Mwanamume Niliyezini Naye Ananitangazia Nami Nimetubu Nifanyeje?
SWALI:
naomba ushauri kuhusu matatizo ya liyo nikabili hapo awali .maana kila mja anaenifaham na asie nifaham ananiona mchafu.kwasa babu nilitembea na mume wa rafikiyangu ila nijambo ambalo owo nikitendo ambacho kilinihuzunisha sana na kujutia maisha yangu kwanza ninafaham ni dhambi ila sikuona hayo nilijitahidi kumuomba mwenzangu msamaha akanissamehe ila mumu wake ananichafuwa na kuzidi kunitia aibu hayoyote sababu nilimkatalia kwenda nae maranyingine ikaleta chuki.sasa nifanyeje iliniyaepuke hayo mwenyeezimungu anisaidie.naomba msada wenu maulam wabillahi taufiq.
JIBU:
Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu 'anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.
Tunasikitika kusikia hali yako hiyo ya majuto kufanya maovu kisha mtu uliyefanya naye maovu anakupaka sifa mbovu. Hii ndivyo hali ya kawaida inavyokuwa kwa kila mwanamke anayezini kwani bila ya shaka mwenye kuzini naye atakudharau na ataendelea kukudharau hadi atakavyo mwenyewe na hakuna wa kumzuia. Hili ni zingatio kubwa lipasalo kuzingatiwa na kila mwanamke Muislamu.
Haya makosa hutokea
Anaposema Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala):
((وَلاَ تَقْرَبُواْ الزِّنَى إِنَّهُ كَانَ فَاحِشَةً وَسَاء سَبِيلاً))
((Wala msikaribie uzinzi. Hakika huo ni uchafu na njia mbaya)) [Al-Israa: 32]
Uchafu na njia mbaya ndiyo kama hayo yaliyokusudiwa kuwa baada ya kuzini hubakia mja katika hali ya uchafu hiyo na matokea maovu ni kama hayo yaliyokufika kuwa na doa la kuzini na kuharibu heshima na stara yako.
Shaytwaan pia naye yuko karibu kabisa na waja kuwaingiza katika maovu hayo, na hutafuta kila njia za kukukaribisha katika maovu hayo. Kama ilivyokuwa katika hali yako ulikuwa hupasi wewe kuishi na mume wa rafiki yako katika nyumba moja kwani
Ikhtilaatw (Kuchanganyika Wanaume Na Wanawake)
Lakini kwa vile sisi ni binaadamu na kufanya makosa ni jambo la kawaida basi la muhimu ni kuwa pale mtu anapokosea inampasa kurudi kwa Mola wake Ambaye Yuko tayari kabisa kupokea tawbah yake. Na hivyo ndivyo inavyoelekea kwako kutaka kurudi, hivyo nayo ni neema kutoka kwa Mola wako kuwa umewahi kutambua makosa na dhambi zako kabla ya kufikia wakati ambao tawbah hazipokelewi tena au kabla ya kuondoka duniani.
Sasa iliyobakia ni kufanya tawbah ya kweli na uzidishe mema mengi, khaswa uzidishe ibada kama kuswali na kufunga Sunnah kwani mema kufuta maovu
((وَاَقِمِ الصَّلاَةَ طَرَفَیِ النَّهَارِ وَزُلَفًا مِّنَ اللَّیْلِ اِنَّ الْحَسَنَاتِ یُذْهِبْنَ السَّیِّئَاتِ ذَلِکَ ذِکْرَی لِلذَّاکِرين))
((Na simamisha Swalah katika ncha mbili za mchana na nyakati za usiku zilizo karibu na mchana. Hakika mema huondoa maovu. Huu ni ukumbusho kwa wanaokumbuka)) [Huud: 114]
Ingia katika kiungo kifuatacho usome mada muhimu zilizomo humu:
Yaliyopita yote maovu ya mja, husamehewa madhambi yake ila ajitahidi asirudie tena kwani kurudia tena itakuwa ni kupata ghadhabu za Mola
((عَفَا اللّهُ عَمَّا سَلَف وَمَنْ عَادَ فَيَنتَقِمُ اللّهُ مِنْهُ وَاللّهُ عَزِيزٌ ذُو انْتِقَامٍ))
((Allaah Amekwishayafuta yaliyopita; lakini atakayefanya tena Allaah Atamuadhibu. Na Allaah ndiye Mwenye nguvu na Mwenye kuadhibu)) [Al-Maaidah: 95]
Ama kuhusu huyo mwanaume kukufedhehesha,
Naye kupita kukuchafua pia kwa upande mwengine ni kheri yako kwani kila anapokutaja nyuma yako ambayo huwa ni kusengenya, basi anakubebea dhambi zako. Na kila anapoendelea huwa hivyo hivyo hatimaye itakuwa ni kupewa wewe thawabu zake hadi abakishwe hana amali njema bali madhambu matupu.
Nasaha yetu ya mwisho na ya dhati ni kuwa endelea kushika dini yako sawa sawa, kufuata amri za Mola wako, na kujieupusha kabisa na Shaytwaan asikutelezeshe tena ukapotea na zidisha
Na Allaah Anajua zaidi