Koshari Na Sosi Ya Kuku - (Misri)
Koshari Na Sosi Ya Kuku - (Misri)
Vipimo Vya Koshari
Mchele - 2 vikombe
Makaroni - 1 kikombe
Dengu za brown - 1 kikombe
Vitunguu vilokatwakatwa (chopped) - 2
Nyanya ziilokatwakatwa (chopped) - 4
Nyanya ya kopo - 1 kijiko cha supu
Kitunguu saumu(thomu/galic) ilosagwa - 1 kijiko cha supu
Pilipili mbichi ilosagwa - 1 kijiko cha chai
Pilipili manga ya unga - 1 kijiko cha chai
Mdalisini kijiti - 1
Bizari ya pilau (cumin seeds) - 1 kijiko cha supu
Hiliki - 2 chembe
Mafuta - 3 vijiko vya supu
Chumvi - kiasi
Vipimo Vya Kuku
Kuku - 3 LB
Kitunguu saumu(thomugalic) na tangawizi - 1 kijiko cha supu
Mtindi (yoghurt) - 1 kijiko cha supu
Pilipili ya masala nyekundu - 1 kijiko cha chai
Bizari upendazo - 1 kijiko cha chai
Ndimu - 1
Vitunguu slesi vilokaangwa - 3
Namna Kutayarisha Kuku
- Kata kuku vipande vikubwa kiasi, osha, weka kando achuje maji.
- Changanya vipimo vya kuku pamoja katika kibakuli.
- Changanya pamoja na kuku, roweka muda wa kiasi nusu saa au zaidi.
- Mchome (grill) kuku hadi aive weka kando.
Namna ya Kutayarisha Koshari
- Tia mafuta katika sufuria, kaanga vitunguu hadi viive kuwa rangi hudhurungi.
- Tia thomu ,mdalisini, bizari ya pilau na hiliki kaanga tena kidogo.
- Tia nyanya, pilipili zote, nyanya kopo, chumvi changanya vizuri ukaange kidogo.
- Epua sosi acha kando.
- Chemsha dengu pamoja na kidonge cha supu ziive nusu kiini na ibakie supu yake. Muda wa kuchemsha dengu inategemea aina yake.
- Tia mchele uchanganyike, funika, pika hadi uive vizuri pamoja na dengu
- Chemsha makaroni hadi yaive , epua chuja maji.
- Changanya pamoja wali wa dengu na macaroni.
- Pakua katika sahani, kisha weka juu yake kuku aliyechomwa, mwagia vitunguu vilokaangwa, kisha mwagia sosi.