Khomeini Ndani Ya Darubini - 6: Wilaayatul Faqiyh
Khomeini Ndani Ya Darubini – 6
‘Wilaayatul Faqiyh’
Imeandikwa na Wajiyh Al-Madini
Toleo la Pili
Viii - Ulezi 'Usimamizi' Wa Mwanachuoni ‘Wilaayatul Faqiyh’
Khomeini ametoa tuhuma nyengine aliyotunga kwenye fikra za Mashia: Ulezi wa Mwanachuoni, ambapo Katiba ya Iran imejikita huko. Hao Mashia (wenyewe) wamegawika kuhusiana na jambo hilo.
Uzushi huu unamaanisha nini, na kwanini ‘Ulamaa wa Kiislamu wakatangaza maamuzi rasmi ya kumtuhumu Khomeini kwa ukafiri kuhusiana na uzushi huu, kama walivyofanya hapo kabla kuhusiana na matamshi mengine yaliyotajwa hapo juu?
Sura hii inaeleza kwa ufupi uzushi huu, kuripulia mbali ukafiri na maazimio yao yaliyojificha, na pia unajadili athari zake kwa Dini ya Shia.
Ix – Neno La Muhtasari
Ushia unatokana na madhehebu ya kwamba hamna Serikali ndani ya Uislamu bila ya kuwepo Imamu. Imamu, kwa mujibu wa fikra zao za uongo, ni lazima ateuliwe kwa hukumu iliyo wazi. Wanadai kwamba Allaah Alimpa amri makusudi kumteua ‘Aliy (Allaah Awe radhi naye) kama ni mrithi wake. Lakini, wazushi (wanaendelea) kutetea (uzushi wao) kwamba, Swahaba walikataa Amri Yake kwa ukafiri wao, na kurithisha ukhalifa kwa Abu Bakr, na kwa ‘Umar baada yake, kisha kwa ‘Uthmaan (Allaah Awe Radhi nao wote), lakini walimkatalia ‘Aliy (Allaah Awe radhi naye) Ukhalifa huo. Mashia wanachanua uongo kwenda kuhusisha uteuzi wa Al-Husayn kutoka kwa ‘Aliy (Allaah Awe radhi naye), na uteuzi wa Al-Hasan.
Ni jambo gani linalotambulikana kwamba ar–Raafidhah (waliowakataa Makhalifa watatu; Abu Bakr, ‘Umar na ‘Uthmaan) wanagawika kwenye madhehebu tofauti. Kila mmoja wao anadai Uimamu upo kwa Imamu wao, lakini baadaye Uimamu ukaharibiwa kwa kifo cha al-Hasan al-Askari, ambae alikufa bila ya kuacha mtoto. Walipogundua kwamba uharibifu wa ghafla wa Uimamu utakuwa ni kikomo cha Dini yao ya uongo na kusababisha madhehebu kukatika kwa mapande, wakafanyiza hadithi ya kutunga za mtoto wa al-Hasan al-Askari (wanaomwita Mahdi) ambaye kwa mujibu wa hadithi zao, alikimbilia kujificha kwenye tundu (pango) huko Samirraa’, Iraq akiogopea kuuliwa na atatokea (tena) karibuni! Hao waliotunga kisa hichi walidhani kwamba watafadhaisha jambo hilo, ya kwamba kuna mtu atatokea baada ya miaka michache na kutambuliwa kuwa ni yeye! Walikwenda mbele hadi kudai kwamba yeyote anayemtaja Allaah katika idadi maalum hatafariki mpaka akutane na huyo Imamu wao Mahdi.
Ushia, kwa msingi wa itikadi zao, hakujaanzishwa Swalah ya pamoja ya Ijumaa wala Jihaad, (ati) wakisubiri kutokea tena kwa huyo Imamu wa 12 wa kutungwa aliyejificha. Lakini hao Rasfidhah (Mashia) walihisi kuwa (ni sawa) kuwapiga vita Swahaba wa Rasuli wa Allaah, na kulaani kila Muislamu muaminifu, na kuwaunga mkono Mazindiyq ambao wanampinga Allaah na Rasuli Wake, na huku wao Marafidha wakijificha kwenye kivuli cha Ahlul Bayt (watu wa nyumba ya Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) wakidai kuwa wao wanawapenda sana Ahlul Bayt na hali ukweli halisi wao ni waovu wakubwa.
Tokea wakati walipotunga uongo mbaya mno wa kupotea Imamu wao huyo waliomtunga (Mahdi), Mashia wameweza kipindi chote kuwa na uhusiano wa kukaza fundo (pamoja) na Mayahudi, Wakristo, Wamajusi na Wanafiki dhidi ya Ahlus-Sunnah Wal-Jama’ah. Mayahudi wamewateka kiakili na kuanzisha Ushia kupitia kwa Abdullah bin Sabaa Yahudi aliyeanzisha kipande cha mwanzo cha dini hii ya uongo. Mayahudi hao wa sasa, pamoja na ufadhili wanaofaidi kutoka Marekani, wameweza kuwa na nafasi ya kuanzisha utawala wao huko Palestina kwa amani, ili kuugawa Ulimwengu wa Waislamu, na kuanzisha badala yake (huko Palestina) imani yao ya Ushia ambao wafuasi wao wamekuwa ni wahisani wao katika kumbukumbu yote kwenye historia. Hivyo, wamechangia vilivyo kwa uanzilishi wa taifa la Kishia. Kwa mara ya mwanzo katika historia ya Ushia kuna kiongozi wa Kishia anayekataa Taqiyyah, ametangaza Jihaad na kusimamisha Swalah ya pamoja ya Ijumaa hata katika kipindi cha kutokuwepo kwa Imamu asiyeonekana! Naye ni Khomeini, aliyefanya hayo yote kwa kupitia sera yake ya ‘Ulezi Wa Mwanachuoni.’
X – Namna Ya Imani Ya Ulezi Wa Mwanachuoni ‘Wilayaatul Faqiyh’ Ulivyoingia Kwenye Mawazo Ya Mashia
Khomeini ameandika ndani ya Kitabu chake “Serikali ya Kiislamu” muda mfupi kabla ya kuzuka kwa Mapinduzi ya Iran. Ndani yake, anawauliza Mashia, “kwa muda gani mtasubiri kabla ya kutokea kwa Imamu asiyekuwepo? Ni lazima tuanze kufanya kazi kuanzia sasa mpaka atakapotokea, kuiweka tayari ardhi kwa ajili yake, ili hapo atakapotokea atakuta mambo yapo sawa na tayari Serikali imeshaanzishwa!”
Ameshauri namna nyengine ya kutumia khums au asilimia ishirini ya pato la mwaka kwa kila Shia kulipwa kwenye al-abeit, akisema “Bani Haashim ambao wanawajibika kupata asilimia tano, wanatosha kupata asilimia kumi ya kila kumi ya thamani hii. Wanazifanyia nini mirundi ya mamilioni kama hii? Tunaweza kuanzisha Jihaad sasa hivi, na kutumia utajiri huu kuanzisha Taifa la Kiislamu!”
Mashia wenyewe walivutiwa na mawazo ya Khomeini, na kupata ndani yake utulivu kutokana na unyanyasaji, dhulma na kufuata kwa maficho dini yao katika kipindi chote cha historia. Wengi wa walioguswa na fikra zake ni vijana wa Kishia na vyama vya upinzani vya Iran mnamo kipindi cha utawala wa kibabe na ubaguzi wa Shah. Hivyo, Khomeini akaongoza nguvu za makundi ya watu pamoja naye. Lakini wakuu wake Khomeini, viongozi wa dini yao, walipinga muelekeo huu mpya na kuuona kama ni kuondoka kwa Ushia kwenda kwenye ukafiri. Dini yao inatangaza sifa ya kwamba hamna Swalah ya pamoja ya Ijumaa itakayoongozwa wala Jihaad kutangazwa bila ya kuwepo Imamu wa uhakika. Hakika Ushia kwa undani wake unaegemezwa kwenye madhehebu ya Uimamu, ni mtu mmoja pekee tu mwenye uhakika anahusika kwa Uimamu, kuwatawala watu kwenye vita na amani, na kuongoza Swalah zao. Namna gani mtu mwengine achukue nafasi yake?
Viongozi wa Kishia walitoa mawazo kwamba hakuna mtu anayeweza kuchukua nafasi ya Imamu wa hakika. Lakini Khomeini alisuluhisha tatizo hilo kwa kubuni cheo cha unaibu wa Imamu wa hakika asiyekuwepo, kujitambulisha kama ni Mwanachuoni ambaye anapambanisha desturi za haki na fiqhi ambazo Mashia ni lazima wazikubali.
Fikra za kutokubaliana na Serikali iliyokuwepo madarakani ya Shah juu ya madhehebu mepya yalitawala miongoni mwa Mashia, lakini yalimurikwa zaidi kutokana na kukubalika sana ambapo Mapinduzi ya Khomeini yalipata kutoka kwa vyama vyote ambao walimpinga Shah na utawala wake, waliungana na Wazayonisti wa Kimarekani na propaganda za Kiyahudi zilizomchora Khomeini kama ni mshindi mzuri. Matokeo yake, vijana wa Kiislamu walitekwa na mng’aro wa Mapinduzi haya. Bila ya hila yoyote, wakafikiri kwamba mtu huyu ni muokovu atakayeutoa kwa ajili yao utawala wa kibabe na ukoloni. Namna zilivyopangwa vizuri propaganda na kuvishwa hayo Mapinduzi ndivyo zilivyoteka akili za Waislamu, hadi kufikia hali ya kutokuwa na wasiwasi wa kuuliza “Ni nini hayo madhehebu ya ‘ulezi wa mwanachuoni’ (ambayo iliyohifadhiwa ndani ya Katiba ya Iran) inamaanisha nini?” Au, “Hayo Mapinduzi ya Iran ya ki-Rafidha (ki-Shia) yanamaanisha nini?”
Kiasili, hakuna mtu aliyesikia sauti ya Mashia ambao walipinga hilo dhehebu la ukafiri, wala tahadhari za wale waliokamata elimu miongoni mwa Ahl-al-Sunnah dhidi ya uvumbuzi huu kuiweka wazi hatari hii na athari zake sio tu kwa Uislamu, bali hata kwa dunia kwa pamoja.
Xi – ‘ulezi Wa Mwanachuoni – ‘Wilaayatul Faqiyh’ Nini Maana Yake?
Madhehebu haya, yaliyoanzishwa na Khomeini, yanaeleza kwamba kipindi ambacho hayupo Imamu wa hakika, kwa mujibu wa imani zao za uongo za Kishia, ulezi na uongozi kwa taifa ni wajibu wa mwanachuoni muaminifu na mchaji Allaah. Kwa mujibu wa Kifungu cha 5 cha Katiba (kilichoelezwa huko nyuma). Kifungu cha 57 kinasomeka kama ifuatavyo:
“Mamlaka ya utawala ndani ya Jamhuri ya Iran, yaani mamlaka ya bunge, uongozi na Mahkama wanalazimika kutekeleza wajibu wao chini ya ulezi wa Imamu”
Na Kifungu 107 kinasomeka:
“Kama idadi kubwa ya watu wanajua na kukubaliana juu ya mwanachuoni anayefaa kuwa na sifa za uongozi kama zilivyoelezwa ndani ya Kifungu cha 5 cha Katiba hii kama zilivyojumuishwa ndani ya mamlaka kuu za dini, kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu, Ayatollah Al-Udhma Imamu Khomeini, vivyo kwamba mwanachuoni huyo atamiliki ulezi na pia majukumu yaliyotokana na vyeo viwili. Vinginevyo wataalamu waliochaguliwa na watu watajadili miongoni mwao nani ambaye mwanachuoni anayefaa na mwenye sifa ya kiongozi muadilifu na anatambulikana kama ni kiongozi wa watu. Vinginevyo ni lazima wateue wanachuoni wawili au watano wenye sifa sawa na wanachama na ‘baraza la uongozi’, na kutambulishwa wao kwa watu”.
Kwa mujibu wa Kifungu 110 cha Katiba, majukumu ya kiongozi au naibu wa Imamu wa hakika, yanaorodheshwa kama ifuatavyo:-
- Kuteua wanachuoni kwenye baraza la kulinda Katiba;
- Kuteua mamlaka kuu ya Mahkama, nchini Iran;
- Kuwapa amri vikosi vya jeshi, pamoja na kujumuisha: uteuzi au kuachishwa kazi kwa Kamanda Mkuu (commander-in-chief), na uteuzi na kuachishwa kazi kwa Kamanda (general commander) wa (kikosi cha) Walinzi wa Mapinduzi ya Iran;
- Kuanzisha Baraza la Ulinzi la Taifa, ambalo linahusisha raia wa Jamhuri, Waziri Mkuu, Waziri wa ulinzi, Kamanda Mkuu, Kamanda wa (kikosi cha) Walinzi wa Mapinduzi ya Iran, washauri wawili watakaoteuliwa na kiongozi;
- Kuteua makamanda watatu wa jeshi, kwa kushauriana na Baraza Kuu la Ulinzi wa Taifa;
- Kutangaza vita au amani, na kuhamasisha kwa ajili ya vita kwa mashauriano kutoka kwa Baraza hilo juu;
- Kutia saini matokeo ya uchaguzi wa raisi baada ya uchaguzi uliofanywa na watu, washindani wa uchaguzi wa raisi ni lazima wathibitishwe na Baraza, kama ni walezi wa Katiba kwa kuanza tu kwa uchaguzi.
- Kumuondoa Rais kama ikiwa ni kwa manufaa ya taifa, baada ya uamuzi wa Baraza Kuu ulioegemezwa katika kutotekeleza majukumu ya Katiba na baada ya kukubaliwa kutoka Baraza la Taifa la Shuura kuthibitisha kushindwa Rais kisiasa.
- Kutoa usamehevu au adhabu hafifu ndani ya mzunguko wa taratibu za Kiislamu, baada ya mashauriano kutoka Mahkama ya juu.
Kwa kusoma kwa uangalifu vifungu vya Katiba ya Iran, na ‘ulezi wa mwanachuoni’ kwa pamoja, kunaonesha ukweli ufuatao:-
1) Muelekeo huu unakwenda kinyume na madhehebu yalioegemezwa kwenye Ushia ya ‘hamna serikali bila ya Imamu wa hakika’. Kwa maana hiyo, Mashia hawatambui mamlaka ya Serikali ya Ahlus-Sunnah ambao wanaamini kwamba jukumu la kuongoza Ummah wa Waislamu linamilikiwa na Khalifah, ambaye anateuliwa na kukubaliwa na Ummah. Na Khalifa au Swahaba, kwa mujibu wa watu wakweli, Ahlus-Sunnal Wal-Jama’ah ni Imamu ambaye ‘Ijtihaad’ yake inaweza kuwa sahihi au sio sahihi, na ambaye anawauliza (na kuwashauri) watu wenye elimu (na ujuzi), na kama watahitalifiana juu ya suala lolote, basi mpatanishi wa mwisho ni Kitabu cha Allaah na Sunnah ya Rasuli Wake kama inavyoamrishwa na Allaah:
يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا أَطِيعُوا اللَّـهَ وَأَطِيعُوا الرَّسُولَ وَأُولِي الْأَمْرِ مِنكُمْ ۖ فَإِن تَنَازَعْتُمْ فِي شَيْءٍ فَرُدُّوهُ إِلَى اللَّـهِ وَالرَّسُولِ إِن كُنتُمْ تُؤْمِنُونَ بِاللَّـهِ وَالْيَوْمِ الْآخِرِ ۚ ذَٰلِكَ خَيْرٌ وَأَحْسَنُ تَأْوِيلًا ﴿٥٩﴾
Enyi walioamini! Mtiini Allaah na mtiini Rasuli na wenye madaraka katika nyinyi. Mkizozana katika jambo basi lirudisheni kwa Allaah na Rasuli mkiwa mnamwamini Allaah na Siku ya Mwisho. Hivyo ni bora na matokeo mazuri zaidi. [An-Nisaa:59]
Hata hivyo, Marafidha wanatangaza kwamba hamna mamlaka ya Serkali bila ya Imamu wa hakika, na kwamba hakuna nafasi ya Ijtihaad, makosa au usahaulifu kwenye kutawala taifa! Ilikuwa hivyo hivyo mpaka Khomeini ambaye bila shaka si ‘ma’asuum’ (aliyelindwa na makosa), alipoibuka na madhehebu ya ulezi wa mwanachuoni, ambayo haipatani (kabisa) na asili kuu ya Marafidha. Hivyo, kulifungua fundo la mwanzo la Ushia.
2) Katiba ya Iran inampa Khomeini (anayedai kuwa na uadilifu, elimu ya fiqhi, na utambuzi wa miaka ya leo) ulazima wa kusalimisha amri zote kwenye mikono yake. Hivyo, mwanachuoni huyo, naibu wa Imamu, amekuwa ni mtunga sheria na kiongozi aliyejiteua mwenyewe, pamoja na mamlaka yasiyo na upinzani juu ya sehemu zote za maisha ya watu wa Iran. Bila shaka yoyote ametumia mabavu yake alipomtoa Rais mteule, Bani Sadr, kutoka ofisini kama kwamba ni mwajiriwa wa chini. Pia amejipa nguvu juu ya daraja zote za Serikali, pia haki ya kuitolea maana, dini na Ijtihaad isiyo na pingamizi.
3) Ni jambo linaloeleweka kwamba Katiba ya Iran imemwekeza Khomeini pamoja na mamlaka yote, haya yamefanywa kwa mnasaba wa madhehehu ya ‘ulezi wa mwanachuoni’, halkadhalika kama ni naibu wa Imamu asiyekuwepo. Pia inaeleweka kwamba Imamu asiyeonekana ni wa hakika kwa mujibu wa dini ya Marafidha, na kwamba usahaulifu, mitelezo au makosa hayapo kwake yeye. Bila ya utata wowote, mamlaka yote kiasili yaliyokuwepo kwa Imamu anayetuhumiwa kuwa hayupo yamesafishwa kiaina yake kwa naibu wake. Athari yake, pingamizi yoyote itakayoelekezwa dhidi ya naibu wake ni, kwa asili yake ni kumkaidi dhidi ya Mnaibu!! Kwa sababu hiyo kila mtu aliyempinga Khomeini alikaribishwa kwenye kutezwa nguvu, kutengwa, kifungo au kifo, bila ya kujali udini, au hadhi ya elimu waliyopata karibuni hao wasio na makosa.
Kwenye Kitabu chake kilichota sauti “Mapinduzi Yenye Mashaka” (Miserable Revolution) Dr. Musa al-Musawi anasema:
“Ulimwengu wote, Waislamu na wasio Waislamu ni lazima wajue kwamba wanachuoni wakuu wa Iran, na Masharifu wa mamlaka ya dini kwa nguvu zote wamepinga madhehebu ya ‘ulezi wa mwanachuoni’ na kutangaza kwamba hakuna mnasaba wowote na dini, na kwamba, ni uvumbuzi na ukafiri. Kiongozi mkuu mtukufu Shariatmadari, ambaye alichangia sana hapo awali kwa Mapinduzi, bado kidogo alipe thamani ya maisha yake kwa kupinga madhehebu haya. Na alipozidi ukereketwa wa upinzani wake, Khomeini akawapeleka nyumbani kwake watu elfu kumi wenye mapanga kwa ajili ya kumuua yeye na wafuasi wake, wakipiga mayowe kwa sauti moja na wakielekeza nyumbani kwake maneno yafuatayo: “tundu la udadisi; ni lazima livunjwe na kuchomwa moto.” Walinzi wa Imamu Shariatmadari walipigana sana dhidi ya uvamizi wa kishenzi uliotangazwa na Imamu aliyeibuka juu kwa thamani ya roho mbili.”
4) Pale Khomeini alipojipatia bila haki nafasi ya unaibu wa Imamu anayedhaniwa (ambaye anajidai kuwa ni bora kuliko Maimamu, Rusuli na Manabii), alijipa haraka nafasi ya Uimamu!
Akizungumza kuhusu Imamu asiyekuwepo, Khomeini anasema:
“Siwezi kumuita (kama ni) kiongozi kwa sababu ni mtukufu zaidi ya hivyo, bali hata siwezi kumuita binaadamu wa mwanzo kwa sababu hakuna wa kumzidi yeye, hivyo naweza kumueleza yeye kwa maneno ya “Muahidiwa (na) mtarajiwa Mahdi” ambaye Allaah Subhanah Amemuhifadhi kwa ajili ya binaadamu. Hivyo, tuna ulazima wa kujiandaa kumuangalia. Kama tutafanikiwa, tutakuwa na uwezo wa kuinua vichwa vyetu kwa fakhari juu ya Serikali (na) idara zetu zote. Tunategemea kwamba nchi nyengine zinajitayarisha kwa kutokea Mahdi, amani iwe juu yake, na kuwa tayari kwa ziara yake.”
Pia Khomeini ameongeza katika risala yake:
“Al-Imam al-Mahdi, ambaye Allaah Amemtenga kama ni hazina kwa binaadamu, ataihudumia haki duniani kote, na kufanikiwa ambapo Mtume aliyekuja kabla yake amefeli (!!).”
Hivyo, Khomeini amemweka Mahdi wake asiyeonekana (ambaye hakupatapo wala hatapatapo tokea) juu ya Rusuli wote. Na kiasili, kwa vile ni naibu wa Imamu anayedhaniwa, pia ni mbora kuliko Rusuli wote. Kwa sababu hii, wafuasi wa Khomeini, wanamuelezea kama ni “Ibraahiym wa leo” na “Muusa wa miaka hii.”
Katika Kitabu chake: “Bwana Mkubwa Khomeini Juu Ya Mezani.” (Master Khomeini on the Scales) Dr. Musa al-Musawi anaeleza, “Khomeini, anajitukuza na kujipandisha hadhi mpaka kwenye nafasi ya kujiteua Fajr Hijazi kama ni mwakilishi wa Iran kwenye Baraza la Watu na Kiongozi wa Taasisi ya Wanaonyanyaswa, gauni (hili ni) kubwa mno la mali nchini.”
Kwa kujipa madaraka yasiyo na upinzani, kama ni naibu wa Imamu, amepata cheo cha “kiongozi” na kukifanya kuwa wito wa makundi kuita “Allaahu Akbar, Khomeini rahbar” Lakini kwa ajili ya kuendeleza matashi yake ya uchu wa madaraka, akaengeza sentensi nyengine kwenye adhana (wito wa kuswali) akiliweka jina lake kabla ya Mtume, kama ifuatavyo:
“Allaahu Akbar, Allaahu Akbar, Khomeini rahbar (kiongozi), Ash-hadu Anna Muhammadn Rasoolullah….”
5) Mtu anaweza kutambua namna taifa linavyoonekana pale mali ghafi, bunge, serikali na watu wanatawaliwa na mzulufu wa miaka yake ya themanini. Kwa neno moja kutoka kinywani mwake anaweza kupitisha sheria, kuteua au kumtoa ofisini yeyote anayependa, kubadilisha dini, au kuua au kutesa yeyote anayependa. Fikiria namna mtu kama huyu anavyoweza kuiburuza nchi kwenye maangamizi, bila ya kuona uchungu! Kama ni mtu anayemuogopa Allaah ilikuwa awe makini sana kwenye mikono yake na utawala, atazalisha msiba mkuu. Vipande vingapi zaidi vivunjwe wakati wa uongozi wa Khomeini?
Dr. Musawi anaelezea: “Khomeini ni najisi na mwenye majisifu hadi kufikia kwamba hajali hata kama dunia nzima itabomolewa kwa mwisho wake yeye; haoni yeyote kuliko yeye mwenyewe. Hii ni tabia mbaya mno aliyokuwa nayo kiongozi wa kidikteta na zaidi kama huyo kiongozi ameekezwa pamoja na nguvu za mwanachuoni mkuu.”
Dr. Musawi anaendelea kuelezea: “Sifa kubwa mno yake ya Kishia ni uhasidi uliojificha anayoibeba dhidi ya mtu yeyote aliyemfanyia ubaya awali, hata iwe karne nyuma. Hasahau makosa ya jinai. Hasahau wala kutoa usamehevu kwa jinai, na analipiza kisasi nafasi ya mwanzo aipatayo. Kumwaga damu na mauaji ya watu hayamshughulishi, wala hafadhaiki kwa kusema uongo hadharani au sehemu za siri.”
“Pindi madaraka yalipokuja mikononi mwake.” Dr. Musawi ameelezea:
“Ametenda makosa ya jinai yanayoweza kufanya ngozi kutambaa. Anachukua rushwa kwa jina la Uislamu, Khomeini ni kovu itakayobakia daima katika historia. Mtawa[1] huyu wa Kitaghuti, mwanachuoni mpumbavu, dikteta muovu na muuaji mkongwe anawazuilia mama watoto wao, na kuwafanya watoto mayatima. Ameua kwa kadiri alivyoweza watoto wa kiume wa watu wa Iran kwa miaka minne kama ambavyo aliua aliye nyuma yake kwa miaka thelathini. Huyu hakika ni mmoja wa laghai (dhalimu) na mnafiki (mkubwa) katika historia”
Dr. Musawi ameongeza:
“Hivyo, wanyonge wa Iran wanalazimika (kujisalimisha) kwa kiu ya mauaji ya mwendawazimu aliyejigeuza katika vazi la mwanachuoni.”
Kama hayo juu ni miongoni mwa tabia za Khomeini, je ni uadui gani unaathiri fikra zake za uongozi usiokuwa na upinzani madarakani?
Tunasoma na kusikia kuhusu mabomoaji na mauaji kila siku. Ameua watu 100, 000 katika kipindi cha miaka ya giza ya uongozi wake. Historia ya sasa haijaonekana tokea Stalin alipojulikana kuwa ni zaidi ya kiongozi mpumbavu kuliko kiumbe huyu. Hata hivyo, hatushangazwi kusikia jinai kama hizo kutendwa na taghuti mwengine kama Stalin, lakini tunashagaa pale taghuti mwenye wazimu kama Khomeini akitenda makosa ya jinai kwa jina la Uislamu na Qur-aan, akisambaza uaduai wake kwenye Ulimwengu wa Waislamu. Hata msikiti mtukufu, Al-Masjid al-Haram huko Makkah, haukupata nafuu kwa uovu wake walipokwenda watu wake kufanya fujo kwenye Hija na kuchoma magari. Kuna uovu zaidi ya ‘ulezi wa mwanachuoni’ muongofu na mchaji Allaah anayezielewa zama za leo?!
6) Kipengele cha ukafiri cha kifungu chenye mnasaba wa ‘ulezi wa mwanachuoni’ zilizotungwa ndani ya Katiba ya Iran, ni kwamba vimemfanyia mwanachuoni huyu (ambaye mikononi mwake kuna nguvu zote), mpatanishi wa mwisho kwa kila mgogoro na kumpa yeye neno la mwisho kwenye dini. Hii inakwenda kinyume na chanzo cha uongozi ndani ya Uislamu. Ni Allaah pekee tu, na kwamba mgogoro wowote baina ya mtawala na mtawaliwa ni lazima urejeshwe kwenye Kitabu cha Allaah na Sunnah za Rasuli Wake kama ilivyoamrishwa na Allaah:
يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا أَطِيعُوا اللَّـهَ وَأَطِيعُوا الرَّسُولَ وَأُولِي الْأَمْرِ مِنكُمْ ۖ فَإِن تَنَازَعْتُمْ فِي شَيْءٍ فَرُدُّوهُ إِلَى اللَّـهِ وَالرَّسُولِ إِن كُنتُمْ تُؤْمِنُونَ بِاللَّـهِ وَالْيَوْمِ الْآخِرِ ۚ ذَٰلِكَ خَيْرٌ وَأَحْسَنُ تَأْوِيلًا ﴿٥٩﴾
Enyi walioamini! Mtiini Allaah na mtiini Rasuli na wenye madaraka katika nyinyi. Mkizozana katika jambo basi lirudisheni kwa Allaah na Rasuli mkiwa mnamwamini Allaah na Siku ya Mwisho. Hivyo ni bora na matokeo mazuri zaidi. [An-Nisaa:59]
Lakini, Katiba ya Iran inaeleza kwamba, migogoro yote ni lazima irejeshwe kwa mwanachuoni muongofu, naibu wa Imamu wa hakika asiyekuwepo, Khomeini. Hivyo, anajiweka nafasi ya Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) kwa kuwa ni chanzo cha madaraka na ni yeye pekee anayeusimamia.
Kwa vile Imamu, kwa mujibu wa Mashia, ni chanzo cha madaraka na bunge, mwenye haki ya kuitolea maana Quran na ni ambaye anaosimamia uongozi. Khomeini, kwa mnasaba wa nafasi kama hiyo ya Imamu na naibu wa Imamu anayedhaniwa, anamiliki mamlaka yote yakiwemo kuteua na kuwaachisha kazi kila kiongozi na mamlaka yoyote nchini kwa mujibu wa Kifungu cha 110, kinachoelezea uhalali wa uongozi.
Xii – Hitimisho
Hivyo, uzushi wa Khomeini, ‘Ulezi wa mwanachuoni’ pamoja na hadithi za Imamu asiyekuwepo (ambaye, hata kama angekuwepo angelikuwa au asingelikuwa na sauti mbele ya huyo anayemwakilisha yeye) zina sifa za uwazi za ukafiri wa hali ya juu.
Vyovyote ukafiri utakavyokuwa, uzushi huu umewaamsha Mashia wengi kutoka kwenye usingizi mnono, kutambuwa uongo wa mawazo wa darasa hili, na uongo muovu mno, madhehebu ya ‘ulezi wa mwanachuoni’. Kwa sababu wao ni wa mwanzo wa kuumia na athari zake. Imewafanya hao wenye kuamini kwenye Uimamu usio na upinzani wa Khomeini na mwenye kuwakilishwa kwa Imamu wa hakika kupata kukabidhiwa watu wa Iran. Mashia wanaompinga Khomeini wanapata adhabu iumizayo.
Kwa kushangaa, Khomeini na wale wanaokubali kuingia kwenye mtego ulio wa kisirani, wanabeba maumivu hadi kusafisha nje madhehebu dunia nzima, na wanadiriki kuimarisha kwenye Ulimwengu wa Waislamu, wakiwaalika Waislamu kuiabudu dini yao ya kisirani na kumkubali kwa kiapo Khomeini kama ni Imamu wa Ummah wote wa Uislamu (!) na pia kama ni naibu wa Imamu wa hadithi! Huyu bila ya shaka ni kama shetani mbaya mwenye kiburi aliye fedhuli na jeuri.
Pia inastaajabisha kuona miongoni mwa Ahlus-Sunnah wale ambao wajinga wa kuona na kuwa wenye busara na utambuzi wakimkubali na kuhubiria fikra zake bila ya kutambua madhehebu, utendaji au upande wa utekelezaji sheria kwa Mahkama kwenye uvumbuzi ulio wa kisirani wa ‘Wilayat al-faqiyh’ au ulezi wa mwanachuoni.