Mwenye Kuhudumia Kituo Cha Mafuta (Petrol Station) Anafaa Kumjazia Mafuta Mteja Aliyebeba Ulevi?
SWALI:
Ama ndugu zangu nina swali moja linani tatiza Mfano mimi nina petrol station au jaalia wewe ndio mwenye hiyo petrol station au ni ya ndugu yako na kuna siku na wewe huwa na kawaida ya kumsaidia. Sasa linakuja gari la
Nategemea fatawa nzuri kutoka kwenu wabillah tawfiq alkm
JIBU:
Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.
Shukrani zetu za dhati kwa swali lako kuhusu biashara. Bila shaka inaeleweka kuwa biashara ina nidhamu zake katika sheria ya Kiislamu. Haifai kwa Muislamu kuuza kitu kilicho haramu wala kusaidia katika uovu. Allaah (Subhaanahu wa Ta‘ala) Anasema:
“Na saidianeni katika wema na ucha Mungu. Wala msisaidiane katika dhambi na uadui. Na mcheni Allaah. Hakika Allaah ni Mkali wa kuadhibu” (5: 2).
Kwa hiyo unapolihudumikia gari lenye kuuza pombe utakuwa umeshiriki katika kueneza ulevi kwa watu na sehemu tofauti. Hivyo haitakuwa sawa kwako kuliuzia mafuta gari
Na Allaah Anajua zaidi