Malfuuf (Mviringisho) Wa Wali Na Nyama Katika Kabeji
Malfuuf (Mviringisho) Wa Wali Na Nyama Katika Kabeji
Vipimo:
Kabeji - 1
Mchele - 1 kikombe
Nyama ya kusaga - 1/4 Pound
Kitunguu saumu(thomu/galic) na tangawizi iliyosagwa - 1 kijiko cha chai
Pilipili mbichi iliyosagwa - 1 kijiko cha chai
Kitunguu - 1
Parsely - 1 msongo (bunch)
Nyanya - 1
Garama Masala (au bizari mchanganyiko) - 1 kijiko cha chai
Chumvi - kiasi
Vifaa Vya Kutia Katika Kupika Malfuuf:
Kidonge cha supu (Stock cube) - 1
Samli au mafuta - 1 kijiko cha supu
Nyanya ya kopo - 1 kijiko cha chai
Nyanya kata ndogo ndogo - 1
Namna Ya Kutayarisha Na Kupika:
- Chambua majani ya kabeji moja moja yasikatike.
- Chemsha maji tia chumvi kidogo, kisha tia majani ya kabeji kwa dakika moja yalainike. Epua, chuja na weka kando katika sinia.
- Osha mchele, urowanishe muda kidogo.
- Katakata kitunguu, nyanya na parsely ndogo ndogo.
- Changanya nyama na thomu, tangawizi, pilipili, kitunguu, nyanya, parsely, bizari na chumvi.
- Kisha changanya pamoja na mchele ikiwa tayari kwa kujazia katika kabeji.
- Tandaza jani la kabeji kisha utie mchanganyiko uliotayarisha na uviringishe. Tazama picha.
- Panga kabeji zote katika sufuria kisha utie maji kiasi yasifikie kufunika kabeji.
- Tia kidonge cha supu, samli, nyanya uliyokata ndogo ndogo na nyanya kopo.
- Funika upike moto mdogo mdogo hadi maji yakaribie kukauka.
- Epua, na panga kabeji katika sahani zikiwa tayari kuliwa.