusuli wote walikuja kwa dhumuni la kusimamisha msingi wa haki duniani, lakini wamefeli kufanya hivyo, hata Nabiy Muhammad, wa mwisho katika Nabiy ambaye alikuja kubadili ubinaadamu na kutumia haki pia amefeli. Mtu ambaye atakuja kufanikisha yote haya na kusimamisha msingi wa haki duniani katika rika zote, na kulipiza makosa ni mtarajiwa Mahdi….’

 

 

‘Hivyo mtarajiwa Mahdi ambaye Allaah amemetengea kama ni hazina kwa binaadamu ataihudumia haki duniani kote, na kufanikiwa ambapo Nabiy aliyekuja kabla yake amefeli (!) Sababu kwanini Allaah Subhaanahu wa Ta’aalaa, ameyatenga maisha ya Mahdi, amani iwe juu yake, ni kwamba hamna yeyote miongoni mwa binaadamu mwenye uwezo wa kubeba kazi tukufu kama hii ambayo si Rusuli wala mababu wa Mahdi waliofanikiwa kwa yale waliyokuja nayo…..’

 

Pia ameelezea:

 

‘Kama Mahdi, amani iwe juu yake, ameshafariki, hakutakuwa na yeyote miongoni mwa binaadamu kuuanzisha msingi wa haki na kuutumikia duniani. Hivyo, mtarajiwa Mahdi, amani iwe juu yake, ametengwa kwa ajili ya kazi hii. Hivyo, siku yake ya kuzaliwa, tutamkomboa kwa roho zetu, ni siku adhimu kuliko sikukuku (zote) za Kiislamu, na sikukuu ‘adhimu kwa viumbe (!), kwasababu yeye ataifanya haki na uadilifu kufanikiwa duniani. Ndio sababu kwanini sisi tukubali kwamba siku ya kuzaliwa ya Mahdi ni ‘adhimu kuliko zote. Atakapotokezea, atawaokoa binaadamu kwa (kutokana na) kuharibika kwao, atawaongoza wote katika njia sahihi, ataijaza ardhi kwa haki na kabla yake kwa dhulma. Siku ya kuzaliwa kwa Mahdi ni tukio ‘adhimu kwa Waislamu, na inategemewa kuwa muhimu kuliko siku ya kuzaliwa Nabiy Muhammad. Hivyo, tunajiandaa kwa ujio wa mtarajiwa Mahdi, amani iwe juu yake (!)’.

 

 

Khomeini anaendelea kusema:

 

“Siwezi kumuita (kama ni) kiongozi, kwa sababu ni mtukufu zaidi ya hivyo, bali hata siwezi kumuita binaadamu wa mwanzo kwa sababu hakuna wa kumzidi yeye, hivyo naweza kumueleza yeye kwa maneno ya “muahidiwa (na) mtarajiwa Mahdi” ambaye Allaah Subhaanahu wa Ta’aalaa amemuhifadhi kwa ajili ya binaadamu. Hivyo tuna ulazima wa kujiandaa kumuangalia (!) Kama tutafanikwa, tutakuwa na uwezo wa kuinua vichwa vyetu kwa fakhari juu ya Serikali (na) idara zetu zote. Tunategemea kwamba nchi nyengine zinajitayarisha kwa kutokea Mahdi, amani iwe juu yake, na kuwa tayari kwa ziara yake.”[1]

 

Matamshi hayo juu kutoka kwa Khomeini yana kufru iliyo wazi kwa sababu zifuatazo:

 

 

1-Anamfanyia mzaha na kumpima kwa ulaini Rasuli na Manabii, zaidi ni Rasuli wetu Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam). Sio hivyo tu, bali ameleta dhidi ya Allaah, utukufu ni wake Rabb, shutuma (dhidi ya Allaah) kwa kukosea na kushindwa, kutokuwa na sifa (muafaka) na kuzembea kuuteremsha ujumbe Wake.

 

 

2-Kama huyu mjinga Khomeini anamaanisha kwamba binaadamu wote hawakuitika ujumbe wao, wala hawakuathirika na ujio wao, na kuendelea kwa kutokuwa na imani za unafiki, isimaanishwe kwamba ni kushindwa au kukosa kurithisha kwa upande wa Mjumbe, kwa sababu kuongoka katika njia sahihi kupo ndani ya mikono ya Allaah, utukufu ni wake Rabb. Rasuli anaweza kuwasiliana na kutangaza na kuufikisha ujumbe. Matokeo yote yapo kwa Allaah. Kama Angelitaka kuwaongoza binaadamu kupitia kwa Rasuli, wangeliongoka. Kama Angelitaka kuwapotoa, hakuna yeyote atakayeweza kufanya kitu. Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):

 

فَمَن يُرِدِ اللَّـهُ أَن يَهْدِيَهُ يَشْرَحْ صَدْرَهُ لِلْإِسْلَامِ ۖ وَمَن يُرِدْ أَن يُضِلَّهُ يَجْعَلْ صَدْرَهُ ضَيِّقًا حَرَجًا كَأَنَّمَا يَصَّعَّدُ فِي السَّمَاءِ ۚ  ﴿١٢٥﴾

Basi yule ambaye Allaah Anataka kumhidi, Humfungulia kifua chake kwa Uislamu. Na yule ambaye Anataka kumpotoa, Hufanya kifua chake kuwa na dhiki chenye kubana kama kwamba anapanda kwa tabu mbinguni…[Al-An’aam: 125]

 

 

Hivyo, muongozo na upotovu yote yapo kwenye mikono ya Allaah pekee. Rusuli ni waonyaji tu, watangazaji wa habari njema ambao wamefanya bidii na kutumia nguvu zao kwa ajili ya Allaah.

 

 

Wote kwa pamoja wanastahiki kweli kweli kuwaongoza watu kwenye njia sahihi, lakini uwezo wa Allaah upo juu (zaidi) Allaah Anasema:

 

فَلَعَلَّكَ بَاخِعٌ نَّفْسَكَ عَلَىٰ آثَارِهِمْ إِن لَّمْ يُؤْمِنُوا بِهَـٰذَا الْحَدِيثِ أَسَفًا ﴿٦﴾

Basi huenda ukaiangamiza nafsi yako (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) kwa ajili yao kusikitika kutokuamini kwao usimulizi huu (Qur-aan). [Al-Kahf: 6]

 

 

وَلَوْ شَاءَ رَبُّكَ لَجَعَلَ النَّاسَ أُمَّةً وَاحِدَةً ۖ وَلَا يَزَالُونَ مُخْتَلِفِينَ﴿١١٨﴾ إِلَّا مَن رَّحِمَ رَبُّكَ ۚ وَلِذَٰلِكَ خَلَقَهُمْ ۗ وَتَمَّتْ كَلِمَةُ رَبِّكَ لَأَمْلَأَنَّ جَهَنَّمَ مِنَ الْجِنَّةِ وَالنَّاسِ أَجْمَعِينَ﴿١١٩﴾

Na kama Angetaka Rabb wako, basi Angejaalia watu wote kuwa ni ummah mmoja. Na hawatoacha kukhitilafiana. 119. Isipokuwa yule Aliyemrehemu Rabb wako. Na kwa hivyo ndivyo Amewaumba. Na limetimia neno la Rabb wako (kwamba): Bila shaka Nitajaza Jahannam kwa majini na watu wote pamoja. [Huwd: 118-119]

 

 

Rehma za uongofu zipo kwa Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa). Hekima zake zisizo na mpaka na uadilifu unawaongoza wachache wenye kuamini, na wengi hawaamini, kama anavyosema:

 

وَمَا أَكْثَرُ النَّاسِ وَلَوْ حَرَصْتَ بِمُؤْمِنِينَ ﴿١٠٣﴾

Na wengi wa watu hawatoamini japokuwa utatilia hima. [Yuwsuf:103]

 

 وَقَلِيلٌ مِّنْ عِبَادِيَ الشَّكُورُ ﴿١٣﴾

Na wachache miongoni mwa waja Wangu ni wenye kushukuru. [Sabaa:13]

 

 

Nabiy (yeyote aliyekuja) hawezi kutambulika kuwa ni mwenye kufeli juu ya watu wake wasioamni, wala asitambulike kuwa ni mkosa kwa kutofanikiwa kama wengi wa (hao) watu wamemkataa yeye; wajibu ulikuwa ni kufikisha ujumbe. Kwa upande wa Nabiy wetu Muhammad, hakuna pingamizi yoyote kuwa yeye ni mwenye tawfiyq miongoni mwa Manabii kwa mnasaba wa uongozaji, yeye ana idadi kubwa ya wafuasi, na ameacha nyuma athari kubwa mno Ulimwenguni. Ni yeye ambaye ameuweka msingi wa haki, na ni yeye ambaye Allaah ameusababisha Ummah (huu) kuwa wa bora (na haujapata kutokea) katika mzunguko wa mwanaadamu. Amesimamisha vizazi vitukufu vyenye kutegemewa kwenye uadilifu, huruma, ukweli na elimu. Kupitia kwake Allaah ameondosha ufisadi duniani, akautengua moto na Majusi (waabuduo moto), Akaiangamiza misalaba ya Nasara (Wakristo), akawaondosha Waarabu kwenye upotovu, akafuta dhulma za wafalme wa Persia (Wafursi) na Mapagani wa Roma.

 

 

Hivyo Allaah Ameimarisha kwa ajili yake ujumbe Wake, taifa na haki, na dunia imeng’ara kwa nuru baada ya giza. Walikuwa wapi Wafursi (Persians), Warumi na Bahari ya Waarabu ilikuwa vipi kabla ya kuja kwake? Rasuli wa Allaah ndie bingwa wa mageuzi dunia nzima, kulingana na matamshi ya wasioamini kama ilivyonukuliwa kutoka Encyclopedia Britannica:

 

 

“Tokea mwanzo wa Uislamu, Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesisitiza tabia ya udugu na imani thabiti miongoni mwa wafuasi wake, vyote ambavyo vimesaidia kuendeleza miongoni mwao hisia za ushirikiano wa karibu ambao ulitia nguvu kwa mnasaba wa maarifa yao (ya kale) katika udhalimu na (kulinganisha) kwa chimbuko ya jamii (mpya ya Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) ) ya Makkah.”

 

 

Kama wasioamini wamekubali kwa dhati juu ya ukweli wa kumuheshimu Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam), sasa ni vipi Khomeini anakataa matunda ya Rasuli wa Allaah na Swahaba waliongoka? Pia anakataa matunda ya Imamu aliowatuhumu kutoka Ahlul-Bayt, japokuwa anadai kuwa wana cheo juu zaidi ya Rusuli wote, Manabii na Malaika. Amewaendea kinyume wote na kuwashushia hadhi yao, kuwatuhumu kwamba hakuna yeyote miongoni mwao aliyeweza kusimamisha haki ardhini, au aliyefanikiwa kuibadilisha jamii ya wanaadamu.

 

Jee huku sio kurtadi, na shutuma kwa maneno ya Allaah yenye kumpendelea Nabiy Wake?

 

يَا أَيُّهَا النَّبِيُّ إِنَّا أَرْسَلْنَاكَ شَاهِدًا وَمُبَشِّرًا وَنَذِيرًا ﴿٤٥﴾وَدَاعِيًا إِلَى اللَّـهِ بِإِذْنِهِ وَسِرَاجًا مُّنِيرًا ﴿٤٦﴾

Ee Nabiy! Hakika Sisi Tumekutuma uwe shahidi, na mbashiriaji na mwonyaji. 46. Na mlinganiaji kwa Allaah kwa idhini Yake; na siraji kali yenye nuru. [Al-Ahzaab:45-46]

 

 

Jee hii nuru iliyomulika Ulimwengu mzima, mwangaza wa haki, rehma na muongozo umefeli kuwaelekeza wanaadamu kwenye njia sahihi, na hakufanikiwa kusimamisha msingi wa haki? Kukataa hili hakuna shaka yoyote ni sifa ya ufedhuli kwa maneno ya Allaah, na kukataa mambo yenye kukamatika.

 

 

Kukataa huko na sifa (hizo mbaya zilizotolewa) hazikupata hata kutolewa na vigogo wa wasioamini au wanafiki. Isipokuwa, mataifa yote yasiyoamini yalitamka kwamba Rasuli wa Allaah amesimamisha msingi wa haki katika mtindo wa aina yake ukilinganisha na wale waliokuja kabla yake, na kwamba Makhalifa baada yake na Swahaba zake walieneza elimu, uadilifu, uongofu na nuru kila sehemu. Walikuwa ni mfano bora kwa usafi (wa tabia), elimu na uadilifu haukupata kuonekana kwa mwanaadamu. Ni nani miongoni mwa binaadamu zaidi ya Nabiy, anayeweza kufanana na Abu Bakr as-Swiddiyq au Al-Faruuq ‘Umar kwenye usafi (wa tabia), haki, huruma au uvumilivu? Jee sio wao hao Swahaba wa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Waislamu baada yao ambao waliwaongoa watu kutoka kuwaabudu binaadamu hadi kumuabudu Allaah peke yake, na kuwaokoa wao kutokana na upofu wa dini kwenda uadilifu wa Uislamu? Yeyote ambaye ana chembe ya shaka kuhusiana na haya ni murtadi na asiyekuwa na shukurani ambapo moyo wake umejaa chuki na husda dhidi ya Ummah wa Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam).

 

 

Khomeini bila ya shaka yoyote ameelemeza tuhuma zake kwenye imani yake ya kufru kwamba Swahaba wa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) wote walikuwa ni wanafiki (na) wasaliti isipokuwa watatu mpaka watano miongoni mwao. Na akishirikiana na wenziwe wasioamini Allaah, Wazindiyq kwa pamoja wametoa shutuma za kufr kwa Swahaba bora wa Rusuli ya Allaah, wamewaendea kinyume Mama wa Waumini, wake wa Nabiy, na kuwatolea laana watu bora wa wabora baada ya Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam). Namna hizo za imani si chochote ila ni kufru iliyo wazi, kwasababu wamesingizia maneno ya Allaah kwa ubora wa wamchao Allaah hao. Allaah Anasema:

 

أُولَـٰئِكَ هُمْ خَيْرُ الْبَرِيَّةِ ﴿٧﴾

Hao ndio wema kabisa wa viumbe. [Al-Bayyinah: 7]

 

 

Lakini Khomeini na kundi lake wamejipa moyo kwa ushahidi wa uongo kwamba wao (Swahaba) ni watu waovu kumkaidi Allaah, lakini tunaona kwenye ushahidi sahihi kuwa Yeye (Allaah) Amekuwa Radhwi nao, na kwamba Yeye Amewaelekea kwa huruma. Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):

 

 

لَّقَدْ رَضِيَ اللَّـهُ عَنِ الْمُؤْمِنِينَ إِذْ يُبَايِعُونَكَ تَحْتَ الشَّجَرَةِ فَعَلِمَ مَا فِي قُلُوبِهِمْ فَأَنزَلَ السَّكِينَةَ عَلَيْهِمْ وَأَثَابَهُمْ فَتْحًا قَرِيبًا﴿١٨﴾

Kwa yakini Allaah Amewawia radhi Waumini walipofungamana nawe ahadi ya utiifu (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) chini ya mti, [Al-Fat-h: 18]

 

 

Walikuwa (idadi yao) ni watu alfu moja na mia nne katika (makubaliano) ya Hudaybiyah. Allaah Mtukufu Anasema:

 

لَّقَد تَّابَ اللَّـهُ عَلَى النَّبِيِّ وَالْمُهَاجِرِينَ وَالْأَنصَارِ الَّذِينَ اتَّبَعُوهُ فِي سَاعَةِ الْعُسْرَةِ ..﴿١١٧﴾

Kwa yakini Allaah Amepokea tawbah ya Nabiy na Muhajirina na Answaar ambao wamemfuata (Nabiy صلى الله عليه وآله وسلم) katika saa ya dhiki[At-Tawbah: 117]

 

 

Walikuwa ni alfu thelathini. Aya hii imeshushwa kwa ajili ya kundi hili la Swahaba wa Nabiy, Allaah awe radhi nao wote. Allaah Anasema:

 

وَعَدَ اللَّـهُ الَّذِينَ آمَنُوا مِنكُمْ وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ لَيَسْتَخْلِفَنَّهُمْ فِي الْأَرْضِ كَمَا اسْتَخْلَفَ الَّذِينَ مِن قَبْلِهِمْ ﴿٥٥﴾

Allaah Amewaahidi wale walioamini miongoni mwenu na wakatenda mema kwamba bila shaka Atawafanya makhalifa katika ardhi kama Alivyowafanya makhalifa wale waliokuwa kabla yao,.. [An-Nuwr: 55]

 

 

Hakika Allaah Ametekeleza ahadi Yake kwa kuwafanya Makhalifa kusimamisha Dini yao, na Akawashushia mapenzi yake juu yao, sifa ni Zake. Lakini wasioamini wanasema; hakufanya kitu kama hichi kwa ajili yao. Na kwa upande mwengine, hao Swahaba, Khomeini na watu wake (Mashia) wanasema, wameibadili Dini ya Allaah, baada ya kifo cha Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam), na wakaharibu Kitabu cha Allaah, na wakairithisha ofisi ya Khalifa kwa wale wasiostahiki, na wakauzuia kwa wale wanaostahiki. Hao Mazindiyq wamekufuru maneno ya Allaah na Rasuli Wake na wakaendelea kwenye ukafiri wao, na kumtuhumu ‘Aliy ambao wao wanadai kumpenda zaidi, kwa kuwa wajinga zaidi kuzidai haki zake, au kuwapinga Makhalifa watatu wa mwanzo, Abu Bakr, ‘Umar na ‘Uthmaan (Allaah Awe radhi nao), au kukufuru kwa lengo la kudai kuwa wanabadili shari'ah za Allaah! Khomeini na kundi lake sio tu wamemdhihaki ‘Aliy (Allaah awe radhi naye), lakini pia wameamini kwamba uzembe wa hali ya juu uliofanywa na ‘Aliy ni kumuoza binti yake ‘Umar, ambaye wanaamini kuwa sio Muumini, (ndivyo wanavyodai). Hofu yake ilizidi zaidi hata baada ya kuingia madarakani, na alishindwa kuitoa “Qur-aan iliyofichwa” ya kweli, na uteremsho uliokamilika ambao uliletwa kwa mkewe Faatwimah! Bali alificha yote haya kwa kuwaogopa watu wake! Hivyo yeye kama alivyo Nabiy kabla yake ameshindwa kuufikisha ujumbe wake, sio yeye wala Rasuli wa Allaah aliyeweza kusimamisha msingi wa haki!

 

 

Yaliyo hapo juu ni baadhi tu ya ufupisho wa madhehebu ya Mazindiyq kuhusiana na ‘Aliy bin Abi Twaalib, na Rasuli wa Allaah, ni kutoamini kulikokuwa wazi kabisa. Wamethubutu kuwapiga vita chini ya udhuru wa uongo kwa bidii na kwa (kutumiwa) jina la Uislamu lakini hakika wameficha maneno ya kupendeza (kwa kupandikiza) dharau na uadui. Bado hali inabaki kuwa wanaendelea kumtuhumu ‘Aliy kwa kuwa mjinga mpaka kufa kwake. Khomeini na watu wake kwa ufedhuli (wao) wanamhukumu Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam), ‘Aliy na kizazi chake kuwashusha hadhi kama ilivyoelezwa na Khomeini: “Hata Rusuli, na mababa wa al-Mahdi wameshindwa kwa yale waliyotegemea kushinda.”

 

 

Huyu Mahdi aliyechorwa hakuwahi kuwepo kabla wala hayupo sasa na wala hatatokea. Wanadai kwamba huyo Mahdi asiyedhihirika alikuwa ni mtoto wa miaka mitatu au minne na alimiliki elimu ya dunia hii na pia elimu ya Akhera, ambaye ameingia kwenye tundu (tunnel) huko Samirraa Iraq tokea 260 H, na hakutoka tena. Hili si chochote ila ni kufurutu ada kwenye upumbavu na hadithi (za paukwa pakawa), kwasababu al-Hasan al-Askari (baba wa msingiziwa Mahdi) hakupatapo kuwa na mtoto wa kiume. Ni hadithi za uongo zilizotungwa kuwadanganya Mashia na majeshi yao kwa ajili ya kuzinyonya pesa zao kwa majina ya Imamu kwa kutumia udhuru wa uongo katika nyumba ya Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam). Walipogundua ya kwamba Imamu waliotuhumiwa watakuja kukatizwa (kukatika kabisa kwa Uimamu) kama Imaam wa mwisho hatokuwa na mtoto wa kiume, wakavumbua uongo huu ili kuweka mlango wa uongo wazi dhidi ya Allaah na Ujumbe Wake, na kuendelea kuutafuna utajiri usio halali.

 

 

Sio Qur-aan wala Sunnah iliyoeleza tukio kama hilo. Wala haijapata kudokezwa na Imamu wao yeyote. Imaam aliyebaki kujificha kwa miaka alfu kumi na mbili, na hatoki kutoka kwenye tundu (pango) hastahili kusadikika. Allaah sio msahaulifu. Allaah Ameeleza ndani ya Kitabu Chake matokeo (yajayo) makubwa (mno), kwa ujumla, mpaka siku ya Hukumu, na Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amezungumzia kwa kila tukio lililo dogo na kubwa. Jee itakuwaje iwe sawa kwamba hakuzungumzia kuhusu hadithi ya Imaam ambayo atakuwa na ushawishi mkubwa na baraka kuliko Rusuli na Manabii wote? Jee alizungumzia kuhusu malezi yake, kutokuwepo kwake, kupotea au kutokea tena, au kwa Naibu zake na mzungumzaji mkuu kama Khomeini na wengineo? Jee inastahili kwamba Rasuli wa Allaah amezungumzia kuhusu moto utakaoripuka Madiynah ambapo moshi wake utakuwa ni mrefu sana (hadi) shingo za ngamia wa Basra – Iraq kuweza kuuona, lakini ameacha kutueleza kuhusu tukio kubwa mno ambapo litatokea baada ya kifo chake? Una umuhimu gani moto wa Madiynah ukilinganisha na Mahdi wa Shia (!), ambaye wanaamini kuwa ni Mtukufu kuliko Rusuli, Manabii na Imamu?

 

 

Kwa ufupi, uzushi huu wa Imaam aliyetuhumiwa ni kuzungumzia kwa yasiyoonekana, na ni mafundisho mabaya ya Imani yasiyopatana (kabisa) na yale yaliyotangazwa na Uislamu kuwa kweli. Wakati wakiamini kwamba huyo Imamu waliyemtuhumu kuwa yuhai baada ya miaka mingi bado ni uongo uliotungwa dhidi ya Allaah na ukafiri.

 

 

Madai kwamba siku ya kuzaliwa ya Mahdi ndio sikukuu ‘adhimu kwa binaadamu wote na kwamba atawaongoza watu njia sahihi, imefanywa tu kwa yule ambaye ni mjinga wa yale ambayo Allaah Ameyaanzisha na kuyabainisha kwa watu. Allaah Ameshaamuru kwamba binaadamu wote hawatakusanyika chini ya dini moja, wala kuongoka, hakuna mabadiliko katika Shari'ah za Allaah, Ni lazima wagawike kwenye Waumini na wasioamini.

 

 

Kutokana na hekima za Allaah zisizo na mfano, wale wasioamini wanakuwa ni wengi sehemu zote na wakati wote. Allaah Anasema:

 

وَمَا أَكْثَرُ النَّاسِ وَلَوْ حَرَصْتَ بِمُؤْمِنِينَ ﴿١٠٣﴾

Na wengi wa watu hawatoamini japokuwa utatilia hima. [Yuwsuf: 103]

 

 

وَإِن تُطِعْ أَكْثَرَ مَن فِي الْأَرْضِ يُضِلُّوكَ عَن سَبِيلِ اللَّـهِ ۚ ﴿١١٦﴾

Na kama ukiwatii wengi walioko ulimwenguni, watakupoteza na njia ya Allaah. [Al-An’aam: 116]

 

 وَقَلِيلٌ مِّنْ عِبَادِيَ الشَّكُورُ ﴿١٣﴾

 Na wachache miongoni mwa waja Wangu ni wenye kushukuru. [Sabaa: 13]

 

Khomeini anadai:

 

‘Siku ya kuzaliwa ya Mahdi ni ‘adhimu kwa Waislamu kuliko siku ya kuzaliwa Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam).’

 

 

Huu ni ukafiri ulio wazi kwasababu anaamini Mahdi wa uongo, ambaye si chochote ila ni hadithi za uongo, kuwa na hadhi zaidi ya Rasuli wa Allaah, mbora wa Rusuli na ni ambaye ametunukiwa kuliko binaadamu wote, na ndie kiongozi wao siku ya Hisabu.

 

 

Ijapokuwa kusherehekea siku za kuzaliwa za Rusuli na Manabii wengine haina mkazo wowote ndani ya Uislamu, Khomeini ameifanya ni wajibu (kusherehekea) kulingana na dini yake ya siri. Kumuongezea cheo Mtuhumiwa Mahdi zaidi ya Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) ni ukafiri ulio wazi.

 

 

Pale tu tutakapotambua kwamba Khomeini amejiteua mwenyewe Naibu kwa Imaam aliyetuhumiwa kwa mnasaba wa amri za sasa zilizotolewa kuitayarisha ardhi na taifa kwa kutokea kwake, tunaelewa kwamba lengo hasa la Khomeini kumuongezea cheo Mahdi wake ni kujipandisha cheo yeye mwenyewe. Kama Mahdi ni Mtukufu kuliko Rusuli wote, basi Naibu wake ni mbora kwa mnasaba wa utukufu wake, na kwa mnasaba wa sharifu wa usharifu wake. Hivyo, imekuwa ni (kazi) rahisi kwa Khomeini kuwafanya wafuasi wake wapofu kumuamini kuwa ni kiongozi, kuliongeza jina lake pamoja na jina la Allaah wakati wa wito wa Swalah “adhaana” misikitini huko Iran, kufanya (hilo jina) wito wa kutiana shime kwa watu (na kuanza) kupiga makelele, hata wakati wa Hijjah Masjid al-Haraam, msikiti mtukufu Makkah, kulia kwa maumivu: “Allaahu Akbar, Khomeini rahbar, labbayka ya Khomeini.” Maana yake “Allaah ni Mkubwa, Khomeini ndie Kiongozi, hapa tunaitikia kwako ewe Khomeini” Badala ya kutamka “Labbayka Allaahumma Labbayka.” Maana yake: “Tupo hapa, tumeitika wito wako, ee Allaah” kama Nabiy alivyotuamrisha tuseme wakati wa ibaadah ya Hijjah. Wafuasi hao hao wa Khomeini wanamuelezea kama ni “Ibraahiym wa miaka (hii)” na “Muusa wa wakati (huu).” Hivyo kwao wao ni sawa na Ibraahiym Khalilyu-Allaah (rafiki wa Allaah) na Muwsaa(‘Alayhis-salaam) ambaye Allaah Amezungumza naye!

 

 

Pale itakapoonekana wazi kwamba huyo Mahdi hakupatapo wala hatotokezea ndipo itakapobainika pia kwamba Khomeini ametunga huu uzushi ndani ya dini kwa nia tu ya kujifanya Bwana wa kutunga sheria na kiongozi wa asili ambaye shughuli zote ni zake yeye. Vinginevyo, ni nani mwengine anayeweza kuongoza watu kwa jina la Rasuli asiyedhihiri, na Mahdi mwenye kujificha ambaye kwao wao ni bora kuliko Rusuli wote? Hii khaswa ndio lengo la Khomeini analotafuta kufanikiwa kwa mujibu wa Katiba ambayo ameitunga na kuifafanua kwa lengo la kujiweka yeye kama ni kiongozi wa taifa ambapo hicho kifungu cha 5 kinasomeka: “Kipindi ambacho Imamu wa 12 yupo kwenye stara, ndani ya Jamhuri ya Kiislamu ya Irani, uongozi wa shughuli na uongozi wa watu ni jukumu la mwanachuoni mtiifu na mchaji Allaah.”

 

 

Hivyo, amefanya rahisi kwa wafuasi wake wapofu na watu wake kumkabidhi yote, kutunga sheria na kusimamia (legislative and executive powers), kumruhusu kuzuia namna anavyoona sawa bila ya kuangalia manufaa ya taifa. Ni kitu kisichowezekana kutokubaliana na Naibu wa Imamu asiye na uhakika wa (kudhihiri)!! Na tokea Khomeini alipokuwa Naibu wa Imamu asiye na uhakika ambaye ni Kiongozi wa Rusuli wote, kama anavyodai, kumpinga yeye ni kumpinga Allaah, na vivyo hivyo kumpinga yeye ni kufru na kurtadi!

 

 

Kwa namna hii Khomeini anawatisha wafuasi wake ilhali wapo kwenye dini yake, kwa sababu kumpinga Naibu wa Imamu asiye na uhakika ni kurtadi! Madai ya kutokuwa na hakika, kuhodhi haki ya kutunga sheria na kumiliki mamlaka yasiyo na mpaka ni sifa ya kufru, kwa sababu kufanya hivyo ameyaweka maneno yake Khomeini badala ya Kitabu cha Allaah na Sunnah ya Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam).

 

 

Inatambulika kwetu Ahlus-Sunnah Wal-Jama’ah kwamba sisi tunaongoza na kuongoza kwa mnasaba wa migogoro yetu kwa Allaah na Rasuli wake (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam). Allaah Mtukufu Anasema:

 

 فَإِن تَنَازَعْتُمْ فِي شَيْءٍ فَرُدُّوهُ إِلَى اللَّـهِ وَالرَّسُولِ إِن كُنتُمْ تُؤْمِنُونَ بِاللَّـهِ وَالْيَوْمِ الْآخِرِ ۚ ...﴿٥٩﴾

Mkizozana katika jambo basi lirudisheni kwa Allaah na Rasuli mkiwa mnamwamini Allaah na Siku ya Mwisho... [An-Nisaa: 59]

 

 

Pale Khomeini alipojiteua mwenyewe kuwa Naibu wa Imamu asiye na uhakika (!) imempasa yeye kujinasibisha kuwa ni mtungaji sheria, tatizo lolote litakalotokezea kwenye Baraza la Shuura, ndani ya Baraza la Mawaziri au ndani ya Idara yoyote, kwa mujibu wa Katiba ya Iran, ambayo tutaijadili hapo baadaye (In Shaa Allaah). Yote haya yanafanyika ili hayo makundi ya watu wapofu kuongozwa (kwa ajili ya) kumlinda yeye kwa kile wanachoita “njia ya Imaam” akili zilizomruka, kufanya hivi kwa huyu Kiongozi wa kizindiyq ambaye anatawala kwa moto na chuma, kuwachonganisha baadhi yao dhidi ya wengine, na kuanzisha ubadhirifu juu ya ardhi kwa kufuata nyayo za mababu zake (watu wa) Karmathi, (watu wa) Mongoli, (watu wa) 'Ubaydi na mfano wa hao Khomeini na wafuasi wake wamewashinda wote waliokuwepo kabla yao katika (mambo ya) uharibifu na uadui.

 

 Vi.  Dai La Khomeini Kwamba Wahyi Haukusimamishwa Kushushwa Baada Ya Kifo Cha Nabiy (Swalla Allaahu ‘Alayhi Wa Aalihi Wa Sallam)

 

Dai hili ni sababu mojawapo ya Wanazuoni wa Kiislamu kumtuhumu Khomeini kwa kufru na kurtadi. Anaeleza:

 

 

‘Faatwimah az-Zahraa aliishi siku 75 baada ya kifo cha baba yake, kipindi ambacho alikuwa mwenye huzuni na mpweke. Jibriyl alikuwa akimzuru na kumfariji, na kumueleza yeye kuhusu matokeo yote ambayo yatatokea hapo baadaye. Inaonesha kutokana na simulizi hii kwamba Jibriyl ndani ya kipindi cha siku hizo sabiini na tano alikuwa akimzuru mara kwa mara, na sifikirii kwamba simulizi kama hii inahusiana na yeyote zaidi ya Rusuli Watukufu. Imaam ‘Aliy alikuwa akiandika Wahy ambazo zilishushwa (kwa Faatwimah) kutoka kwa Jibriyl. Inawezekana hata mada ya Iran ilikuwa ni miongoni mwa wahyi zilizoteremshwa juu yake (!).

 

 

Hatuna uhakika kwa hilo, lakini (ni jambo) linalowezekana, kwa sababu Imaam ‘Aliy alikuwa ni ambaye akiandika huo wahy kama ambavyo alikuwa ni mwandishi kipindi cha Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam). Kushuka kwa Jibriyl (kwa ajili ya) kumuendea mtu si jambo rahisi au mada nyepesi, na wala siamini ya kwamba Jibriyl anashuka kwa mtu yoyote, ni lazima kuwepo ulinganifu (wa utukufu) baina ya roho ya yule anayeshukiwa na Jibriyl na Jibriyl mwenyewe, ambaye anatambulika kuwa na “roho bora takatifu”. Ulinganifu huu ulipatikana baina ya Jibriyl na Rusuli bora kama Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam), ‘Iysa, Muwsaa, Ibraahiym na mfano wa hao(‘Alayhimu-salaam). Jibriyl hakupatapo kushuka kwa wengine zaidi ya hawa. Sikupata kamwe kuona mapokezi yanayoeleza kushuka kwa Jibriyl juu ya Imamu. Hivyo, cheo hicho kitukufu hakuna aliyekipata baada ya kifo cha Rusuli zaidi ya Faatwimah. Hii ni mojawapo ya sifa ambazo Faatwimah ametofautishwa.

 

 

Tamko hili lina alama nyingi za ukafiri:

 

1-Kukaidi kwa Khomeini (amekataa) kwamba Utume na wahy ulisimama kuendelea baada ya kifo cha Rasuli wa Allaah, kama inayothibitishwa kwa maneno ya Allaah:

 

مَّا كَانَ مُحَمَّدٌ أَبَا أَحَدٍ مِّن رِّجَالِكُمْ وَلَـٰكِن رَّسُولَ اللَّـهِ وَخَاتَمَ النَّبِيِّينَ ۗ وَكَانَ اللَّـهُ بِكُلِّ شَيْءٍ عَلِيمًا ﴿٤٠﴾

Hakuwa Muhammad (صلى الله عليه وآله وسلمbaba wa yeyote miongoni mwa wanaume wenu, lakini ni Rasuli wa Allaah na ni mwisho wa Manabii. Na Allaah daima ni Mjuzi wa kila kitu. [Al-Ahzaab: 40]

 

 

na Hadiyth ya Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) :

“…na Amefunga mstari wa Utume kwangu mimi, hakuna Rasuli baada yangu.” [Hadithi sahihi].

 

 

Hamna makubaliano miongoni mwa Umma (Taifa la Waislam) kuhusiana na imani ya Khomeini aliyoipinga na kuichanganya kwa madai yake kwamba Jibriyl aliteremka juu ya Faatwimah, na kumshushia Qur-aan iliyo kamili ambayo vitabu vya Kishia, vinadai kuwa (Qur-aan hiyo yao) ni kubwa mara tatu zaidi kuliko Qur-aan yote.”

 

 

2-Kufru ya aina ya pili kwenye tamko lake ni kuhusiana na dai kwamba inawezekana wanawake kuwa ni Rusuli-Manabii na kupokea wahyi. Lakini Allaah Anasema:

 

وَمَا أَرْسَلْنَا مِن قَبْلِكَ إِلَّا رِجَالًا نُّوحِي إِلَيْهِم مِّنْ أَهْلِ الْقُرَىٰ ۗ 

109. Na Hatukutuma kabla yako (Rasuli) isipokuwa wanaume Tuliowafunulia Wahy katika watu wa miji. [Yuwsuf: 109]

 

 

Neno ‘wahyi’ liliotajwa kwa mnasaba wa mke wa ‘Imraan, Maryam na mama wa Muwsaa, ina maana ya “maongozi” (ya Allaah), kama Anavyosema:

 

وَأَوْحَىٰ رَبُّكَ إِلَى النَّحْلِ أَنِ اتَّخِذِي مِنَ الْجِبَالِ بُيُوتًا وَمِنَ الشَّجَرِ وَمِمَّا يَعْرِشُونَ﴿٦٨﴾

Na Rabb wako Akamtia ilhamu nyuki kwamba: Jitengenezee nyumba katika majabali, na katika miti, na katika wanavyojenga. [An-Nahl: 68]

 

 

kwa maana ya “Aliwaongoa nyuki.” Sio mama wa Muwsaa wala mke wa ‘Imraan waliowahi kuwa Manabii-Rusuli, lakini Khomeini amemfanya Faatwimah Rasuli au Nabiy aliyepokea wahyi kupitia kwa Jibriyl.

 

…/4

 

 

 

[1] Dondoo kutoka kwenye hotuba iliyotolewa na Khomeini Shaaban 15, mwaka 1400 H. iliyosababisha fatwa kutoka kwenye Ulimwengu wa Kiislamu kutolewa zikimtuhumu Khomeini kwa ukafiri.

 

 

 

 

 

Share