Kabeji Ya Kukaanga
Kabeji Ya Kukaanga
Vipimo:
Kabeji - ¼ kabeji
Karoti - 2
Kitunguu - 2 viwili
Nyanya - 1
Nyanya ya kopo - 1 kijiko cha chai
Pilipili mboga - ½
Chumvi - kiasi
Pilipili manga - ½ kijiko cha chai
Bizari ya manjano - ¼ kijiko
Pilipili zilorowekwa katika siki
(hot pepper rings) - 2 vijiko vya supu
Mafuta - 2 vijiko vya supu
Namna Ya Kutayarisha Na Kupika
- Katakata kabeji, karoti, vitunguu, pilipili mboga, nyanya weka kando.
- Tia mafuta katika karai kaanga vitunguu hadi vilainike na kuanza kugeuka rangi. Usiache vikageuka rangi sana.
- Tia nyanya, nyanya ya kopo, chumvi, pilipili manga, bizari, endelea kukaanga kidogo.
- Tia karoti endelea kukaanga kidogo.
- Tia kabeji na pilipili mboga kaanga kidogo tu.
- Zima moto na changanya na pilipili zilokatwakatwa na kurowekwa katika siki (hot pepper rings) ikiwa tayari kuliwa.