Itikadi Za Ushia Kutoka Katika Vitabu Vyao: 1 Itikadi Yao Juu Ya Allaah Manabii, Shahaada Yao
Itikadi Za Ushia Kutoka Katika Vitabu Vyao: 1
Itikadi Yao Juu Ya Allaah Manabii, Shahaada Yao
1. Hatutamkubali Allaah huyu wala Mtume wake huyo ambaye Khalifa wake ni Abu Bakr [Anwaarun-Nu’maniyyah, Mjadala 2, uk. 278 - Kilichochapishwa Iran].
2. Mitume wote (‘Alayhimus Salaam) hawapewi utume mpaka wakubali kuamini kwa makosa vitendo vya Allah [Uswuul al-Kaafi, Mjadala 1, uk. 265 - Kilichochapishwa Iran].
3. Wamesema hawachukuwi jukumu ya kwamba kuamini Qadar na kubarikiwa kunatokamana na Allaah [Uswuul al-Kaafi, Mjalada 1, uk. 293 - Kilichochapishwa Iran].
4. Ma-Imamu kumi na nne ambao wamelindwa na makosa [Ma’asumiyn] hao hawana cha kuwafananisha nacho katika kufanya makosa yaliotanguliya ama hawakukosa kabisa, wao ni kama Allaah. [Chouda Sitaray, uk. 2 - Kilochapishwa Pakistan].
5. Hakuna tofauti baina Allaah na ‘Aliy Katika sifa mfano, za Ubwana wa Pete ya Sulaymaan, Ubwana wa siku ya Qiyaamah, Ubwana katika Swiraat [Kivuko cha juu ya moto wa jahannam], Ubwana katika Uwanja, Ubwana wa kuumba majani katika miti, Ubwana wa utundaji matunda, Ubwana wa uteremshaji mvua, Ubwana wa usukumaji wa maji katika mito. [Jila-ul-‘Uyuun, Mjalada 2, uk. 85 - Kilochapishwa Pakistan].
6. Kwamba Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) na wajukuu wake wako kila mahala na wanajua kila kitu, Na hili ni umbile lao lililo madhubuti na halitokamani na Allaah. [Jila-ul-‘Uyuun, Mjalada 2, uk. 85 - Kilochapishwa Pakistan].
7. Allaah Anapozungumzia baraka Anazungumza kwa lugha ya kifursi na Anapozungumziya adhabu huzungumza kwa lugha ya kiarabu. [Taariykh-al-Islaam, uk. 163 - Kilochapishwa Lahore].
8. Itikadi ya shia wanapotamka shahada ni “La Illaaha ila Allaah, Muhammadur-Rasuulu-Allaah, ‘Aliy Waliyu-Allaah, Wasiyur-Rasuulil-Allaah, Wa Khaliyfatuh bila Fasl.” [Tuhfa Namaaz Ja’afariyyah, uk. 10 - Kilochapishwa Pakistan].
9. Mahala popote ndani ya Qur-aan panapotajwa neno “Rabb”, Maana yake ni “’Aliy” [Jila-ul-‘Uyuun, Mjalada 2, uk. 66 - Kilichochapishwa Pakistan].
10. Qur-aan haitoonekana (haitopatikana) kwa usahihi wake mpaka atakapokuja Imamu Mahdi (Imamu wa 12 wa Shia). [Anwaarun-Nu’maaniyyah, Mjalada 2, uk. 360 - Kilichochapishwa Iran].