Mambo Kumi Tunayoyapoteza

 

Mambo Kumi Tunayoyapoteza

 

Imekusanywa na Ummu ‘Abdillaah

 

Kutoka Katika Mafundisho Ya Imaam Ibnul Qayyim (Rahimahu Allaah)

 

Alhidaaya.com

 

 

 

1. Elimu Yetu:

 

Kuipoteza bila ya kuifanyia kazi.

 

 

 

2. Matendo Yetu:

 

Kuyapoteza kwa kutokuwa na Ikhlaasw.

 

 

 

3. Mali Zetu:

 

Kupoteza kwa kutumia kwa vitu ambavyo havitatuletea Ujira mbele ya Allaah (Subhaanahu wa Ta‘ala). Tunapoteza Pesa zetu, vyeo vyetu, mamlaka yetu, kwa vitu ambavyo havina faida katika haya Maisha ya dunia au katika Akhera.

 

 

 

4. Mioyo Yetu:

 

 

Imepotea kwa sababu ipo tupu na mapenzi ya Allaah, na hisia zipo mbali kwenda kwake, na hisia za Iymaan na kuridhika. Hapo ilipo, Mioyo yetu imejaa kitu au mtu fulani.

 

 

 

 

5. Miili Yetu:

 

Tunaipoteza kwa sababu hatuitumii kwa Ibadaah na kumuabudu Allaah na kumtumikia.

 

 

 

6. Mapenzi Yetu:

 

Hisia za mapenzi yetu zimepinduka mielekeo yake, haimwelekei Allaah, bali inaelekea kwenye vitu vingine au watu wengine.

 

 

 

 

7. Muda Wetu:

 

Tunapoteza, hatuitumii ipasavyo, kufidia kwa kilicho pita, kwa kufanya ambacho kinastahiki kufanya muda huu katika mambo mema ili kufidia yale mabaya yaliyopita.

 

 

 

8. Akili Zetu:

 

Tunapoteza kwa vitu visivyo na manufaa, ambavyo vinaleta hasara kwa jamii na mtu binafsi, sio kwa mazingatio au kutafakari.

 

 

9.  Kazi Zetu:

 

Kupoteza kwa kumhudumikia mtu ambaye hatotuweka karibu na Allaah au japo kutunufaisha katika hii dunia.     

 

 

 

10.  Kumdhukuru Kwetu Allaah:

 

 

Tunazipoteza kwa sababu hazituathiri sisi au mioyo yetu.

 

 

 

Share