Mpunga Wa Nazi Kwa Mchuzi Wa Nyama Ng’ombe Na Mchicha
Mpunga Wa Nazi Kwa Mchuzi Wa Nyama Ng’ombe Na Mchicha
Wali (mpunga unaonukia)
Mchele - 4 Vikombe
Tui la nazi - 6 vikombe
Chumvi - kiasi
Namna Ya Kutayarisha Na Kupika
- Osha mchele
- Bandika tui jikoni likichemka tia mchele na chumvi.
- Funika uchemke, tui likikauka wacha moto mdogomdogo hadi wali uive ukiwa tayari. Ikiwa unatumia mkaa unapalia juu yake.
Mchuzi wa nyama Ng’ombe
Nyama - 1 kilo
Kitunguu saumu(thomu/galic) na tangawizi ilosagwa -2 viijiko vya supu
Viazi/mbatata - 2
Kitunguu maji kilokatwakawa (slice ndogo) - 2
Nyanya/tungule - 4
Nyanya kopo - 3 vijiko vya supu
Majani ya mchuzi/mvu - 3 msongo (bunches)
Bizari ya mchuzi (simba 2) - I kijiko cha chai
Ndimu - 1 kamua
Mafuta - ¼ kikombe
Chumvi - kiasi
Namna Ya Kutayarisha Na Kupika
- Weka nyama katika sufuri, tia kijiko kimoja cha kitunguu thomu na tangawizi, chumvi, ndimu na chemsha nyama hadi iwive na ibakie supu yake kidogo.
- Weka mafuta katika sufuri nyingine, kaanga kitunguu. Vinapogeuka rangi tia majani ya mchuzi endelea kukaanga hadi vigeuke rangi ya hudhurungi (golden brown)
- Tia nyanya/tungule, viazi/mbatata, endelea kukaanga mpaka nyanya ziive.
- Tia nyama na supu yake kisha tia nyanya ya kopo, kotmiri, bizari ya mchuzi, chumvi uache mchuzi kidogo katika moto hadi viazi viive vikiwa tayari.
Mboga Mchicha
Mchicha - 4 michano/vifungu
Kitunguu - 1
Kitunguu saumu(thomu/galic) - 3
Nyanya/tungule - 2
Tui la nazi zito - 1 kikombe cha chai
Chumvi
Namna Ya Kutayarisha Na Kupika
- Osha mboga iache ichuje maji.
- Ikatekate kisha weka katika sufuria.
- Katika kitunguu maji, kitunguu thomu kisage au kikatekate kidogodogo (chopped), nyanya.
- Weka jikoni ipikike kwa maji yake na mvuke.
- Tia tui endelea kuweka katika moto mdogomdogo hadi ikaribie kukauka ikiwa tayari.