Baada Ya Kupata Hedhi Kisha Damu Humtoka Kidogo Kidogo Kwa Masiku Zaidi

 

SWALI:

Mie huwa naenda siku nne (4) natumika katika hedhi, lakini niogapo udhu, bado damu inatoka kidogo kidogo sana kwa siku kama kumi (10) inanipelekea kunifanya niwe naswali adhuhuri nikitenguka naacha alasiri nk.  Yawezekana ni ugonjwa bado sijajua, je ili niwe na uhakika nihesabu siku ngapi nimalizapo hedhi  za kisheria ili niwe na udhu, niweze kuswali ,kufunga n.k

Kheir nawaombea kwa Allah, amiiiin

wenu


 

 

JIBU:

Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.

Shukrani zetu za dhati kwa dada yetu uliyeuliza swali hilo muhimu kuhusu damu ya ada iliyo na utata kama ulivyoeleza. Ama kuhusu hilo yapo mambo ambayo tunafaa tuyaangalie ili tupate hukumu muwafaka. Mambo yenyewe ni kama yafuatayo:

  1. Ikiwa unaweza kutofautisha baina ya damu yako ya hedhi na damu nyingineyo, utaangalia hii damu ikiwa rangi, harufu na twabia (maumbile) yake ni kama ya hedhi au ni tofauti. Ikiwa ni kama ya hedhi basi utabaki katika makatazo ya kuswali, kufunga na kujimai na mumeo kama ulivyokuwa. Kwani hakuna muda maalumu wa mwisho wa hedhi. Ukipata damu ambayo ni kinyume na kawaida ya hedhi yako, utaoga na kuswali kwani hiyo haitakuwa ni ada ya hedhi yako.

  2. Ikiwa huwezi kutofautisha baina ya hedhi na damu nyingineyo, na jambo hili linapatikana kwa wanawake wengi, utabaki katika hali ya hedhi. Hivyo, hutaswali, hutafunga wala kujamiiana na mumeo mpaka utwaharike kwani hakuna mipaka ya muda kwa damu ya hedhi.

  3. Ama ule umanjano na kufifia kwa rangi ni maji anayoona mwanamke kama usaha na umanjano wake umeiva. Mwanamke anapoona hii baada ya kukatika damu au baada ya kukauka, haichukuliwi kuwa ni hedhi, naye atakuwa twahara. Kwa hiyo, ataswali, atafunga na kuweza kujamiana na mumewe. Hiyo ni kwa mujibu wa Hadiyth ya Umm ‘Atwiyah (Radhiya Allaahu ‘anha) aliyesema:

  4. Tulikuwa hatuchukulii kufifia kwa rangi na umanjano chochote” (Abu Daawuud, an-Nasaaiy na Ibn Maajah).

Bonyeza viungo vifuatavyo upate maelezo zaidi:

Damu Ya Hedhi Inayoendelea Kwa Muda Mrefu

Istihaadhwah (Damu Inayoendelea baada ya Hedhi) Na Hukumu Zake

 

Na Alaah Anajua zaidi

 

Share