Khomeini Ndani Ya Darubini - 4: Shutuma Zake Za Ukafiri Kwa Abu Bakr Na 'Umar Na Maswahaba

 

Khomeini Ndani Ya Darubini – 4

 

Shutuma Zake Za Ukafiri Kwa

Abu Bakr Na ‘Umar bin Al-Khatwaab Na Swahaba

 

Imeandikwa na Wajiyh Al-Madini

 

Toleo la Pili

 

Alhidaaya.com

 

 

 

 

Kama walivyo Mazindiyq wengine (ndivyo alivyo Khomeini), ambao wanaegemeza uovu na chuki dhidi ya Uislamu na watu wake, ambao wanampiga vita Rasuli wa Allaah na Swahaba zake, na ambao wanajificha chini ya udhuru wa uongo wa mapenzi ya Ahlul Bayt, Khomeini anasema:

 

 

“Hatujadili kwa wakati huu, na Mashaykh wawili (Abu Bakr na 'Umar), na Mashaykh wawili wala jeuri walizotenda dhidi ya Qur-aan, wakaharibu (kwa fujo) pamoja na Swahaba wa Allaah wakatangaza vitu ruhusa na visivyoruhusiwa kwa makubaliano yao wenyewe wakatenda dhulma dhidi ya Faatwimah, binti halali wa Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na watoto wake (Faatwimah). Lakini tunataka kuonesha ujinga wao wa amri za Allaah na dini. Watu kama hao wajinga (na) wapuuzi, madhalimu na wakorofi hawakustahihi kuingia ofisi za Kiimamu, wala kuingizwa miongoni mwa watu wenye madaraka.”[1]

 

 

Muongo anazidi kueleza:

“Ni jambo linaloeleweka kwa yote yaliyotangulia kwamba uovu wa Mashaykh wawili dhidi ya Qur-aan haukuwa na muhimu kwa Waislamu. Hayo ni kwa sababu (Waislamu) ama walikuwa miongoni mwa Mashaykh wawili na kushirikiana nao au dhidi yao, lakini hawakujaribu kusema kitu kwa wale waliomtendea Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na binti yake namna walivyofanya. Hata kama mmoja wa wapinzani atahitaji kusema kitu, maneno yake yatapita bila ya kufanyiwa kazi hata kama mambo hayo yametajwa ndani ya Qur-aan. (Hao ni) Wale ambao hawakujizuilia njiani mwao, wala kujiuzulu kwenye ofisi zao.[2]

 

 

Khomeini khabithi anamueleza Al-Faaruwq ‘Umar, Allaah Awe Radhi naye dhidi ya adui zake, anasema:

 

 

“Matendo ya ‘Umar yametoa dalili ya kutoamini mafundisho ya imani yasiyopatikana na Qur-aan na uovu wa aya zilizotajwa kwenye Qur-aan.”[3]

 

 

Hakuna shaka yoyote kwamba madai haya ya Khomeini yanaonesha ukafiri na kurtadi, na kutoongoka kwa njia ya Waumini kwa sababu zilizo nyingi:

 

 

Kuwapiga vita Mashaykh wawili (Abu Bakr na ‘Umar), na kuwatuhumu wao kwa kutoamini na kurtadi, na kuwasingizia wao kwa uovu wa Qur-aan kwa makusudi na kwa ujinga, na kuwatuhumu kwao kwa ujinga na uhaini; kwanza, ni kuyatukana maneno ya Bwana wa Ulimwengu, Subhaanah, Ambaye Amewasifia wao, na kuwachagua kuwa ni Washirika wa Rasuli Wake, Mtakatifu wa viumbe vyote, na Akawatofautisha wao kwa muongozo (sahihi) wale ambao wamepigana mtindo mmoja bega kwa bega na Rasuli wake kwenye vita vyote. Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alioa binti zao, na amewaeleza vyema wao kuwa ni bora wa Swahaba wengine.

 

 

Amewabashiria kuingia kwao Peponi, na wamefurahia Ridhaa ya Allaah. Ummah wote wa Waislamu umethibitisha kwa wema isipokuwa waliortadi na wazushi ambao wamepinga makubaliano ya Ummah. Allaah Mtukufu Anasema:

 

إِلَّا تَنصُرُوهُ فَقَدْ نَصَرَهُ اللَّـهُ إِذْ أَخْرَجَهُ الَّذِينَ كَفَرُوا ثَانِيَ اثْنَيْنِ إِذْ هُمَا فِي الْغَارِ إِذْ يَقُولُ لِصَاحِبِهِ ﴿٤٠﴾

Msipomnusuru (Rasuli), basi Allaah Amekwishamnusuru, pale walipomtoa (Makkah) wale waliokufuru akiwa wa pili katika wawili; walipokuwa katika pango, [At-Tawbah:40]

 

 

Huu ni ushahidi kutoka kwa Allaah unaomkubali Abu Bakr Asw-Siddiyq, Allaah Awe Radhi naye, ambaye alikuwa na Nabiy pale wote wawili walipojificha kwenye pango walipokimbilia Madiynah, mazingira yaliyokuwa mazito kabisa na hakupatapo Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) kuyapata.

 

 

Kumpiga vita Abu Bakr kuna maana ya kurtadi maneno ya Allaah:

 

 

وَسَيُجَنَّبُهَا الْأَتْقَى ﴿١٧﴾الَّذِي يُؤْتِي مَالَهُ يَتَزَكَّىٰ ﴿١٨﴾وَمَا لِأَحَدٍ عِندَهُ مِن نِّعْمَةٍ تُجْزَىٰ ﴿١٩﴾

Na ataepushwa nao mwenye taqwa kabisa. 18. Ambaye anatoa mali yake kujitakasa. 19. Na hali hakuna mmoja yeyote aliyemfanyia fadhila yoyote hata amlipe. [Al-Layl: 17-19]

 

 

 

Wafasiri kwa pamoja wanakubaliana kwamba aya hizi zinamuelezea Abu Bakr Asw-Swiddiyq ambaye alikuwa akiwanunua watumwa kwa pesa zake na (kisha) kuwaachia huru, akitafuta Radhi za Allaah. Kumpiga vita inamaanisha kumpinga Allaah, Utukufu ni Wake Muweza, kwa maneno ya wazi, kwa sababu Yeye Amemchagua kuwa ni mtu wa mwanzo kuingia kwenye Uislamu, na makundi ya watu yakaongozwa (kuingia kwenye Uislamu) na yeye katika enzi za mwanzo za Uislamu. Allaah Amemchagua kuwa mshirika wa Nabiy Wake kipindi chote cha maisha yake, kabla na baada ya Utume. Alipofariki, mwili wake ulilazwa pembezoni mwa mwili wa Rasuli wa Allaah na ‘Umar, ya kwamba ushirika wao uendelezwe mpaka Siku ya Mwisho.

 

 

Kumpiga vita Asw-Swiddiyq kunalazimisha kumpinga Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) Aliyemchagua kuwa ni mshirika wake kipindi chote cha maisha yake. Pale Rasuli wa Allaah alipoulizwa. Ni nani miongoni mwa watu ni mpenzi wako? Akasema “Aaishah” Kisha akaulizwa Na katika wanaume? Akajibu “Baba yake” [Al-Bukhaariy na Muslim] Pia alisema: “Kama itanibidi nichukue miongoni mwa watu wa ardhini rafiki, nitamchukua Abu Bark, lakini undugu wa Uislamu na mapenzi yake ni bora.”

 

 

Inakubalika na wote kwamba yeyote anayempiga vita Asw-Swiddiyq amepingana na Allaah Mtukufu na Rasuli wa Allaah, aliyemuoa binti yake na kuishi naye kwa maisha yake yote yaliyobaki. Hivyo, kama Asw-Swiddiyq alikuwa mjinga, kama Khomeini (muongo mkuu na asiye na akili anavyodai), basi hili (shtaka) linaelekezwa kwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam), kwa sababu ameshindwa kuwafunza watu wake kipindi chote cha kushirikiana nao, na kama as-Swiddiyq alikuwa ni haini asiye muadilifu, kama waongo wanavyodai, basi (hao) ni Swahaba zake, Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) ndiye atakayepelekewa lawama.

 

 

Mmoja anaweza kumuuliza Khomeini na Mazindiyq wote kama yeye “Jee Rasuli wa Allaah alikuwa akimtambua Abu Bakr Asw-Swiddiyq kiimani au sio?” Kama jibu litakuwa ‘sio’ basi wamejitangaza wenyewe kuwa hawana Imani na ni Wartadi, kwasababu watakuwa wanamtuhumu kwa ujinga na hukumu mbaya kwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) kwa kushindwa kuzitambua sifa za mshirika wake wa maisha. Na kama watasema: ‘Ndiyo’, akimtambua kwamba Abu Bark alikuwa mjinga na dhalimu lakini alibaki kimya, badala yake akimsifu, akafanya ndoa na mtoto wake, akafariki ilhali kichwa chake kipo kwenye kifua chake (‘Aaishah), na akamteua kuongoza Swalah ya Jama’ah. Kama watakubaliana na yote haya basi wanajitangazia wenyewe kukosa Imani, kwa sababu haiyumkiniki kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akubaliane na uongo na makosa ya tabia, wala haimpasi kufanya hivyo. Lolote kati ya majibu hayo mawili yatakayotolewa, itaonesha ukosefu wa Imani.

 

 

Pia tunawauliza hawa wakaidi wa Imani sahihi: Alikuwa wapi Allaah Mtukufu pale kwa pamoja Asw-Swiddiyq na al-Faaruuq wakimuendea kinyume Rasuli Wake, kama munavyodai, wakiwa na nia ya kupata madaraka baada yake? Kwanini Allaah hakushusha aya za Qur-aan kuwafichua wao wakati Allaah Alipokuwa Akishusha maneno kwa mnasaba wa mambo ambayo si mazito kama uzito wao? Iweje Allaah Ashindwe kuleta habari za kuwafichua uovu wao kama kweli walikuwa waovu kama wanavyodaia Khomeini na Mashia wenzake wapotofu?

 

 

Wakati mmoja Allaah Aliteremsha aya zinazomfichua mnafiki ambaye alisaliti moja kati ya vita (vilivyopiganwa na Rasuli) na mwengine aliyemtukana Nabiy kwa neno. Wengine walifichuliwa kwa kujenga msikiti kama ni kitu kizuri kwa waumini na hali ulikuwa ni wa shari. Jee ni vipi iwezekane (wewe) Khomeini, Allaah hakuwafichua wale waliomfanyia hila Rasuli Wake kama mnavyoendelea kutuhumu, kuipinga Dini Yake, na kuunyanyasa ukoo wa Rasuli Wake? Kama mnasema ya kwamba Allaah Alikuwa Akijua yote haya lakini Hakuwafichua, bila shaka mtakuwa mnajikubalisha dhidi yenu wenyewe kwa kurtadi kwa kumpinga Allaah Asiye na kasoro kwa kutomtahadharisha Rasuli wake dhidi yao na hivyo kukubaliana na kosa na uongo. Yuko mbali na madai yenu. Na kama mtasema ya kwamba Allaah Hakushusha maneno kuwafichua wao, tutadai kwenu nyinyi kutuletea mbele yetu ushahidhi wenu. Tunaendelea zaidi kuwauliza kwanini Nabiy hakuweka wazi maneno hayo au angalau kuwapa hadhari Swahaba wake na Ummah wake dhidi ya Mashaykh wawili; Abu Bakr na ‘Umar? Na kwanini alificha ukweli kuhusu wao maishani kote?

 

 

Mtambue nyinyi waasi na wartadi, kwamba hamumpigi vita Abu Bakr na ‘Umar, bali Rasuli wa Allaah. Hakika mnampiga vita Allaah Mtukufu Ambaye Yupo juu ya mbingu zake saba, na kuupiga vita ukoo wa Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) ambao nyinyi mnadai walikuwa ni wasaidizi wa mipango. ‘Aliy alikuwa wapi pale Kitabu cha Allaah kikiharibiwa, na pale Swahaba walipochukua kwa nguvu? Kwanini akuzungumzia hilo? Kwanini yeye alikuwa ni msaidizi mkuu na mshauri wa Abu Bakr na ‘Umar? Na walikuwa wapi watu wake wengine wa Nabiy kipindi kilichotuhumiwa ni cha hatari?

 

 

Mnadai mara kwa mara kwamba Mashaykh wawili wamewapokonya urithi ‘Aliy na Faatwimah kutoka kwa mali ya Nabiy, kwamba Faatwimah alishtaki dhidi ya Asw-Swiddiyq kuhusiana na mada hii, na kwamba ‘Aliy na Al-‘Abbaas walijadiliana na Mashaykh (hao) wote, wakidai haki zao za urithi. Tunasema, hili lilitokea, lakini kiwango cha madai dhidi ya Mashaykh wawili, ya (kuwatuhumu) kubadilisha Dini ya Allaah, na kuchukua ukhalifa kwa nguvu, na vita vyenye (kuhitaji) kutiliwa mkazo kuliko mambo yapitayo ya kidunia (kwenye) suala la urithi. Jee ‘Aliy, Faatwimah na Al-‘Abbaas wanajali zaidi kuhusu kipande cha ardhi kuliko Dini ya Allaah na uongozi wa Ummah wa Kiislamu? Jee walishtaki kwa Mashaykh wawili kuhusiana na urithi na kukataa shitaka juu ya kubadili Dini ya Allaah na kubadilisha Kitabu Chake? Jee walificha hamasa zao pale ilipokuja kuhusu madai ya haki zao na kuikosa pindi walipodai haki za Allaah? Hili ni tusi kubwa mlilolitoa dhidi ya ukoo wa Nabiy. Walikuwa wapi maelfu ya Waislamu pale Dini ya Allaah ilipobadilishwa? Jee walikuwa hao Waislamu waliojitolea mali zao na maisha yao kwa ajili ya kutafuta radhi za Allaah wafedhuli wakubwa (kuliko) kusahihisha makosa? Ni wao ambao Allaah Amewasifia na kuwafanya taifa bora lililopata kutokea kwa wanaadamu. Bila ya shaka yoyote, mnadai kwamba wote walirudi kutoka kwenye Uislamu kwenda kwenye kufru isipokuwa watatu au watano kati yao.

 

 

Unageuka kutoka kwenye Uislamu kwenda kufru pale tu ulipotuhumu ujinga kwa Allaah, na kushutumu kwamba Yeye Amekubali dhulma na jeuri, kuwapatia bure wasioamini kucheza uharibifu na Dini Yake, Yuko mbali na yale munayomsingizia Kwake.

 

 

Allaah(Subhaanahu wa Ta'aalaa) Ameahidi kukilinda Kitabu Chake, Anasema:

 

إِنَّا نَحْنُ نَزَّلْنَا الذِّكْرَ وَإِنَّا لَهُ لَحَافِظُونَ ﴿٩﴾

Hakika Sisi Tumeteremsha Adh-Dhikra (Qur-aan) na hakika Sisi bila shaka ndio Wenye kuihifadhi. [Al-Hijr :9]

 

 

Lakini bila ya shaka yoyote wewe ni murtadi kwa kupinga kwamba Allaah Ametimiza ahadi Yake, kwamba Yeye Hakuleta kwa Rasuli Wake na taifa lake baada yake dini, Abu Bakr na Umar hakutoa mali iliyoachwa na Nabiy kwa warithi wake kwa ile sababu ya kwamba Nabiy (Swalla Alllahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alielekeza “Sisi Rusuli haturithiwi: Mali yetu tunayoiacha nyuma inagaiwa sadaka...”

 

 

ukawasifu watu waovu, kuwafanya marafiki. Mliingia kwenye kurtadi mlipodai kwamba Allaah Alichagua kwa Manabii wake wapenzi wanafiki, waongo na wasaliti. Mliingia kwenye ukafiri pale mlipomshutumu Rasuli wa Allaah (kutowapa) dharau kwa Mashaykh wawili. Hamkumuamini Allaah pale mliposhtaki kwamba Rasuli wa Allaah alitoa mabinti wa wanafiki na wasioamini, na mlipodai kwamba alikaa nao wote ‘Aaishah na Hafswah kama ni wake zake akielewa fika kuwa sio wenye kuamini. Ulirudi kwenye kutokuwa na imani pale ulipotoa uongo kwa Allaah, Mtakatifu ni Yeye Muweza, kwa kuusifu Ummah wa Muhammad kwenye Kitabu Chake:

 

 

مُّحَمَّدٌ رَّسُولُ اللَّـهِ ۚ وَالَّذِينَ مَعَهُ أَشِدَّاءُ عَلَى الْكُفَّارِ رُحَمَاءُ بَيْنَهُمْ ۖ تَرَاهُمْ رُكَّعًا سُجَّدًا يَبْتَغُونَ فَضْلًا مِّنَ اللَّـهِ وَرِضْوَانًا ۖ سِيمَاهُمْ فِي وُجُوهِهِم مِّنْ أَثَرِ السُّجُودِ ۚ ذَٰلِكَ مَثَلُهُمْ فِي التَّوْرَاةِ ۚ وَمَثَلُهُمْ فِي الْإِنجِيلِ كَزَرْعٍ أَخْرَجَ شَطْأَهُ فَآزَرَهُ فَاسْتَغْلَظَ فَاسْتَوَىٰ عَلَىٰ سُوقِهِ يُعْجِبُ الزُّرَّاعَ لِيَغِيظَ بِهِمُ الْكُفَّارَ ۗ وَعَدَ اللَّـهُ الَّذِينَ آمَنُوا وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ مِنْهُم مَّغْفِرَةً وَأَجْرًا عَظِيمًا﴿٢٩﴾

Muhammad (صلى الله عليه وآله وسلم) ni Rasuli wa Allaah. Na wale walio pamoja naye ni wakali zaidi dhidi ya makafiri; wanahurumiana baina yao. Utawaona wakirukuu na wakisujudu wakitafuta fadhila na radhi kutoka kwa Allaah. Alama zao dhahiri zi katika nyuso zao kutokana na athari za sujudu. Huo ni mfano wao katika Tawraat, na mfano wao katika Injiyl kama mmea umetoa chipukizi lake, likautia nguvu kisha likawa nene, kisha likasimama sawasawa juu ya shina lake, liwapendezeshe wakulima, ili liwatie ghaidhi makafiri. Allaah Amewaahidi wale walioamini na wakatenda mema miongoni mwao maghfirah na ujira adhimu. [Al-Fat-h: 29]

 

 

Utaniwia radhi, hakika hukurudi kwenye ukafiri, kwasababu (tokea mwanzo) hukuwa na imani wala hukupata kuingia kwenye Uislamu, wala hakupata kuamini Kitabu cha Allaah wala Rasuli Wake (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam). Madai yako si kitu ila unapiga chenga na kusema uongo na madai yako ya kuwa pamoja na ukoo wa Nabiy ni uongo, kwasababu wewe kwa kweli ni adui mkuu wa ukoo. Kila muongo mbaya mno na mwenye kwenda kombo, umedai kwamba alikuwa ni miongoni mwa watu wa Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam). Iwezekane hao wenye ndimi chafu kuwa ni watu bora na jamaa kwa ukoo wa Nabiy?

 

 

Tambua, kuwa Allaah Anakuelewa na Ameutawala ukoo wa Nabiy bila ya tuhuma zako mbovu, na mbali sana kutokana na uongo wako, na Anawalinda kutokana na njama zako.

 

 

Kwa ufupi, kwa kuwaendea kinyume Mashaykh wawili, Khomeini amemuendea sivyo Allaah, Rasuli Wake na Ukoo wake safi, na pia Ummah wake Mtukufu ambao Allaah Ameusifu, Akaegemeza mashahidi dhidi ya wa mwanzo na taifa la mwisho. Akisema:

 

وَكَذَٰلِكَ جَعَلْنَاكُمْ أُمَّةً وَسَطًا لِّتَكُونُوا شُهَدَاءَ عَلَى النَّاسِ وَيَكُونَ الرَّسُولُ عَلَيْكُمْ شَهِيدًا ۗ ﴿١٤٣﴾

Na ndivyo hivyo Tumekufanyeni ummah bora na adilifu ili muwe mashahidi juu ya watu na awe Rasuli shahidi juu yenu…. [Al-Baqarah: 143]

 

 

Sifa ni zake Allaah Ambaye Amebashiria kwa uzuri, wema na ubora wa Ummah wa Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam), kwa imani thabiti ya Abu Bakr Asw-Swiddiyq na ‘Umar Al-Faaruwq, na kwa kuwabashiria kwao Pepo. Laana za Allaah ziwe juu ya kila mkorofi na mchongezi mwenye chuki ambaye yupo dhidi ya Ummah mtukufu na muongofu.

 

 

 

…/5

 

 

 

[1] Khomeini, Kashf al-Asrar, pp. 107

 

[2] ibid, pp. 118

 

[3] ibid pp. 117

 

Share