Mke Anamsikiliza Kaka Badala ya Mume – Na Kisha Anaomba Talaka

 

SWALI:

mungu ajaleye wene kushugulekeya website hi kila la kheri kwa bidi wanavofana kutowa nasiha za kidini zitamfa mweslamu katika maesha yake

Mimi nimiowa kabla ya miezee enee, imitokeya problem kabla weeki tatu na mke wangu,(mke wangu alikuwa anampendeleya sana ndugu yake kwa kila kitu utasema kwamba mimi siyo mume waki) na shemedi yangu kangeleya katika problem, badalaa kutenegeneza kavuruga, shemedi umtu kaanza kutowa masharti ya kipuzi unaweza kusema tamma ya pesa, mradi mimi nimizikataa, sasa mke wangu na ndugu yake nimiwasafirisha kwa mama yao ili labda watatuleya, lakini hamna faidi mke wangu kaomba talaka bila sababu, na wamianza kusingizeya kwamba tumiwadulumu na wamianza kuwasema wazazi wangu na wamitukana matusi mabaya, sasa nikimpa mke wangu talaka sitokuwa nimidulumu, hata kama kaomba msamaha kwa makosa makubwa aliofana.



 

JIBU:

Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu 'anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.

Shukrani zetu za dhati kwa ndugu yetu aliyetuuliza swali lake kuhusu mas-ala ya talaka. Hii ni shida inayopatikana mara nyingi pindi uchaguzi katika ndoa haukufuata msingi wa Dini ya Uislamu.

Uislamu umetupatia muongozo kabambe kabisa kwa mume anayetaka kuoa na pia mke anayetaka kuolewa. Kushindwa kwa hao wawili kufuta muongozo huo ndio kunatokea matatizo kama hayo ya watu kutusiana na baadaye mmoja wao huenda akajuta lakini majuto huwa hayana faida tena.

Makosa mengine yanayofanywa ni mtu bila ya sababu yoyote kumchukua shemeji na kumuweka kwake. Shemeji huyo ambaye hana kazi wala hataki kazi anakuwa ni vurugu katika ndoa ya wanandoa. Hakika ni kuwa ni lazima mtu anayefanyiwa ihsani asiwe ni mwenye kuvunja au kuvuruga nyumba ya watu walioshikanishwa katika fungano ya ndoa. Ndugu yangu hakika umechelewa kuwasilisha tatizo lako mpaka limetupa mpaka na kuwa vigumu kurekebisha.

Ndugu yote kwa yote uliyofanyiwa inafaa uvumilie na usamehe kwani kufanya hivyo unapata daraja kubwa mbele ya Allaah Aliyetukuka. Allaah Aliyetukuka Anasema: “Na ni nani mbora wa kusema kuliko aitaye kwa Allaah na akatenda mema, na akasema: Hakika mimi ni katika Waislamu? Mema na maovu hayalingani. Pinga uovu kwa lilio jema zaidi. Hapo yule ambaye baina yako naye pana uadui atakuwa kama rafiki jamaa wa kukuonea uchungu. Lakini hawapewi wema huu ila wanao subiri, wala hawapewi ila wenye bahati kubwa” (41: 33 – 35).

Hivyo lipa uovu uliotendewa kwa kufanya wema na InshaAllaah Allaah Aliyetukuka Atakupa yaliyo mazuri na mema hapa duniani na Kesho Akhera.

Tunakushauri kabla ya kutoa talaka jaribu kutafuta suluhu baina yako na mkeo kwa kwenda nyumbani kwao na kujaribu kuzungumza na wazazi wake. Kama ikishindikana kupata muafaka hutakuwa na dhambi wala kufanya dhuluma kutoa talaka hiyo. Bali atakaye hasirika ni mkeo kwa kuomba talaka bila sababu yoyote.

Tunakutakia kila la kheri na mema na mafanikio.

 

Na Allaah Anajua zaidi

Share