Wazazi Wa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) Ni Watu Wa Janna (Peponi) Au Motoni?

 

 

Wazazi Wa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) Ni Watu Wa Jannah (Peponi) Au Motoni?

 

Alhidaaya.com

 

 

                                                   

 

 

 

SWALI:

 

Ustadh nilikuwa nataka kuuliza kuhusu baba na mama yake Nabii Muhammad (s.w) ni watu wa motoni au wa peponi?

 

 

JIBU:

 

 

AlhamduliLLaah Himidi Anastahiki Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) Rabb wa walimwengu, Swalaah na Salaam zimshukie Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhwiya Allaahu 'anhum) na waliowafuata kwa wema mpaka Siku ya Mwisho.

 

 

Kwanza kabla hatujajibu swali lako, tunakunasihi kutokufupisha kumswalia Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam). Bonyeza viungo vifuatavyo upate maelezo:

 

Hukmu Ya Kufupisha Thanaa (Kumtukuza Allaah) Na Kumswalia Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam) Na Maamkizi Ya Kiislam

 

Al-Lajnah Ad-Daaimah: Haijuzu Kufupisha Kumswalia Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) Katika Maandishi

 

Imaam Ibn Baaz: Kufupisha Kumswalia Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) Kwa Mfumo Wowote Haijuzu

 

 

Hakika ni kuwa tunapata Hadiyth kutoka kwa Abu Hurayrah (Radhwiya Allaahu ‘anhu) kuwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alisema: “Niliomba ruhusa kutoka kwa Allaah kumuombea maghfirah mamangu, lakini Hakunipatia. Nikamuomba idhini nilizuru kaburi lake (mamangu), Naye Akanipatia ruhusa” [Muslim]

 

Kukatazwa huku kwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) ni kwa sababu ya mama yake kutokuwa Muislam. Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) Anatufahamisha:

 

مَا كَانَ لِلنَّبِيِّ وَالَّذِينَ آمَنُوا أَن يَسْتَغْفِرُوا لِلْمُشْرِكِينَ وَلَوْ كَانُوا أُولِي قُرْبَىٰ مِن بَعْدِ مَا تَبَيَّنَ لَهُمْ أَنَّهُمْ أَصْحَابُ الْجَحِيمِ﴿١١٣﴾

Haimpasi Nabiy na wale walioamini kuwaombea maghfirah washirikina japokuwa ni jamaa zao wa karibu baada ya kuwabainikia kwamba wao ni watu wa moto uwakao vikali mno. [At-Tawbah: 113]

 

 

Ifahamike kuwa baba na mamake Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) hawakuwa Waislamu nao waliaga dunia katika ukafiri. Ama kuwa wataingia Motoni au Peponi hilo ni la Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) kuwasamehe au kuwaadhibu. Hii si ajabu kwani babake Nabiy Ibraahiym (‘Alayhis Salaam) hakuwa Muislamu ndio akaagiziwa:

 

وَمَا كَانَ اسْتِغْفَارُ إِبْرَاهِيمَ لِأَبِيهِ إِلَّا عَن مَّوْعِدَةٍ وَعَدَهَا إِيَّاهُ فَلَمَّا تَبَيَّنَ لَهُ أَنَّهُ عَدُوٌّ لِّلَّـهِ تَبَرَّأَ مِنْهُ ۚ إِنَّ إِبْرَاهِيمَ لَأَوَّاهٌ حَلِيمٌ ﴿١١٤﴾

Na haikuwa Ibraahiym kumuombea maghfirah baba yake isipokuwa kwa sababu ya ahadi aliyoahidiana naye. Lakini ilipombainikia kwamba yeye ni adui wa Allaah, alijiepusha naye. Hakika Ibraahiym ni mwenye huruma mno na mvumilivu. [At-Tawbah: 114]

 

 

Na Allaah Anajua zaidi

 

 

Share