Amembusu Mke Wa Mtu, Anajuta Na Ametubu, Je, Amjulishe Mume Wa Huyo Mwanamke? Na Mwanamke Bado Anamtaka
SWALI:
Assalam alaikum. Suala langu nikua nina rafiki yangu kaniuliza swali nikashindwa kumjibu. Anauliza: je kumbusu mke wa mtu na unajua
JIBU:
Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.
Shukrani zetu za dhati kwa swali lako kuhusu kumbusu mke wa mtu.
Ni hakika kutokana na maelezo yako kuwa umefahamu alilofanya si sawa kishari’ah.
Allaah Aliyetukuka Anatuhimiza
Kwa maasiya yoyote kusamehewa inatakiwa afanye toba ya kweli kweli, bila ya hivyo atakuwa bado ana dhambi. Ama ikiwa dhambi aliyofanya inahusisha heshima au haki ya mtu ni lazima atimize masharti manne kabla ya kusamehewa. Masharti yenyewe ni
1. Ni kuacha maasiya hayo.
2. Kujuta kwa kufanya.
3. Kuazimia kutorudia tena madhambi hayo.
4. Kumuomba msamaha mwanaadamu aliyemfanyia makosa.
Kukosekana moja katika masharti haya, toba yake itakuwa haijakamika. Bila shaka upo msingi muhimu wa Fiqh ambao unasema: “Dhara dogo katika madhara mawili”. Huenda katika kwenda kumwambia mume kukatokea dhara kubwa la kuachwa mke au kupata madhara mengine kutoka kwa mume.
Katika hofu hiyo ataacha kumwambia mume kuhusu yaliyotendeka huku akimuomba
Ama akiwa ana habari kuwa mume huyo amepata habari kuhusu hayo yaliyotendeka itabidi awe jasiri wa kumkabili amwambie yaliyojiri pamoja na kumtaka msamaha.
Hata hivyo, inatakiwa tuwe na tahadhari
Kwa kuwa nduguyo amekwambia amejuta
Na Allaah Anajua zaidi