Nani Mwenye Haki Ya Mtoto Mke na Mume Wanapoachana

SWALI

 

asalam alekum

nataka kujuwa kuhusu mtoto wa kiume kama baba na mama wamewatana na mke ameolewa na mume mwengine na baba haki hapo nchini mtoto ana haki baba amtukuwe mtoto kwa mamake ampeleke kwa ndugu yake na mamake baba ni sawa kunyangajwa mama toto nataka kujuwa kama ni haki kwa sababu makadhi wa kwetu kenya wanasema  baba ana haki  nataka kujuwa  kama nihaki shukran mngu awajazi kwa kuwaweka watu kama nyinyi kutusaidia matatizo yetu tulio mbali masalam


 

JIBU

 

Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.

 

Shukrani zetu za dhati kwa swali lako kuhusu ulezi. Hakika ni kuwa mtoto akiwa mdogo mama ana haki zaidi ya kumlea/ kuwalea baada ya kuachana na hasa akiwa/ wakiwa wananyonya. Mtoto anapopata fahamu anapatiwa uchaguzi anataka kwenda kwa baba au mama. Hii ikiwa mwanamke hajaolewa na mume mwengine lakini anapoolewa baba anakuwa na haki zaidi kwa mtoto kuliko mama mzazi.

 

Kitu ambacho unafaa kupigania labda ni kupatiwa fursa wakati mwengine uwaone na kukaa na mtoto/ watoto ili pia wawe ni wenye kukuzoea na wasiwe ni wenye kukusahau.

 

Twakutakia kila la kheri katika mafungamano yako mapya na mume mpya na Allaah Aliyetukuka Akutilie mahaba, tawfiki na Awadumishe pamoja.

 

Na Allaah Anajua zaidi

 

 

Share