Kufuturu Kabla Ya Kuswali Magharibi Inafaa?

 

SWALI:

A'Kumww maulamaa hukunilipo mambo ni tofauti nalivyokuwa east africa na watu huwa na tabia ya kufturu kwanza kisha ndo sawla ya magharib

 


JIBU:

Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu 'anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.

Kufuturu kabla ya kula, ni muhimu ujue kufuturu haswa ni kule kufungua kinywa wakati unapoingia tu wakati wa Magharibi. Hivyo, wanavyofanya hao ndugu zako kula kabisa kabisa hadi washibe, kuna hatari ya kuwachelewesha kuswali Swalah ya Magharibi ingawa haikatazwi kufanya hivyo ikiwa hawatoichelewesha Swalah ya Magharibi. Ama baada ya Swalah ndio vizuri kula chakula cha kushiba kwa wasaa wake mtu bila kuwa na wasiwasi wa Swalah au kuharakisha mlo wake na kumfanya mtu kula kwa pupa bila utulivu

 

Hadiyth ifuatayo imetuonyesha umuhimu wa kuwahi kufuturu (kufungua kinywa) pale tu wakati unapoingia bila kuchelewesha kabisa.

 

  لا تزال أمتي بخير ما عجَّلوا الإفطار -  رواه الإمام أحمد .

((Ummah wangu utabakia katika kheri watakapokimbilia kufuturu)) [Imaam Ahmad]

Tunakuombea Swawm nyepesi na yenye kutakabaliwa huko ulipo inshaAllaah.

Na Allaah Anajua zaidi

 

 

Share