Kuvaa Kanzu Ni Sunnah? Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) Alikuwa Akivaa Mavazi Gani?
SW
Assalam aleykum sheikh wangu.. swali langu la leo naomba unitowe dukuduku langu.. je..! huku kuvaa kanzu ni sunna au ni vazi tu
JIBU:
Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.
Kwanza kabla hatujajibu swali lako, tunakukumbusha kuwa unapoandika jina la Allaah au Mtume, usifupishe mbele yake kwa kuweka (S.W.) au (S.A.W.)
Shukrani zetu za dhati kwa swali lako kuhusu mavazi ya Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam). Inafahamika vyema kwa kila mmoja wetu Muislamu na asiyekuwa Muislamu kuwa Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) asili yake alikuwa Mwarabu. Katika maisha yake aliishi (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) katika mazingira ya Kiarabu na vazi
Kwa kulichukua kubaki vazi la kanzu kuwa ni vazi
Mbali na kusema hayo, Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) kuusahilishia Ummah wake katika mambo mengi na mavazi vile vile alikuwa na mavazi tofauti
Baadhi ya Hadiyth zinazoelezea hayo ni:
§ Imepokewa kwa Ibn ‘Abbaas (Radhiya Allaahu ‘anhuma) kwamba Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: “Vaeni katika nguo zenu nyeupe, kwani hizo ni katika nguo zenu zilizo bora kabisa na pia muwakafini nazo maiti zenu” (Abu Daawuud na at-Tirmidhiy, na akasema ni Hadith Hasan Swahiuh. Isnadi yake ni Sahihi na ameisahihisha Ibn Hibbaan).
§ Na amesema Abu Ramthah Rifaa‘ah at-Taymiy (Radhiya Allaahu ‘anhu): Nilimuona Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akiwa na nguo mbili za kijani (Abu Daawuud na at-Tirmidhiy kwa Isnadi iliyo Sahihi. Pia imenukuliwa na an-Nasaa’iy, na Isnadi yake ni Sahihi).
§ Na imepokewa kwa Jaabir (Radhiya Allaahu ‘anhuma) kwamba Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) aliingia siku ya kufunguliwa Makkah akiwa na kilemba cheusi (Muslim).
§ Na amesema mama wa Waumini ‘Aaishah (Radhiya Allaahu ‘anha): Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amevishwa sanda ya nguo tatu nyeupe zilizotengenezwa Sahuuliyyah (aina ya nguo kutoka kijiji hicho cha
§ Na amesema Mughiyrah bin Shu‘bah (Radhiya Allaahu ‘anhu) kwamba: Usiku mmoja tulikuwa katika safari pamoja na Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) …Wakati huo alikuwa amevaa juba la sufi na hivyo hakuweza kutoa mikono yake mpaka alipoitoa kutoka katika sehemu ya chini ya
§ Amesema Ummu Salamah (Radhiya Allaahu ‘anha): Ilikuwa nguo bora kwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) ni kanzu (Abu Daawuud na at-Tirmidhiy, na akasema hii ni Hadyith Hasan).
§ Na imepokewa kwa Ibn ‘Umar (Radhiya Allaahu ‘anhuma) kwamba Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: “Allaah Hatawaangalia wale watu walioburuza (zikavuka mafundo ya miguu) nguo zao
§ Na imepokewa kwa Abu Hurayrah (Radhiya Allaahu ‘anhu) kwamba Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: “Allaah Hamuangalii mwenye kuburuza (kuvaa nguo yenye kuvuka mafundo ya miguu [Isbaal]) nguo yake kwa kiburi” (al-Bukhaariy, Muslim na Maalik).
Kwa mujibu wa Hadiyth hizi tunapata kuwa vazi bora
i. Vazi lisiwe ni lenye kubana.
ii. Vazi lisiwe ni la kuonyesha ndani.
iii. Kutoburuza nguo aina yoyote kwa mwanamme [Isbaal - kuvuka mafundo ya miguu].
iv. Kutosifu umbile lake (lisimbane).
v. Lisifanane na vazi la kike.
vi. Lisifanane na vazi la makafiri.
vii. Lisiwe vazi la kifakhari, umaarufu, na mitindo [fashion].
Na Allaah Anajua zaidi